Nataka Rais Magufuli ashindwe

Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
DAH, mkuu umeongea POINT sana ,tatizo watu wanaendeshwa ka mihemko badala ya kuufikirisha ubongo na tafakuri za kina,kweli kuna haja ya uwepo wa uhuru wa maoni tena mpana na usio na mwisho lakini uhuru huo usiwe wa mtu kaamka na mindoto yake anakuja humu anatoa stori za ajabu ajabu za kutunga tunga kisha aachiwe tu,

hata huko kwa wenzetu uhuru hupo ila wanautumia kwa nji ipasavyo,mfano kuna mijitu hapa Jf lazima kila siku iweke uzi ambao hauna kichwa wa miguu mradi tu naye aonekane ameweka uzi,kwa kweli ukifikiria sana unaona sisi wenyewe ndio tunajikosea heshima na kuifanya serikali itafute nji ya kuminya uo uhuru,ikumbukwe haijakatazwa kukosoa,kaa kukosoa tukosoe sana tena bila aibu wala hiyana yeyote lakini katika kosoa hiyo tuzingatia ukweli,staha na madhara ya huo ukosoaji wake,

wakati mwingine unasoma uzi unajiuliza huyu ni mtanania kweliii au ni pandikizi la mataifa jirani? ndugu zanguni machafuko ya Misri,Tunisia Libya na nchi nyingin za kiarabu kwa kaisi kikubwa yalitokana na watu kulishana matango pori juu ya serikali zao na hiyo ilikuwa ni mikakati ya nnchi za ng'ambo kuziharibu nchi za kiarabu,atokeo yake watu wakaamini propaganda na kuamua kujiweka rehani kwa kitu ambacho hakina ukweli wowote ule,leo hii hata hawajielewi .

Leo hii walibya wanalia,wamisri wanalia,watunisia wanalia ,wamepoteza ndugu na jamaa zao kwa ujinga ,kwa kudanganywa na kuchonganishwa,

Kuhusu suala la mmiliki wa Jf kukamatwa na leo inasemekana atafikiswa mahakamani,nazani watanzania hapa hatuahitaji kuwa kama WEHU,tusio jua nini maana ya mahakama,maadamu imebainika kile kilichosababisha akakamatwa na kuzuiliwa ndani ,vema tukawa watulivu huku tukiacha mahakama kazi yake ,ndio tuanze kuja na hayo malalamiko yetu mara baada ya maamuzi kutoka kwani ukitazama sheria Mmiliki wa JF na polisi wote wako sawa katika madai yao.

Mwisho watanzania nchi hii ni yetu sote,hakuna mwenye kusema hii ni nchi yangu,kama umezaliwa tanzania mkono wako wa kulia unaalama ya ndui,ni wajibu wako kuilinda tanzania dhidi ya wanapropaganda wanaoishi kwa kueneza maneno ya ajabu ajabu juu ya Tanzania,maneno ambayo hayana hata tone la ukweli.

Tukikubali hali hii mwisho wa siku tutajikuta tunalia na kujutia,mifano ya misri,libya na tunusia sio ya kubeza,tunachotakiwa kuzingatia hapa tusikubali yaliyotokea huko yanatokea hata hapa kwetu,japo kweli kuna baadhi ya maeneo ambapo serikali haijafanya vema lakini subra na utulivu ulio na uvumilivu vibaki kuwa mioyoni mwetu, wenzetu wa Ghana walivumilia mwisho akafanya maamuzi ya kistarabu na maisha yanaendelea,so na sisi hatuna budi kufanya hivyo kama tu tumewachoka watawala hawa tulio nao.
Mazingira yanayotengenezwa sasa ndio chachu na ramani ya kujenga mjengo wa kitunisia na kimisri japo wewe waona kuwa udikteta ndiyo kinga kwa yaliyotokea misri. We are building an evil society
 
Mkuu,huyu kiongozi sio mbaya ila kuna vitu vichache anakosea kama binaadam kwa kuruhusu mihemko yake binafsi iliyopitiliza kwenye mambo ya msingi,anatakiwa ajicontrol sana kwani mara nyingi jambo hili humuaribia,abadilishe mindset yake juu ya wanaomkosoa,naamini kwa uchapakazi wake akisikiliza hoja zao na kupata ushauri wa watu wake wa karibu anaowaamini zaidi,anaweza kutoboa sana,kwani sio wote wanaokukosoa hawana hoja,akilitambua hilo atafanya mambo makubwa sana

Akizipanga vizuri karata zake,anaweza kuwa the best president ever happened in our country
Nimefurahika sana kwa jibu baada ya kusoma majibu ya wadau hapo juu. Huu ndio ukosoaji wa kizalendo. Lakini tumumbwa tofauti lazima wadau kama hao hapo juu wawepo.
 
Nyani ngabu kwa mara ya kwanza, kwa jinsi ninavyokusoma na kukuelewa, aidha umeandika kwa hasira au ni bandiko la kuchokonoa mawazo ya wanaJF!

1) Unataka Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Kumbuka yeye ni Rais na nyuma yake anao milioni kadhaa ya wananchi waliomweka madarakani kwa kura zao. Kwa msingi huo, wewe na wenye mawazo kama wewe, mtashindwa na kulegea. Katiba ya JMT (1977) inampa madaraka makubwa kama unavyofahamu. Pamoja na hilo anawajibika kulinda haki na uhuru wa kila mwananchi, hata na wanaomwombea kushindwa na kulegea kama wewe.

2) Hakuna aliye juu ya sheria, hivyo mtu yeyote akivunja sheria, atafikishwa kwenye vyombo husika. Kama ulivyoandika "Haogopwi mtu zama hizi". Hata wewe Nyani Ngabu maandiko yako haya yakionekana yanaashiria kuvunja sheria ya mtandao, hutoogopwa. Hizi ni zama za utawala wa sheria.

3) Ukichemka nami nitakukusoa kama ninavyokukosoa kwa hoja zangu hizi. Ukichapia kiingereza nitakucheka, ila naamini utachapia tu kwa kuwa lugha ya kiingereza umeisomea darasani na kufundishwa na mwalimu ambaye pia siyo lugha yake ya asili.

4) Kwa hiyo nami nataka ushindwe na ushindwe kabisa kwa kudhani ndoto zako zinaweza kuwa kweli na maombi yako hayo kuhusu Yeye, yakurudie. Mwungwana humwombea binadamu mwenzake heri!

Mimi mdau hayo ndiyo yangu ninayosema.
Sheria IPI anayoilinda na iliyompa mamlaka ya kupiga marufuku mikutano ya halaiki ya vyama vya Siasa
Unaweza kuwa ulijitayarisha kwa kuweka Hoja nzuri. Lakini pale moyo unapotangulia akili ndipo palipo kukisesha Tu.
Sio mzimamizi mzuri wa sheria
Msimamizi mzuri wa sheria ni yule anayetumia sheria zinazomruhusu kutenda au kuacha kutenda huku akiheshimu zile zinazomkataza kutenda au kutotenda jambo
 
nyani ngabu ushindwe na ulegee. napenda uhuru wa habari ila sio wa kuwalinda wenye lengo la kuendeleza dhuluma kwenye jamii kufanikisha malengo yao. kwa kuonyesha chuki kwa jpm nahisi una maslahi na watumbuliwa wa ufisadi rushwa uzembe na ubadhilifu au mrija wa dili umekatwa.
NN sidhani kama ana maana alegee kwenye mapambano dhidi ya Ufisadi na uvivu lah. Mapambano dhidi ya wenye mawazo kinzani na yake ndio anayombewa ashindwe na alegee
Mapambano dhidi ya ufisadii Hureeeeee
 
Kaka ubarikiwe...vichwa vya namna hii ndio vinapaswa kuwa hapa JF.

Unajenga hoja yako bila dhihaka na matusi.

JF inaharibiwa na watu wachache ambao tafsiri ya uhuru wa kutoa maoni/mawazo kwao ni kujenga na kutoa propaganda za uongo zenye kujenga chuki na uhasama ktk jamii na wasiguswe. Kwakuwa taifa hili linaongozwa kwa mujibu wa sheria...inatupasa kutii sheria za nchi zilizopo hata kama sheria hizo hatuzitaki.

Haiwezekani uje hapa jukwaani ubwabwaje unavyotaka bila kupima athari za kauli zako halafu wakuache tu. Hio Serikali hata sisi wananchi tutaishangaa...haipo hapa duniani.

Uhuru bila mipaka ni fujo.

JF bila nidhamu ya kuongea ni fujo...tusikubali watu wachache wakatuharibia JF yetu.....
Where we dare to talk openly
JF yenu inaslogan gani ?
Amini ya kuwa jambo laweza kuwa la kijinga kwako kwa sababu Tu huna taarifa sahihi. Mkianza kuchuja mtachuja kwa kutegemea nini ?
Objectivity itakuwa wapi ? Chukua linalokufaaa achana na lisilokufaa wewe lakini kuna mty mahali au wakati furani litamfaa.
Maana ya uhuru wa kuroploka iko hapo Mkuu
 
Magufuli ana weakness kama Kiongozi. Lazima ajifunze ku-accommodate hata wale wanaompinga au wenye tofauti na mawazo yake. Kitu ambacho ni kigumu kwa viongozi wengi wa Africa.

Having said that, bado naamini kwa dhati kabisa Magufuli ana nafasi kubwa ya kuwa kiongozi bora Tanzania. Kwa sababu anaweka maslahi ya taifa mbele. Hatujawahi kuwa na Kiongozi wa namna hiyo.

Haya ya kukamata waandishi wa habari na mengine ya kuminya wigo wa demokrasia, yanazungumzika.
Uhuru wangu wa kufikiri na kusema ninachofikiri unapita umuhimu wa mengine yote. Mengine yote yangekuwa na maana kama angelinda uhuru wangu wa mawazo na kutoa niwaxacho pasipo kijibiwa kwa polisi kunikamata bali kwa mawazo pia
Kwenye Equation ya maendeleo ya taifa lolote uhuru wa kutoa maoni ndiyo msingi wa mafanikio katika nyanja zingine zote
 
endeleeni kubwabwaja tu...huu uzi ni kwa ajili ya wtu wnye green card
 
Magufuli naye ni binadamu ana mazuri yake na mapungufu, tusamehane kwenye mapungufu.
Ukiweza kumfanya atambue hilo utakuwa umetatua tatizo kubwa sanaaa
Wewe unawaza hivyo kuhusu yeye ! Je ? Na yeye anajitambua hivyo ?
 
Kuamini kuna maisha baada ya kifo ni umasikini wa fikira...the strongest will survive, that's why we have to fight for our rights mambo ya utalipiwa na mungu ni kukubali kuonewa ambalo ni kosa kikatiba.

In this occurrence we have different perception according to the thread..mfano kuna yule mama alie sema Binti wa mkulu alijiua, wakati tuliofahamu ugonjwa mpaka mauti tulibaki tumepigwa butwaa mzee wake wakati ule alihangaika sana kujaribu kunusuru maisha yake mmpaka kwa TB Joshua walifika then kuna mama zima linaleta uongo bado Max analilinda.
Sasa uzuri wa forum kama hii ni pale ambapo wewe unayejua kweli tofauti na ya mwingine unaweka ili wengine wapata chakula ya ubongo kukuchambueni hoja zenu. Kuzia hilo ni kufanya watu wasifikiri Bali wanene Yale wanayosikilizishwa Tu.
Hoja ijibiwe kwa hoja na sio kwa polisi na virungu. Personal attack kwa yeyote ziwe handled inavyotakiwa na watu waelimishwa namna ya kujadili na kuwakilisha mawazo pasipo kulenga nafsi
 
embu jaribu kufikiria hili,wewe unasingiziwa au unazushiwa jambo ambalo halipo,mfano unaambiwa jambo baya ambayo litakuchukia na hata kukukoseshea stasha mbele ya jamii,utachukuliaje? na wakati huo jamii tayar nimeshaanza kuamini juu ya hilo jambo na kuanza kuwa na mihemko nalo,si utachukia siyo? au utafurahi na kuona ni jambo la kawaida? tafakari kwanza usione kawaida wakifanyiwa wenzako ,wewe je?
Mfano
Sio jambo ukisema ni la uzushi ili mradi linakufedhejesha basi kweli linakuwa na uzushi. MTU akiandika kuwa ulibaka mtoto.wawza kusema la uzushi kwa kuwa Tu unatambua kuwa hukuonwa! Kusema kuhusu jambo hakulifanyi kuwa kweli kama sio kweli na halulifanyi kuwa la uwongo kama ni la kweli.
Truth is objective bro
 
mkuu, yote hayo yanakutoka kwa kuwa mkuu wa Jf amekamatawa na polisi au yanakutoka kwa kuwa unaagenda yako binafsi,binafsi nafurahi kwa kuwa unatumia uhuru wa kutoa yako ya moyoni hapa tena bila kusumbuliwa lakini bahati mbaya unautumia vibaya kwa kujaribu kuchanganya na mihemko ,yu mkini wewe ni shabiki wa upinzani umechukia magufuli kushinda ,lakini braza maneno au kauli uliyotumia kuonyesha hisia zako ni makali sana,kumbuka unayemshukia ni Rais wa nchi na hata kama wew hupendezwi naye sio kwamba unazuia kuonyesha hisia zako,lakini jaribu kuwa na staha ,jua kuna wenye mioyo kama wewe walimpenda na kumchagua na hata kama huyo lubuva alimpitisha jua na nyeye pia alimpenda ndio maana kampitisha ,

Braza uhuru huu tulionao wa walau kuandika hisia zetu tusiutumie vibaya kiasi hiki,kiasi cha kukosea heshima nafasi ya Urais kiasi hiki,Uungwana ni dawa kuliko mihemko
Hii tabia ya kutaka kuweka taasisi ya Urais juu ya kila kitu ni aina ya udhaifu na madhara yake ni makubwa sana.
Kama inakaliwa na binadam utukufu inaopewa ni batili ndugu yangu. Nakubaliana nawe kuhusu staha sio kwenda kwa rais pekee Bali kwa binadam wote kuwa na staha dhidi ya bibadam mwingine ypyote pasipo kihali hali take yoyote.
Tuache kujenga matabaka kwa kukuza taasisi kupita Mungu
Atheist wanayo haki na Mungu anawapenda pasipo kijali namna wanamsema au kumwandika
Kwa nini Taasisi ya Urais ambayo twamini iko chini ya Mungu ipewe utisho ambao Mungu hajajipa ?
 
Atokeee, tumemchoka jamani, kama vipi nipeni bomu nikajitoe mhanga, nipo tayari kwa sababu sina furaha yoyote duniani hapa,, nipeni bomu
Wewe ndiye mbaya kuliko. Hoja inajibiwa kwa hoja
Paza sauti habari ya kutumia vitu unavyosema ni matokeo ya ukichaaa ndugu yangu. Jenga hoja za kujenga na kurekebisha matumizi ya dhana dhidi ya binadam mwenzako ni ujuha perse
 
Dah...mambo yapo simpo tu...sheria iliishapitishwa na bunge....kazi ya polisi ni kuhakikisha sheria zinafuatwa ...Tatizo lipo wapi??..Hii sharia haiilindi serikali tu...pia mtu binafsi au Taasisi...sasa kama umevunja sheria halali unashitakiwa....unajitetea....mahakama inaamua....sasa hii fichaficha sijui hata ni ya nini.... 😡😡😡
Hivi kwa nini mlalamika awe Polisi, Mkamataji awe Polisi pia ?
Tunafanya nini Tz
 
Kushindwa kwa Magufuli ni kushindwa kwa watanzania wote, kufanikiwa kwa Magufuli ni mafanikio kwa watanzania wote. Nawaomba ndugu zangu tuweke utaifa mbele. Ni mawazo yangu lakini nisiwakwaze
Read between lines uelewe maana ya "ashindwe"
 
Wewe ndiye mbaya kuliko. Hoja inajibiwa kwa hoja
Paza sauti habari ya kutumia vitu unavyosema ni matokeo ya ukichaaa ndugu yangu. Jenga hoja za kujenga na kurekebisha matumizi ya dhana dhidi ya binadam mwenzako ni ujuha perse
Duh!

Mshikaji vipi?

Naona umeamua kweli kweli leo.
 
Ashindwe kwenye kuwaziba watu midomo au ashindwe kwenye kila jambo?
Naamini kwenye kuminya uhuru wa maoni kwa mapana yake Tu. Wanaofikiri kuwa ashindwe kufanya kazi njema hawajaelewa bandiko la NN
 
ni kweli mkuu... hapa kuna fikra pevu sana na zimewasaidia watawala wengi kujirekebisha. Lakin swala linakuja kwamba, kama kweli tunatoa mawazo ya maana kwa nini tunaogopa kungundulika na vyombo vya usalama? kwa nini kuwaficha vyombo vya usalama kama wakihitaji kujua nani kasema nini? Uoga huu unatoka wapi??

Tazama michango yangu yote katika jukwaa hili, sijawahi kumtukana mtu, hata nikitoa mawazo ya kuikosoa serikali naongea kwa staha, sina hofu yeyote ya kujulikana na vyombo vya usalama.

kabla ya kushambulia vyombo vya usalama tujipime wenyewe.. je tunaongea kwa staha au tunataka jamii forums liwe jukwaa la kujifichia matusi yetu kwa watu??

Max Mello nakuombea umalizane nao hao watu urudi kuendelea na shughuli zako, Mungu ni mwema, utatoka tu bro.
Umesahau kuwa kusema mtu wa chombo cha usalama kapokea Rushwa ni jambo Jema kwa mchukia Rushwa lakini ni jambo baya kwa asiyetaka ijulikane
Hoja ijibiwe kwa hoja watu wasifungwe midomo !
 
Unajua sio siri najaribu sana kumpenda Magufuli lakni nashindwa. Kuna baadhi ya mambo anafanya vizuri lakni mengi ni hovyo. Sisi sio wasukuma wote kuna makabila 120 na dini na wasiokuwa na dini. Nchi inahitaji busara zaidi kuongoza sio sifa za kijinga au hasira.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom