Nataka Rais Magufuli ashindwe

Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
mm nafuraia sana jamii f kwasababu nikiwa jukwaa la siasa nabishana na rais waziri wabunge nk kwasababu wapo na id fake Ila nikiwazidi onja ndiyo madhara yake haya
 
Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupashana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.

Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.

Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Max kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.

Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hizo azma yake iwe muhali.

Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.

Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.

Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.

Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.

Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.

Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.

Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
Mmmh kweli umechafukwa
 
nimesoma Kwa makini ila lengo nilitaka kuona Kwa wale wenye akili fupi Lumumba fc kama wamechangia Uzi huu, sikumuona MTU kama lizabon, yuko WAP? uwenda anaandika Uzi kuhusu lowasa si bureeee
 
Hatari mzeee

Ha ha ha ha kwi kwi kwi kwi
Jamaa kaniacha hoi bila mbavu kuwa huwa anashiriki mijadala na rais, mawaziri, wabunge nk lakini akiwazidi hoja wanataka wamshughulikie. Teh teh teh teh. JF uishi milele. Atakayekugusa akutane na maneno ya Lusekelo
 
Viroboto mliopo humu go and tell him that "We ain't scared"! Na tutakosoa tu.. Hamna namna nyingine
 
Nilisikia Jana Lisu anasema kuwa ule Ujumbe uliandika najuwa hata hili utaandika ila ukiendelea juwa utaandika ukiwa hauko huru..lakini kumbuka Melo yuko kikaangoni uda huu ili atoe email na namba za simu ya member akikosea kidigo tu nahisi wataanza na wewe
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom