Nataka Rais Magufuli ashindwe

Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
Biblia na yesu alisema mchungaji mwema uwatangulia kondoo kwa mbele sasa makanisa na wanaojidai mitume na manabii mbona wameufyata wameacha kondoo kwa mbele ya mbwamwitu alafu utasikia watu wakiwa waita watumishi wa mungu kumbe makanjanja wapiga dili kondoo si kitu kwao wakristo acheni kudanganya makanisani nyinyi!!!!!
 
Kuamini kuna maisha baada ya kifo ni umasikini wa fikira...the strongest will survive, that's why we have to fight for our rights mambo ya utalipiwa na mungu ni kukubali kuonewa ambalo ni kosa kikatiba.

In this occurrence we have different perception according to the thread..mfano kuna yule mama alie sema Binti wa mkulu alijiua, wakati tuliofahamu ugonjwa mpaka mauti tulibaki tumepigwa butwaa mzee wake wakati ule alihangaika sana kujaribu kunusuru maisha yake mmpaka kwa TB Joshua walifika then kuna mama zima linaleta uongo bado Max analilinda.
huyo mmama alieleta uongo kwa nini yeye asikamatwe na anajulikana kabisa na kila mtu? max amemlinda wapi wakati muhusika anajulikana mkuu?
 
Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupashana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.

Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.

Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Max kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.

Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hizo azma yake iwe muhali.

Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.

Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.

Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.

Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.

Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.

Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.

Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
Kaka dua la kuku halimpati mwewe.Raisi ni Taasisi inayoheshimika duniani kote wewe ni nani hata ukaandika andiko la kumkashfu Raisi wetu mpendwa.Sheria ni msumeno .Mex kama hana hatia ataachiwa na kama ana hatia sheria itachukua mkondo wake.Unachokitafuta utakipata muda si mrefu walikiwepo wajuaje wengi sana kabla yako.Be carefull
 
Kosa sio LA maxence.bali kosa ni lako kupeleka umbea kwa mabosi.naona unatishia watu maisha.
 
Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupashana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.

Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.

Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Max kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.

Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hizo azma yake iwe muhali.

Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.

Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.

Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.

Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.

Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.

Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.

Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
USHÌNDWE WEWE MILELE . .
MTU MZIMA OVYO KABISA
 
Tunaogopa, wewe upo Tennessee USA, sisi tupo Tandale Kwa mtogole ,wakati tuking'olewa meno wewe utakuwa unakula burger za McDonald's.
Wajukuu zako watakuja kukulaumu sana.kama babu zetu wangekuwa waoga kama wewe.mpaka leo hata uhuru huu wa bendera tusingeupata.
 
anapiga hatua moja mbele sita nyumba labda kukamata watu na kuminya Uhuru wa habari ndo viwanda vyenyewe hivyo.....hivi Ghana au Gambia waliwezaje kukubali kupokezana madaraka?
 
Nyani Ngabu Mzee Mwanakijiji na wenzao kibao walijitoa ufahamu na kuwa wapiga filimbi wa Hemelini toka jina la Bwana huyu lilipopitishwa pale Dodoma kwa mizengwe inayovunja haki zote za kidemokrasia ambayo wao walikuwa wakiipigania. Wakaandaa na makala nyingi za kumsifia na kuuaminisha umma wa Watanzania kwamba sasa nchi imepata mkombozi. Ni vyema wakanyamaza na kuendelea kumpigia debe huyo mwokozi bila kujali kamgusa nani. Maana akiguswa Sumaye ..hoyeeee! Akiguswa Mbowe...Hoyeee....sasa wamegusa hata kategemeo ketu kalikobaki ndo wanaomba alaaniwe? No. Tumvumilie kidogo " Anyooshe" Tanzania...
Umenielewa sana.Huo ndio ukweli.Wanafiki wakubwa.
 
Mkuu, umeanza kuhamasisha au?

Unataka ashindwe wapi khasa, kuwa "specific".

Kila atakachokifanya kishindwe...yaani ashindwe kila kitu mpaka familia imshinde (ingaweje nasikia ilishamshinda siku nyingi)
 
Ashindwe kwenye kuwaziba watu midomo au ashindwe kwenye kila jambo?
 
JF ni Jukwaa linalofuatiliwa sana na viongozi.
Inasemekana baada ya viongozi kutoa matamko yao, huja huku haraka kuangalia maoni ya vijana.
Wanakuja huku kwa kuwa waliopo huku wanajielewa.

Vita dhidi ya JF ni vita dhidi ya wanao jielewaa.

Ila wakumbuke kuwa JF haijawahi kushindwa na haitoshindwaa!!
[HASHTAG]#GREATJF[/HASHTAG]
ni kweli mkuu... hapa kuna fikra pevu sana na zimewasaidia watawala wengi kujirekebisha. Lakin swala linakuja kwamba, kama kweli tunatoa mawazo ya maana kwa nini tunaogopa kungundulika na vyombo vya usalama? kwa nini kuwaficha vyombo vya usalama kama wakihitaji kujua nani kasema nini? Uoga huu unatoka wapi??

Tazama michango yangu yote katika jukwaa hili, sijawahi kumtukana mtu, hata nikitoa mawazo ya kuikosoa serikali naongea kwa staha, sina hofu yeyote ya kujulikana na vyombo vya usalama.

kabla ya kushambulia vyombo vya usalama tujipime wenyewe.. je tunaongea kwa staha au tunataka jamii forums liwe jukwaa la kujifichia matusi yetu kwa watu??

Max Mello nakuombea umalizane nao hao watu urudi kuendelea na shughuli zako, Mungu ni mwema, utatoka tu bro.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom