Nataka Rais Magufuli ashindwe

Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
DAH, mkuu umeongea POINT sana ,tatizo watu wanaendeshwa ka mihemko badala ya kuufikirisha ubongo na tafakuri za kina,kweli kuna haja ya uwepo wa uhuru wa maoni tena mpana na usio na mwisho lakini uhuru huo usiwe wa mtu kaamka na mindoto yake anakuja humu anatoa stori za ajabu ajabu za kutunga tunga kisha aachiwe tu,

hata huko kwa wenzetu uhuru hupo ila wanautumia kwa nji ipasavyo,mfano kuna mijitu hapa Jf lazima kila siku iweke uzi ambao hauna kichwa wa miguu mradi tu naye aonekane ameweka uzi,kwa kweli ukifikiria sana unaona sisi wenyewe ndio tunajikosea heshima na kuifanya serikali itafute nji ya kuminya uo uhuru,ikumbukwe haijakatazwa kukosoa,kaa kukosoa tukosoe sana tena bila aibu wala hiyana yeyote lakini katika kosoa hiyo tuzingatia ukweli,staha na madhara ya huo ukosoaji wake,

wakati mwingine unasoma uzi unajiuliza huyu ni mtanania kweliii au ni pandikizi la mataifa jirani? ndugu zanguni machafuko ya Misri,Tunisia Libya na nchi nyingin za kiarabu kwa kaisi kikubwa yalitokana na watu kulishana matango pori juu ya serikali zao na hiyo ilikuwa ni mikakati ya nnchi za ng'ambo kuziharibu nchi za kiarabu,atokeo yake watu wakaamini propaganda na kuamua kujiweka rehani kwa kitu ambacho hakina ukweli wowote ule,leo hii hata hawajielewi .

Leo hii walibya wanalia,wamisri wanalia,watunisia wanalia ,wamepoteza ndugu na jamaa zao kwa ujinga ,kwa kudanganywa na kuchonganishwa,

Kuhusu suala la mmiliki wa Jf kukamatwa na leo inasemekana atafikiswa mahakamani,nazani watanzania hapa hatuahitaji kuwa kama WEHU,tusio jua nini maana ya mahakama,maadamu imebainika kile kilichosababisha akakamatwa na kuzuiliwa ndani ,vema tukawa watulivu huku tukiacha mahakama kazi yake ,ndio tuanze kuja na hayo malalamiko yetu mara baada ya maamuzi kutoka kwani ukitazama sheria Mmiliki wa JF na polisi wote wako sawa katika madai yao.

Mwisho watanzania nchi hii ni yetu sote,hakuna mwenye kusema hii ni nchi yangu,kama umezaliwa tanzania mkono wako wa kulia unaalama ya ndui,ni wajibu wako kuilinda tanzania dhidi ya wanapropaganda wanaoishi kwa kueneza maneno ya ajabu ajabu juu ya Tanzania,maneno ambayo hayana hata tone la ukweli.

Tukikubali hali hii mwisho wa siku tutajikuta tunalia na kujutia,mifano ya misri,libya na tunusia sio ya kubeza,tunachotakiwa kuzingatia hapa tusikubali yaliyotokea huko yanatokea hata hapa kwetu,japo kweli kuna baadhi ya maeneo ambapo serikali haijafanya vema lakini subra na utulivu ulio na uvumilivu vibaki kuwa mioyoni mwetu, wenzetu wa Ghana walivumilia mwisho akafanya maamuzi ya kistarabu na maisha yanaendelea,so na sisi hatuna budi kufanya hivyo kama tu tumewachoka watawala hawa tulio nao.
Kaka ubarikiwe...vichwa vya namna hii ndio vinapaswa kuwa hapa JF.

Unajenga hoja yako bila dhihaka na matusi.

JF inaharibiwa na watu wachache ambao tafsiri ya uhuru wa kutoa maoni/mawazo kwao ni kujenga na kutoa propaganda za uongo zenye kujenga chuki na uhasama ktk jamii na wasiguswe. Kwakuwa taifa hili linaongozwa kwa mujibu wa sheria...inatupasa kutii sheria za nchi zilizopo hata kama sheria hizo hatuzitaki.

Haiwezekani uje hapa jukwaani ubwabwaje unavyotaka bila kupima athari za kauli zako halafu wakuache tu. Hio Serikali hata sisi wananchi tutaishangaa...haipo hapa duniani.

Uhuru bila mipaka ni fujo.

JF bila nidhamu ya kuongea ni fujo...tusikubali watu wachache wakatuharibia JF yetu.....
 
jf ndiyo sehemu yalipofichuliwa maovu na baadhi ya ufisadi na vitu ambavyo havikuwa vikienda saw yani jf imemuamsha rais na watumish wengne.
 
Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupashana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.

Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.

Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Max kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.

Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hizo azma yake iwe muhali.

Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.

Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.

Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.

Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.

Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.

Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.

Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
Bhado najiuliza Huyu ni nyani ngabu.
 
Mimi natamani January makamba, nape nnauye na wote walioshadadia sheria ya mitandao wafe tuwazike tumalize shida. By the way nna maono watakufa soon

Na jela siendi na nisharopoka maono ya Lema
Naamini ungekua na real ID usingesema haya maneno na kama ungesema hata mmeo anayo kazi nyingine ya ziada..
 
Kaka ubarikiwe...vichwa vya namna hii ndio vinapaswa kuwa hapa JF.

Unajenga hoja yako bila dhihaka na matusi.

JF inaharibiwa na watu wachache ambao tafsiri ya uhuru wa kutoa maoni/mawazo kwao ni kujenga na kutoa propaganda za uongo zenye kujenga chuki na uhasama ktk jamii na wasiguswe. Kwakuwa taifa hili linaongozwa kwa mujibu wa sheria...inatupasa kutii sheria za nchi zilizopo hata kama sheria hizo hatuzitaki.

Haiwezekani uje hapa jukwaani ubwabwaje unavyotaka bila kupima athari za kauli zako halafu wakuache tu. Hio Serikali hata sisi wananchi tutaishangaa...haipo hapa duniani.

Uhuru bila mipaka ni fujo.

JF bila nidhamu ya kuongea ni fujo...tusikubali watu wachache wakatuharibia JF yetu.....
hakiak mkuu,muhimu keelekezana pale inapobidi
 
"Kwakua Aliweza Kulisukuma Gari Mpaka Upande Wa Pili Basi Akadhani Na Udereva Anauweza"..Somji Juma Malekani.....
 
Kwani mtu akiandika kitu unakipokea tu? Uwongo ni sehemu ya maisha na inasaidia wavivu wafanye utafiti kujua ukweli siyo kulishwa tu. Ya dangote yameiumbua serikali yetu. Alipokuwa anaongea dangote mwenyewe uliona viongozi wetu walivyokuwa wadogo kimwili kiakili na kiroho. Nilishindwa kuamini niliyekuwa namwona jirani na dangote ni yule prof wa nishati na madini iliyeshaongea mengi kuhusu dangote tofauti na dangote mwenyewe. Hawajali kufanya uchunguzi ni kuropoka tu kwenye vyombo vya habari. Sijui mkalimali alitafsirije kauli ya washindwe na walegee. Mungu ivushe Tanzania
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom