Natamani sana kuacha pombe ila nashindwa

Natamani sana kuacha pombe ila nashindwa

Ni maamuzi tu wala hakuna haja ya kukaa mbali na wanywaji. Mimi nimekua toka mdogo nimezungukwa na walevi, wanywaji, wapiga vyombo, na wavuta sigara na bangi, class yetu olevel ilikua ya wapiga maji muda wote na mimi ndio nilikua nawapeleka vilabuni kupiga vyombo.

Nimefika advance mambo yalikua hayo hayo, tunatoroka kwenda kwenye vilabu vya pombe na washkaji, wanapiga wanazima nawakokita hadi bwenini, kote huko sijawahi kuigusa. Chuo kikuu the same, nikamaliza nikafanya kazi ya whole sales ya pombe za aina yote kwa bar na migahawa, nilikua nakesha bar, sijawahi kugusa.

Kwenye shughuli zangu za kila siku nimezungukwa wa walevi na wanywaji kila kona ila sijawahi kugusa.

Kunywa pombe, kuacha yote ni maamuzi, haihusiani kabisa na kwamba washkaji zako ni walevi basi na wewe unakua mlevi.

Hajaamua kuacha, akiamuq anaacha, ukiona anashindwa kuacha ni hajaamua.

Unachoongelea wewe ni tofauti na kitu kinaitwa Kuwa addicted..

Huyu ni mlevi tayari ambaye akiikosa Pombe muda flan, hamu yake inayomjia ni kubwa sana kujizuiya ni mtihan zaidi, sasa ukisema hakuna shida kuwa anaweza kukaa hata karibu na walevi eti ajiamulie asinywe ni uwongo)

Moja ya njia salama kwake ni kujikwepesha na kila njia ya kuweka ukaribu na kutumia kilevi.
 
Ifahamu pombe.png
 
Kuna kanuni inaitwa ppt, people place
Bia moja angalau dakika 30 ndo iwe imeisha, mfano mimi nikiwa nacheki movie , kuperuzi jf na x , au kusoma kitabu cha hadithi , ndio unakuta naburudika na pombe yangu mdogo mdogo .
Bia ukshafungua dkk 10 nyingi ishapoa, sasa dkk 30 c akuw unakunywa mikojo?
 
Akiishiwa tunampa, yuko wapi kwani nimsendie kreti ahangaike nalo weekend.....
Uzuri mmoja kama ananywea bar mpaka kutumia 100k kwenye pombe ni kiherehere chake tu kama anakunywa local bia hata 20 kuisha kwa mtu mmoja ni uongo , labda anajifanya pedeshee ndama mutoto ya ng'ombe.
 
Kabisa na ukinywa kwa makelele na ma vibe na walevi wengine lazima ugide kupitiliza ili uende nao sambamba , ushauri mzuri wa pombe apate kwa wanywa pombe na sio kwa walokole
Siwezi acha pombe kisa kupitiliza nikitoka na bajeti yangu haizid aani mambo ya kuzungukwa sjui na Hawa wanaojiuza hapana kwakweli,

Me naona nipo tofaut sana na watu pengine 😂
 
Uzuri mmoja kama ananywea bar mpaka kutumia 100k kwenye pombe ni kiherehere chake tu kama anakunywa local bia hata 20 kuisha kwa mtu mmoja ni uongo , labda anajifanya pedeshee ndama mutoto ya ng'ombe.
Nimeshangaa hata akinywa imported km Heineken 4,000 sita zinamtosha mbn
 
Wakuu mko salama?

Wakuu kiukweli mpaka nimeanza kujichukia kuhusu unywaji wa pombe. Mfano jana nimepiga maji hadi sijui nilirudije ghetto,sometimes kumbukumbu zinapotea sababu ya pombe, kiuchumi napo naathirika,yani naweza nikawa na ka laki moja kangu mfukoni,nikiingia bar tu hako kalaki kataisha na madeni juu.

Sasa asubuhi hii sijui ndo pombe jana nilizinywa nyingi au sijui ni nini nimeingia bafuni nimetapika sana.

Kwa kweli hii hali inanisononesha mno,natamani kuachana na huu unywaji lkn kila nikisema niache nitakaa siku mbili tu naanza tena.mfano leo nilipanga nisiguse pombe ila tayari kuna jamaa yangu ametoka kahama huko ana mpunga keshanambia jioni tukutane tupige vyombo.

Wakuu najinasuaje na unywaji huu wa tungi?
Umecheki naniliuu ipo Salama? Maana hujui hata ulirudije gheto. Nikushauri tu usipoacha pombe utaishia gheto hadi uzeeni. Kuitwa Baba mwenye nyumba sahau
 
Siwezi acha pombe kisa kupitiliza nikitoka na bajeti yangu haizid aani mambo ya kuzungukwa sjui na Hawa wanaojiuza hapana kwakweli,

Me naona nipo tofaut sana na watu pengine 😂
Kabisa , unakuta mziki wa hovyo kwenye spika zenye mende , mataa yana marangi ya hovyo , then mtu anagida local bia kwa fujo , hapo kashindia wali maharaka au chips kavu , lazima ulaumu pombe tu
 
Ulevi ni utumwa, mtu wkishakuwa mlevi hana tofauti na mla madawa ya kulevya. Unakuwa na msalaba wako kila siku umeubeba. Binafsi nina mifano mingi sana, watu wanajuta ila ndio hivyo hawawezi tena kuacha.
 
Kabisa , unakuta mziki wa hovyo kwenye spika zenye mende , mataa yana marangi ya hovyo , then mtu anagida local bia kwa fujo , hapo kashindia wali maharaka au chips kavu , lazima ulaumu pombe tu
Mbona pombe Ina chemistry rahisi mnaendana tuu, huyo dogo jau
 
Mimi kwa upande nikiwaga serious kwenye kipindi Cha maombi au kufunga au nikiwa karibu na mungu kipindi flani najikutaga automatic pombe naichukuia na naacha na hata zile kampani za pombe uwa hazinitafuti ZINAKIMBIA na hii kitu sio mara moja ni zaidi ya mara mbili na hapa uwezi amini nimemaliza mfungo Wangu wa mwezi mzima sijagusa pombe kwaiyo naimani ipo siku nitakuja KUACHA kabisa pombe nimeshaona njia sahihi ni kumpokea yesu akujaze roho mtakatifu ndio utaweza kuvuka ila hivi hivi Mzee utoboi shetani ana nguvu Sana
 
Bila shaka pombe ulianza kuzinywa ukubwani mkuu, nyie ndo wale ambao mlikuaga na washkaji wanapiga tungi mnawaona kama vile wanapotea sasa na ww life ikakuingiza kwenye mstari ukajikuta unazipiga mpaka zimekutalawa badala ya wewe kuzitawala.

Jifunze kuwa na kiasi anza pole pole ikibid ukisikia hamu ya tungi nenda kanunue mbili tatu kisha jitungue peke yako ukiwa home na sio bar, tafuta hobbies nyingine za kukuliwaza mfano movies, gym, reading books n.k . Najua washkaji ni ngumu kuwakwepa hasa wakiwa wanakupa michongo ila jitahidi uwe na kiasi tu na vipaumbele vyako vianze kwanza kisha pombe ifuate.

#Mwanaume kuacha pombe ni Ufala na mwanaume kuruhusu pombe ikutawale ni ufalala vilevile. GAMBE NI MAISHA. kuwa na kiasi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom