Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
Huyu rais nilidhani angekuwa wa maana kumbe bora mpenda safari Kikwete. Huu udikteta angeupeleka kwenye mambo ya msingi angefanya la maana sana. Seems hana shughuli anazi create kama Mjinga mjinga yule taahira Paul Makonda
Umeona eeh hafai.
 
Poti,

Umeandika hii kitu umekasirika. Calm down bro. Magufuli akishindwa in Tanzania imeshindwa. Si yeye. Tutakaoumia ni sisi. We should always know Tanzania is bigger kuliko hasira zetu. Uhuru una gharama na bahati mbaya Max ndo amekuwa kafara. Na wengine watafuata.

Possibly members humu na kwingineko tuanzishe fund ya kuwatetea akina Max. In fact it is good ameenda mahakamani tutajua mbichi na mbivu.

Kwani nimesema ashindwe kwenye kila kitu?

Hebu rudia tena kusoma labda utaelewa ninachotaka ashindwe.
 
Ubaya wa ukada ni unaona udikteta asubuhi ila jioni unaona huohuo udikiteka kuwa umahiri.
Ubaya wake ni pale ndugu yako au maslahi yako yakiguswa na kwa unafiki wa umri unampinga.
Ila akikamatwa fulani,kupigwa n.k ambaye hali chakula nawe,basi mdomo hutoa sifa tu kwa dikteta.
Kaleteni Ben Saanane
 
Kwani mtu ukitoa maoni yako pasipo kutoa matusi au ukianzisha uzi wenye uhalisia na usio wa kichochezi unakuwa na hofu ya nini?

Tatizo lililopo kuna baadhi yetu tumekuwa maarufu kutunga stori za uongo na kuzijengea hoja then tunataka jamii iamini kama ni kweli kumbe ni upotoshaji

Mtu kama umeanzisha mada yako na ushahidi unao kwa nini uogope? Endapo utahitajika polisi si unapeleka ushahidi?

Fikiria mtu anayeanzisha uzi hapa eti Dangote anahamishia kiwanda Kenya na hizo habari zinasambaa dunia nzima kumbe ni uonge pasipo kufikiria negative impacts kwa wawekezeji walioko huko nje. Mtu kama huyu leo hawezi fanywa kitu sababu tu anatumia ID feki sishangai kesho akaibuka na jambo jingine

Watu wa namna hii lazima washughulikiwe hakuna kulea ujinga. Watanzania tumekuwa maarufu sana wa kupika majungu

Ninakubaliana na wewe kabisa uhuru wa kutoa maoni lazima uheshimiwe na watawala kwani ni takwa la kikatiba lakini uhuru huo lazima uzingatie utu na nidhamu.

Leo mtu akimchukia mtu flani sababu za kiitikadi za vyama au jambo lolote, kesho anamtungia tuhuma na kusambaza kwenye mitandao. Vitu vya namna hiyo siyo vya kulea
Hakuna stori za uongo.
 
Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupashana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.

Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.

Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Max kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.

Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hizo azma yake iwe muhali.

Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.

Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.

Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.

Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.

Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.

Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.

Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
Be care my son
 
Mkuu,huyu kiongozi sio mbaya ila kuna vitu vichache anakosea kama binaadam kwa kuruhusu mihemko yake binafsi iliyopitiliza kwenye mambo ya msingi,anatakiwa ajicontrol sana kwani mara nyingi jambo hili humuaribia,abadilishe mindset yake juu ya wanaomkosoa,naamini kwa uchapakazi wake akisikiliza hoja zao na kupata ushauri wa watu wake wa karibu anaowaamini zaidi,anaweza kutoboa sana,kwani sio wote wanaokukosoa hawana hoja,akilitambua hilo atafanya mambo makubwa sana

Akizipanga vizuri karata zake,anaweza kuwa the best president ever happened in our country
 
Hivi mna u hakika kuwa Rais ndiye kaagiza, kiongozi wetu hapa JF akamatwe?
====
Staha katika kumshauri rais ni muhimu.
Staha ninini?
Niwekee Tafsida katika haya maneno ili nizingatie staha ya ushauri kwa Rais.

(KIVUKO CHA MV DAR KILICHOSIMAMIWA KIMUCHAKATO NA WAZIRI WA UJENZI DK.MAGUFURI NA AKAKIKAGUA KWENDA BAGAMOYO NA KUTANGAZA NI KIZURI SANA CHA KISASA NI KIBOVU)

(ZITO KABWE ASEMA NDEGE ZA MAGUFURI NI MTUMBA ZILIPAKWA RANGI)

(UUZWAJI NYUMBA ZA NHC ULIOSIMAMIWA CHINI YA WAZIRI MAGUFURI ULIJAA UTATA)

Nipe mfano staha ipi hapa nitumie?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom