Nataka Rais Magufuli ashindwe

Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
Watu wenye hekima huwa wanawaonya kina Maxence kuhusu kucheka na watu wanaongea pumba na matusi kupitia nyuma ya keyboard lakini hawakusikia, ndiyo malipo ya kulea ujinga wanaanza kuyapata. Watu wanashangaa nini hata Marekani huko mnakotaka kukimbilia ukimbizi mitandao mikubwa kama yahoo inapelekeshwa na serikali itakua hapa? Watu tujifunze kuwa uhuru una mipaka yake, maana kama una uhuru wa kufanya lolote basi ua mtu uone kama huo uhuru wako utafuatwa, sentensi ya Uhuru inasema "una uhuru wa kufanya lolote ili mradi usivunje sheria" kwanini waliongeza hilo neno kuvunja sheria??? lakini MSIMISEKE SENIOR hapa kuna wengi wanajifanya wanajua huko hawajaverify hizo personel details zao. Mbaya zaidi wanaishi bongo na wanatumia mtandao wa bongo. Kwanini wasiende kutapika hizo nyonga zao katika mitandao ya kimataifa maana huko ndiko wataianika serikali labda na wao kiingereza kinawashinda.

Umeongea vyema.

Watu wanasahau hata huko wanakodhani kuna uhuru wa kuyoa maoni wafanye rejeo la mmiliki wa Mtandao wa Wikleaks ni kitu gani kilimpata baada ya kutoa taarifa za kiuchunguzi na kijasusi za baadhi ya mataifa makubwa. Hadi leo yupo mafichoni
 
Unaongea mambo ya ajabu.
wale mawaziri waliokuwa wkiongelea sakata la Dangote na makaa ya mawe, gesi na dizeli ulisikia wakisema nini?
By the way, kupata kesi hapa si lazima uongee matusi. Ukiikosoa serikali kwa namna yoyote ya wazi jamaa analala na wewe mbele.

Ukitaka kusalimika, isifie serikali, kisha mimina mitusi mikubwa, mizito na minene kuelekea upande wa "wale wenzetu" halafu uone kama utaguswa. Sheria ina macho bwana, inaangalia rangi na sura.

Waliongea hadharani tukawatambua. Na wewe kama unajiamini na habari zako kwa nini ufiche ID yako?
 
Worst president ever happened in Tanzania hafai! hafai! hafai hata kidogo JK kutupa huyu mtu ametuingiza chaka moja baya sana!
 
ndugu usujidanganye kuwa ukitoa taarifa za ukweli ndo utakuwa salama!. determinant ya usalama wako ni yule anaye athirika na taarifa yako, kama ana nguvu za kukuadhibu atakuadhibu pamoja na ukweli wako wa wazi! kumbuka kupekuliwa kwa kubenea na kumwagiwa tindikali zikitafutwa zinazo daiwa kuwa nyaraka za serikali zinazo husu kagoda, richmond na EPA. Kwa kifupi wistle blowers hawako salama kama taarifa zao zina waumiza wenye mamlaka!.

Tatizo ni kushindwa ni kushindwa kujiamini
 
Umeongea vyema.

Watu wanasahau hata huko wanakodhani kuna uhuru wa kuyoa maoni wafanye rejeo la mmiliki wa Mtandao wa Wikleaks ni kitu gani kilimpata baada ya kutoa taarifa za kiuchunguzi na kijasusi za baadhi ya mataifa makubwa. Hadi leo yupo mafichoni
Julian Asange hakufanya kosa lolote lakini sasa mwaka wa 3 jua analiona kupitia dirishani pamoja na vyombo vyote vya habari ku report huku ni kujipa moyo tu kuna waandishi wa Aljazeera wapo misri wameswekwa ndani lakini misri inapata misaada kibao kutoka marekani. Mimi ngoja ninyamaze maana nimeona wameanza kuzifuta comments zangu japo situmii lugha chafu na wanawaacha wanaotukana
 
Kwani mtu akianzisha habari hapa kwamba Dangote anahamishia kiwanda Kenya na wewe ukaamini, unafikiri ni nani anapaswa kuswekwa rumande? Kwa maoni yangu, ni wewe unayeamini vitu hovyo hovyo bila kuhoji. Jinga kabisa. Tena hustahili kuchangamana na jamii. Unapaswa kufungwa. Yaani mtu anakuambia lile likiwanda linahamishiwa Kenya na wewe unakubali tu kama zuzu. Na kwa taarifa yako, investors ni watu makini and very informed. Usifikiri wanayumbishwa kwa taarifa fake unazoweka hapa JF. Umeniuzi sana kwa sababu ni watu wenye mawazo kama yako mnaojenga hoja za kijinga mpaka Max yuko ndani sasa na hatima yake haifahamiki. Eti impacts kwa wawekezaji huko nje! Ndio ulichomwambia JPM na kufanya Max akamatwe? Mijitu mingine sijui kwanini imetokea kuwa sehemu ya jamii yetu. Nalaumu sana elimu yetu. Ndio imetupatia watu wa namna hii. We need to do something guys.
Mbona povu linakutoka. Uhuru wa kutoa maoni lazima uheshimiwe na watawala lakini uhuru usiokuwa na mipaka ni utumwa na uwendawazimu. Endelea kubwabwaja sana lakini ukweli ndo huo. Suala la Max kushikiliwa hakuna anaye liunga mkono

Elewa hoja yangu vizuri. Siungi mkono hata kidogo kushikiliwa kwa Max mimi hoja yangu ni sisi members kujifanya wajuaji sana, badala ya kujenga hoja kwa facts tunakaa kubuni na kueneza habari za uongo na chuki huku tukijificha nyuma ya pazia la ID feki
 
Kwani manunuzi ya chadema kwenda kwa Lowasa yaliidhinishwa na nani??


Kwa jinsi bavicha mlivyo wachawi mnapinga hadi maendeleo ya watanzania!!!

Shame on you wakala wa mafisadi
 
Tatizo ni kushindwa ni kushindwa kujiamini
kama umewaanika jinsi walivyo fanya wizi wao unadhani watakusalimisha?, tena naona awamu hii inweza kuwa corupt kuliko zilizo tangulia kwasababu inataka kufanya mambo yake gizani!!!, walianza na bunge kufichwa,...................
 
Mimi maoni yangu ni kwamba ameshindwa moja kuporomoka kwa soko la hisa kufirisika kwa mabenki kuuma kwa biashara kushukuru kiwango cha uwezo wa bandari kunyanyasa wawekezaji kunywa wanafunzi elimu ya juu vyuo kuongeza kushukuru thamani ya fedha ya Tanzania kukosa kana dawa zikiwamo chanjo kukandamiza democrasia maisha na uchumi wa mwananchi mmoja mmoja kuporomoka Magufuli ameshindwa na hii ni laana inamwandama
 
Mimi natamani January makamba, nape nnauye na wote walioshadadia sheria ya mitandao wafe tuwazike tumalize shida. By the way nna maono watakufa soon

Na jela siendi na nisharopoka maono ya Lema

Clueless
Maybe yu think yu are in a dark area, but yu are seen so clearly. Sipendi asiyejipenda. Usimfuate Nyani Ngabu ndugu, hawa wana pa kujificha, tena wengine ni maccm wametumwa humu jf kulianzisha halafu kina bendera hufuata upepo wajitumbukize kumbe ndo kuishia hivyo.
Poleni, hamnipati ng'oo familia yangu bado changa nina kitoto tumebarikiwa juzi tu hata mama yao hajamaliza siku za kunywa mtori.
 
Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupashana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.

Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.

Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Max kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.

Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hizo azma yake iwe muhali.

Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.

Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.

Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.

Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.

Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.

Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.

Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
Likiwaka jua lawama ,ikinyesha mvua lawama,akiwa mpole lawama ,akiwa mkali napo lawama,mwisho wa yote ni kuwa kila mtu ana mtazamo tofauti,na pia tukumbuke wanaosoma habari kwenye mitandao ni kikundi kidogo tu na wengi wao sio wapiga kura na hawapo nchini kushiriki ujenzi wa Taifa ama kweli fimbo ya mbali haiui nyoka.
 
Mimi natamani January makamba, nape nnauye na wote walioshadadia sheria ya mitandao wafe tuwazike tumalize shida. By the way nna maono watakufa soon

Na jela siendi na nisharopoka maono ya Lema
ha ha ha ha ha
 
Kadri unavoogopa kufa ndivo unavokufa haraka,maana ukiogopa hutoendesha chombo cha moto,wala hutokwenda shamba isijeigwa na nyoka,hutolala ukiogopa usingizi.utakufa haraka na njaa.nadhani tunatoka mchana tunaenda usiku,andaeni vijinga maana tutakanyagana na hili haijalishi umeva gwanda wala ganda,utakanyagwa tu!
 
Mimi maoni yangu ni kwamba ameshindwa moja kuporomoka kwa soko la hisa kufirisika kwa mabenki kuuma kwa biashara kushukuru kiwango cha uwezo wa bandari kunyanyasa wawekezaji kunywa wanafunzi elimu ya juu vyuo kuongeza kushukuru thamani ya fedha ya Tanzania kukosa kana dawa zikiwamo chanjo kukandamiza democrasia maisha na uchumi wa mwananchi mmoja mmoja kuporomoka Magufuli ameshindwa na hii ni laana inamwandama
Unakimbilia wapi andika polepole kwa umakini
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom