Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa.
Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.
Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu.
Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
Nyani ngabu kwa mara ya kwanza, kwa jinsi ninavyokusoma na kukuelewa, aidha umeandika kwa hasira au ni bandiko la kuchokonoa mawazo ya wanaJF!
1) Unataka Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Kumbuka yeye ni Rais na nyuma yake anao milioni kadhaa ya wananchi waliomweka madarakani kwa kura zao. Kwa msingi huo, wewe na wenye mawazo kama wewe, mtashindwa na kulegea. Katiba ya JMT (1977) inampa madaraka makubwa kama unavyofahamu. Pamoja na hilo anawajibika kulinda haki na uhuru wa kila mwananchi, hata na wanaomwombea kushindwa na kulegea kama wewe.
2) Hakuna aliye juu ya sheria, hivyo mtu yeyote akivunja sheria, atafikishwa kwenye vyombo husika. Kama ulivyoandika "Haogopwi mtu zama hizi". Hata wewe Nyani Ngabu maandiko yako haya yakionekana yanaashiria kuvunja sheria ya mtandao, hutoogopwa. Hizi ni zama za utawala wa sheria.
3) Ukichemka nami nitakukusoa kama ninavyokukosoa kwa hoja zangu hizi. Ukichapia kiingereza nitakucheka, ila naamini utachapia tu kwa kuwa lugha ya kiingereza umeisomea darasani na kufundishwa na mwalimu ambaye pia siyo lugha yake ya asili.
4) Kwa hiyo nami nataka ushindwe na ushindwe kabisa kwa kudhani ndoto zako zinaweza kuwa kweli na maombi yako hayo kuhusu Yeye, yakurudie. Mwungwana humwombea binadamu mwenzake heri!
Mimi mdau hayo ndiyo yangu ninayosema.