Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupashana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.
Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.
Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Max kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.
Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hizo azma yake iwe muhali.
Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.
Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.
Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.
Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.
Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.
Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.
Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
Ashindwe vipi tena?
Watu huku mtaani wanafurahia maisha ya kutumbuliwa na "maisha ya kimalaika".
Huyu ndie kiongozi "aliyesubiriwa kwa miaka mingi" na wadanganyika, "ni zawadi kutoka kwa Mungu" ili kuwafanya wadanganyika waamke kutoka usingizini.
Ametuletea "mabadiliko tuyatakayo" kama nitaazima msemo wa wapambiaji.
Link
Serikali ya Tanzania yathibitisha ununuzi wa Ndege aina ya boeing 787
Huyu ni kiongozi anayemtanguliza "Mungu" mbele kwa yale ayatendayo, ni mpole na mwenye huruma kwa walio chini yake.
Ni kiongozi mpenda DOMO-krasia na mapangaboi. Ni mpenzi wa ndege kiasi ambacho ujengaji wa viwanja vya ndege unachapiwa kazi ya mwendokasi.
Anawapenda wapinzani na amejenga jeshi la polisi imara na wanajeshi kwa ukakamavu wao na utendaji kazi wao wa utii bila kuuliza maswali wanaingizwa kwenye utumishi wa umma (kazi za kiraia, sio kijeshi) badala ya kubakizwa makambini na maporini.
Sasa tuangalie "movie" tu itakavyoishia. Huyu Kiongozi alituomba tumwombee kwa Mungu awe na angalau robo au nusu ya uvumilivu wa walalahoi anaowaongoza sijui kama tumefanya hivyo. Kama hatukufanya ni vyema tuanze sasa kwa sababu inawezekana ametishwa kwa maono ya baadhi ya wabunge.
Lakini nini kinachokushangaza juu ya utendaji kazi au (hapana kazi tu) ya mtukufu? Mwenyewe amekiri tena kadamnasi kwamba "yeye ali-beep tu urais" na Kivuitu akapokea simu.
Sasa badala ya kuiombea amani ya nchi, inapasa tuelekeze nguvu na maombi yetu kwenye kujiombea nafsi zetu kwa sababu polisi inaomba ushirikiano kutoka kwa wamiliki wa mitandao, watu wanapotea na maiti zinaokotwa huku maisha ya kitaa yakiwa ni ya ku-enjoy wote.
Je inawezekana kwamba wanaopotea na kuonekana kwenye visandarusi ni kwa sababu ni wahamiaji haramu au ni wale walioshindwa kupiga dili? Au ni watu walioshindwa kuimba mapambio?
Haya tumsifu Mungu.
Kila nafsi itaoja mauti na ipo siku ya hukumu. Tusijisahau.