Nataka Rais Magufuli ashindwe

Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
1481691098875.png
 
Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupashana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.

Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.

Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Max kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.

Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hizo azma yake iwe muhali.

Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.

Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.

Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.

Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.

Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.

Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.

Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
Hawezi kushindwa km maisha yamekushinda achana nayo
 
Nataman Sana kutoa povu langu hapa ila ndy hivyo sina mil.3 wala mil.6 wala hao wadhamini wawili ila ntasema tyuu AMENI KWA MAOMBI YA MLETA UZI
 
Vijana wa Kitanzania mnaongoza kwa UNAFIKI ulimwenguni. Unatumia Fake ID humu JF wakati huo huo unahoji Uhalali na Utendaji wa Rais wa Jamhuri ya Muungano! Ama kweli wapiga Dili mmeshikwa pabaya.
Kwani wewe ndo Duterte au na wewe MNAFIKl?
 
Ashindwe na alegeee, kwanza wala sikumpigia kura mimi, na wala sikuiona sura yake kwenye ballot....
 
Kwani mtu ukitoa maoni yako pasipo kutoa matusi au ukianzisha uzi wenye uhalisia na usio wa kichochezi unakuwa na hofu ya nini?

Tatizo lililopo kuna baadhi yetu tumekuwa maarufu kutunga stori za uongo na kuzijengea hoja then tunataka jamii iamini kama ni kweli kumbe ni upotoshaji

Mtu kama umeanzisha mada yako na ushahidi unao kwa nini uogope? Endapo utahitajika polisi si unapeleka ushahidi?

Fikiria mtu anayeanzisha uzi hapa eti Dangote anahamishia kiwanda Kenya na hizo habari zinasambaa dunia nzima kumbe ni uonge pasipo kufikiria negative impacts kwa wawekezeji walioko huko nje. Mtu kama huyu leo hawezi fanywa kitu sababu tu anatumia ID feki sishangai kesho akaibuka na jambo jingine

Watu wa namna hii lazima washughulikiwe hakuna kulea ujinga. Watanzania tumekuwa maarufu sana wa kupika majungu

Ninakubaliana na wewe kabisa uhuru wa kutoa maoni lazima uheshimiwe na watawala kwani ni takwa la kikatiba lakini uhuru huo lazima uzingatie utu na nidhamu.

Leo mtu akimchukia mtu flani sababu za kiitikadi za vyama au jambo lolote, kesho anamtungia tuhuma na kusambaza kwenye mitandao. Vitu vya namna hiyo siyo vya kulea
Unaakili ya ndio mkuu ww huna fact
 
Hivi mtu akisema Dangote anahamia Kenya wakati hahamii kuna tatizo gani? Huoni watu waliosema Dangote anahamia Kenya ndio waliomuibua JPM na Dangote baada ya sisi kuchoshwa na mawaziri wetu ambao walikuwa na lugha gongana kwa suala hilo hilo moja?

Majukwaa kama haya ni majukwaa ambayo huweza kuandika lolote ikiwemo tetesi, hivyo serikali inapaswa kuiangalia JF kama mahali panapoweza kuwekwa tetesi, au maoni tu ya mtu yakajadiliwa, hivyo haipaswi kutunisha misuli dhidi ya tetesi na maoni yetu, maaana ni haki yetu kuwa na maoni hata yale yanayotofautiana na approach ya serikali katika mambo mbalimbali.

Jambo linalofanyika sasa ni la hatari na halipaswi kuungwa mkono hata kidogo. Na kwa kifupi haya huweza tu kufanywa na serikali isiyojiamini katika kile inachokisimamia. Wananchi sio wajinga kiasi cha kushindwa kuona utendaji wa serikali kwa kupofushwa na kinachoandikwa JF au mahali pengine. Kama serikali inafanya mazuri haina sababu ya kuweweseka. hata siku moja, serikali isitarajie itasifiwa tu, hilo halipo. Mtafungia JF, magazeti na redio lakini njia za mawasiliano ndio kwanza zinazidi kuibuliwa. Dunia ya sasa sio ya kukimbizana na maoni ya watu, bali ni dunia ya kutafakari na kufanyia kazi maoni hayo!
 
Naona moderator wamejitoa ufahamu.
Na hii ndio.itaikost jf, mtu anaandika upupu kama.huu achekewe kisa eti Timu kata fukua
Mimi ninakerwa sana mtu unapohusisha kila kinachoandikwa hapa na mambo ya chadema. Kwani wote walioko hapa wana vyama?
Tujifunze kukubali madhaifu yetu hakuna aliyekamilika chini ya jua na ukiona mtu analazimisha kuwa perfect ana matatizo makubwa sana.
 
Kwani mtu ukitoa maoni yako pasipo kutoa matusi au ukianzisha uzi wenye uhalisia na usio wa kichochezi unakuwa na hofu ya nini?

Tatizo lililopo kuna baadhi yetu tumekuwa maarufu kutunga stori za uongo na kuzijengea hoja then tunataka jamii iamini kama ni kweli kumbe ni upotoshaji

Mtu kama umeanzisha mada yako na ushahidi unao kwa nini uogope? Endapo utahitajika polisi si unapeleka ushahidi?

Fikiria mtu anayeanzisha uzi hapa eti Dangote anahamishia kiwanda Kenya na hizo habari zinasambaa dunia nzima kumbe ni uonge pasipo kufikiria negative impacts kwa wawekezeji walioko huko nje. Mtu kama huyu leo hawezi fanywa kitu sababu tu anatumia ID feki sishangai kesho akaibuka na jambo jingine

Watu wa namna hii lazima washughulikiwe hakuna kulea ujinga. Watanzania tumekuwa maarufu sana wa kupika majungu

Ninakubaliana na wewe kabisa uhuru wa kutoa maoni lazima uheshimiwe na watawala kwani ni takwa la kikatiba lakini uhuru huo lazima uzingatie utu na nidhamu.

Leo mtu akimchukia mtu flani sababu za kiitikadi za vyama au jambo lolote, kesho anamtungia tuhuma na kusambaza kwenye mitandao. Vitu vya namna hiyo siyo vya kulea
DAH, mkuu umeongea POINT sana ,tatizo watu wanaendeshwa ka mihemko badala ya kuufikirisha ubongo na tafakuri za kina,kweli kuna haja ya uwepo wa uhuru wa maoni tena mpana na usio na mwisho lakini uhuru huo usiwe wa mtu kaamka na mindoto yake anakuja humu anatoa stori za ajabu ajabu za kutunga tunga kisha aachiwe tu,

hata huko kwa wenzetu uhuru hupo ila wanautumia kwa nji ipasavyo,mfano kuna mijitu hapa Jf lazima kila siku iweke uzi ambao hauna kichwa wa miguu mradi tu naye aonekane ameweka uzi,kwa kweli ukifikiria sana unaona sisi wenyewe ndio tunajikosea heshima na kuifanya serikali itafute nji ya kuminya uo uhuru,ikumbukwe haijakatazwa kukosoa,kaa kukosoa tukosoe sana tena bila aibu wala hiyana yeyote lakini katika kosoa hiyo tuzingatia ukweli,staha na madhara ya huo ukosoaji wake,

wakati mwingine unasoma uzi unajiuliza huyu ni mtanania kweliii au ni pandikizi la mataifa jirani? ndugu zanguni machafuko ya Misri,Tunisia Libya na nchi nyingin za kiarabu kwa kaisi kikubwa yalitokana na watu kulishana matango pori juu ya serikali zao na hiyo ilikuwa ni mikakati ya nnchi za ng'ambo kuziharibu nchi za kiarabu,atokeo yake watu wakaamini propaganda na kuamua kujiweka rehani kwa kitu ambacho hakina ukweli wowote ule,leo hii hata hawajielewi .

Leo hii walibya wanalia,wamisri wanalia,watunisia wanalia ,wamepoteza ndugu na jamaa zao kwa ujinga ,kwa kudanganywa na kuchonganishwa,

Kuhusu suala la mmiliki wa Jf kukamatwa na leo inasemekana atafikiswa mahakamani,nazani watanzania hapa hatuahitaji kuwa kama WEHU,tusio jua nini maana ya mahakama,maadamu imebainika kile kilichosababisha akakamatwa na kuzuiliwa ndani ,vema tukawa watulivu huku tukiacha mahakama kazi yake ,ndio tuanze kuja na hayo malalamiko yetu mara baada ya maamuzi kutoka kwani ukitazama sheria Mmiliki wa JF na polisi wote wako sawa katika madai yao.

Mwisho watanzania nchi hii ni yetu sote,hakuna mwenye kusema hii ni nchi yangu,kama umezaliwa tanzania mkono wako wa kulia unaalama ya ndui,ni wajibu wako kuilinda tanzania dhidi ya wanapropaganda wanaoishi kwa kueneza maneno ya ajabu ajabu juu ya Tanzania,maneno ambayo hayana hata tone la ukweli.

Tukikubali hali hii mwisho wa siku tutajikuta tunalia na kujutia,mifano ya misri,libya na tunusia sio ya kubeza,tunachotakiwa kuzingatia hapa tusikubali yaliyotokea huko yanatokea hata hapa kwetu,japo kweli kuna baadhi ya maeneo ambapo serikali haijafanya vema lakini subra na utulivu ulio na uvumilivu vibaki kuwa mioyoni mwetu, wenzetu wa Ghana walivumilia mwisho akafanya maamuzi ya kistarabu na maisha yanaendelea,so na sisi hatuna budi kufanya hivyo kama tu tumewachoka watawala hawa tulio nao.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom