Mkuu mkiwa mmezaliwa watoto tisa nyumba moja,wanne wakawa wanaishi mbali na watano mnaishi na familia,walio mbali wakawa wanakuja na hoja za mmojawenu anayewaongoza mliyemchagua hafai wakati haishi humo,pengine tayari ana familia yake inabidi mumtilie shaka,mbaya zaidi hatoi suluhisho ni nani anafaa ila mijadala yake ni kuharibu tu.Hata mkifarakana haishi hapo tena.Mfatilie huyu jamaa,ni mojawapo ambao ni kama wapo nje lakini maisha yamewashinda,ya huko waliko yamewashinda na ya wanakotokea(asili) yamewashinda.Mtu anayesema raisi aachie ngazi kwa kejeli kibao bila kujua gharama na yanayoweza kutokea nchi ambayo hakai ni wa kupuuza kwa gharama yoyote.Ndo maana nimekupa mfano wakati Chadema wanaandaa UKUTA alikuwa anashinikiza watu waandamane waingie mtaani wapigwe tu na wajeda.Fatilia post zake kila anachosema ni kama matokeo ya matakwa yake yawe + au - yeye hana la kupoteza.Bado unaona ni mtu wa maana kumsikiliza?,mtu anayeishi hapa hapa kuna vitu hawezi andika wala kuongea kama anajua madhara yake.Hebu mfatilie thread zake hata tatu au nne halafu nipe jibu mkuu.