Natabiri jaribio lolote la kubadilisha Katiba na ukomo wa Rais litaibua mazito

Natabiri yakuwa jaribio lolote la kubadili katiba nakurefusha ukomo wa Rais litazuwa Moto wa kisiasa ambao haukuwahi kutokea tangu kuwepo kwa Taifa hili.

Yani hamtoamini wala kudhania. Itakuwa ni siku mbaya na nzito kwa Taifa ndipo sote tutaamini kweli kuna deep state in side state.

Nasali Jambo hili lisitokee wala kusemwa tu. Madhara yake yatatutesa sana kama Taifa.

Mungu ibariki Tanzania.
Kwa aina ya wa Tanzania hata wakiongeza kutawala kwa huyu Mwami Magufuli iwe maisha hakuna wakupinga labda wapingaji wapinge kwenye vijiwe vya kahawa
 
Ficha ujinga wako basi
Huyo jamaa yako kwa miaka mitano hiyo miradi yake haitaisha kamwe.
Pia kwa ubabe na ukatili wake aliofanya kwa baadhi ya watu lazima awe na mashaka akiingia MTU mwingine atalipa visasi .
So ni lazima ajiongezee muda mpaka afie madarakani
 
Suggest mkakati wa kumzuia ili watu wa stop speculation.
Maana uchaguzi wa 2020 uliporwa kwa nguvu ya jeshi... je, mkakati wa kupambana na jeshi ni upi if I may ask?
Haya mambo complex, hayana majibu mepesi na mimi sijifqnyi kuwa na utaalamu wa kujua majibu yote.

Ingekuwa ni rahisi hivyo, wengine wangekwishatekeleza utatuzi kwa ufanisi.

Hilo jeshi unalolisema lenyewe limegawanyika. Kuna watu wengi sana jeshini hawaoendi ujinga unaoendelea. Na wengine waliandika moaka "waraka wa jeshi" miaka michache nyuma kupinga uozo wa muelekeo wa nchi.

Kitu cha kwanza kabisa ni kupinga matokeo ya 2020 na ku expose fraud. Kuanalyze makosa ya 2020 na kutafuta utatuzi.

Bila hilo, hata Magufuli asipoendelea 2025, ataweka pandikizi lake litakaloendeleza sera zake.

Hapo ndipo utakapoona ku fight Magufuli asiongeze muda 2025 tu ni smallmindedness. Kwa sababu badala ya ku fight mfumo, mtakuwa mnaishia ku fight mtu.

Na hata Magufuli akiondika, kama mfumo unaruhusu mwingine aendeleze alipoachia Magufuli, mnaweza kusema afadhali ya Magufuli kuliko huyu aliyemfuatia.

Tulikuwa tunamsema vibaya Kikwete hapa, nikawaambia rafiki zangu kwamba siwezi kushangaa rais qtakayemfuatia Kikwete akawa wa ovyo kuliki Kikwete kwenye utawala bora.

Nimetaja baadhi ya mambo hapo juu.

Mkakati unaweza kuhusisha kufungua kesi za uchaguzi kupinga matokeo na kuanika uozo. Yani hata mahakama zikiendeshwa kwa amri kutoka juu, media coverage tu ya uozo itasaidia ku expose mambo.

It is one thing nchi kujua CCM wameiba kura, it is quite another upinzani ku expose hili systematically katika court system, with full evulidence. Halafu kufanya a countrywide and unternational PR campaign kuanika uozo wa CCM walivyoiba kura.

Na kama mahakama za ndani hazitoi haki, mkakati uhusishe kuimulika nchi kimataifa zaidi mpaka watawala watie adabu.

Sasa hivi Tanzania imejitoa Mahakama ya Afrika, kwa kiasi kikubwa ili kuepusha upinzani kupeleka kesi za ku challenge matokeo ya urais (ambazo mahakama za Tanzania haina jurisdictiin nazo). Lakini sinasikia hata mpinzani mmoja akiliongelea hili. Watu wanaongelea Magufuli atajiongezea muda 2025!

Kuna mambo yanayoendana na kuingiliana kama kutafuta katiba mpya, kupunguza madaraka ya rais, kutafuta tume huru ya uchaguzi, kuimar8shq nankushirikishq civil society zaidi, kuwa na utamadunibwa uwazi na zaidi, kuweka utamaduni wa consumer protection.

List ni ndefu sana. Na mimi sina majibu yote.

Hii si kazi ya upinzani tu.

Kuna hata wazee wa CCM kina Warioba, Msekwa, Butiku wanaojiheshimu nanm kuheshimiwa wanaweza kutumika kurudisha mambo fulani yanayoenda arijojo kwenye mstari.

Ila, ninachoona ni utamaduni wa "electocracy". Badala ya democrqcy, tuna electocracy.

Kuanzia CCM mpaka upinzani, watu wako focused kwenye elections tu.

CHADEMA ndiyo kabisa wanajichanganya.Huku wanasemq uchaguzi haukuwa wa huru wala haki, huku wengine wanataka ubunge uliotokana na uchaguzi huo huo.

Ndiyo maana uchaguzi wa 2020 umeisha tu, watu wanaanza kuongelea 2025.

Bila hata kuchambua uchaguzi wa 2020 ulikuwaje, makosa yalikuwa wapi, tuyasahihishe vipi ili tusirudie tena makosa hayo 2025.
 
Hilo jambo lipo na liko njiani,madaraka ni matamu sana,alikuwa anajisemesha mbele ya umma kwenye kampeiinii ili aonekane mtu mwema anyefuata katiba kumbe ni sifuri,Wakirsto mna shida sana kwenye madaraka ,na huu wimbo umeimbwa na wakiristo sijui watawala wenu wasali wapi AMBWENE KAIMBA WIMBO WA CHOZI LA HAKI
 
Unaelewa hata tofauti ya kujua na kuamini?

Mkuu una akili sana, unasoma sana..
Hakuna asiyejua hilo humu lakini kutumia same trick kila mara all over these years is getting monotony and boring.
Nikutakie usiku mwema japo sijui huko ulipo ni muda gani
 
Magufuli alisema anataka kumaliza upinzani 2020.

Akasema hataki mtu anayemlipa mshahara (wakuu wa mikoa, wilaya etc) jimboni kwake apite mpinzani.

Ndiyo kiini cha wizi mkubwa uliofanyika mpaka bunge limekosa wapinzani.

Haya mambo aliyasema wazi Magufuli na mtu yeyote ambaye angesema kuhusu wizi wa kura 2020 angeweza kusema hivyo kwa fact, kwa kauli za Magufuli.

Twende kwa fact. Haya mambo ya speculation kila mtu anasema yake.

Sasa una kauli gani ya Magufuli aliposema kwamba atazidisha muda wake wa urais?

Nasema hivi, kauli ya kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki ni ya wazi sana, na ni ya karibuni kuliko hizo nyingine zote. Kwenye kuongeza muda siangalii zaidi kauli maana sio mkweli, hapo naangalia zaidi matendo yake. Narudia tena hataongeza muda, lakini nitashangaa sana iwapo hataongeza muda. Kirahisi hivyo yaani.
 
Unaji contradict.

Unasema hataongeza muda, halafu utashangaa iwapo hataongeza muda.

Ni kama unasema unajua jua litachomoza kesho asubuhi.

Halafu unasema jua likichomoza kesho asubuhi utashangaa.

Sasa jambo unalojua litatokea litakushangaza vipi?
 
Mkuu una akili sana, unasoma sana..
Hakuna asiyejua hilo humu lakini kutumia same trick kila mara all over these years is getting monotony and boring.
Nikutakie usiku mwema japo sijui huko ulipo ni muda gani
Yani kama hujui 1+1 =2 katika base ten math niache kukuhoji kuhusu hilo kwa kuogopa kurudia somo moja hilo hilo?

Sasa kama hujui 1+ 1= 2 tutafikaje kwenye Riemann Zeta Functions?

Kati ya mimi niliyeuliza swali na wewe unayekimbilia bila kulijibu nani analeta tricks hapa?
 
Natabiri yakuwa jaribio lolote la kubadili katiba nakurefusha ukomo wa Rais litazuwa Moto wa kisiasa ambao haukuwahi kutokea tangu kuwepo kwa Taifa hili.

Yani hamtoamini wala kudhania. Itakuwa ni siku mbaya na nzito kwa Taifa ndipo sote tutaamini kweli kuna deep state in side state.

Nasali Jambo hili lisitokee wala kusemwa tu. Madhara yake yatatutesa sana kama Taifa.

Mungu ibariki Tanzania.
Kwenda zako kazi yenu kuleta uzushi na kujaribu kufanya iwe issue ya kusadikika. Wewe nani kakwambia kuna mpango wa magufuli kuongeza muda. Mwenyewe kashaeleza mara tele hatavunja katiba kuhusu mihula. Zote hizo ni mbinu za kujaribu kuleta sintofahamu zinazosimamiwa mabeberu na kupenyezwa kupitia vibaraka wao.
Mabeberu na vibaraka wao wasubiri tu maana wataona kitakachotokea 2025 maana ccm haina uhuba wa kina magufuli. Tuombe mungu tu atupe uhai.
 
Ushakuwa muimba Taarabu, mtoto sio ridhiki weyeeee
Huna hoja, unaleta viroja.

You are not worth my shells.

I am placing you in my ignore list.

Kuanzia sasa sitaona unachoandika.

Sina muda wa kubishana na ngumbaru asiye staha.
 
Natabiri yakuwa jaribio lolote la kubadili katiba nakurefusha ukomo wa Rais litazuwa Moto wa kisiasa ambao haukuwahi kutokea tangu kuwepo kwa Taifa hili.

Yani hamtoamini wala kudhania. Itakuwa ni siku mbaya na nzito kwa Taifa ndipo sote tutaamini kweli kuna deep state in side state.

Nasali Jambo hili lisitokee wala kusemwa tu. Madhara yake yatatutesa sana kama Taifa.

Mungu ibariki Tanzania.
Moto wa kisiasa utatoka wapi wakati mmesusa kuwa kwenye bunge? Unategemea utoke kwa hao mamluki walioko nje ya nchi yetu?

Unajidanganya tu. Katiba lazima ifanyiwe mabadiliko kidogo ili kutoruhusu mercenaries kugombea urais wa JMT na kuruhusu jumuiya za wanawake za vyama vya siasa kuwakilisha majina ya wapendekezwa wa wabunge wa viti maalum directly kwenye NEC bila kupitia kamati kuu za vyama etc
 
Yani kama hujui 1+1 =2 katika base ten math niache kukuhoji kuhusu hilo kwa kuogopa kurudia somo moja hilo hilo?

Sasa kama hujui 1+ 1= 2 tutafikaje kwenye Riemann Zeta Functions?

Kati ya mimi niliyeuliza swali na wewe unayekimbilia bila kulijibu nani analeta tricks hapa?

Brother wewe una akili, You are well learned, unasoma sana na una uwezo mkubwa wa kuelezea complex stuffs na kila mtu analijua hilo. Hutakiwi prove anything to anybody kwa sababu ni kitu obvious, Wengi tunakubali jinsi ulivyo deep kwenye vitu mbali mbali for years

Kingine Sijakukimbia ila sijaona umuhimu wa kuendelea kubishana kwa vitu vilivyo wazi hususani na mtu naemuheshimu kama wewe...

simply sina spirit ya kushindana kwenye discussions maana huwa nafanya ili kuongeza ufahamu ila si kuprove kuwa niko njema kuliko wengine unless mtu anishambulie and yet huwa napuuza mara nyingi.

Have a nice time brother
 
Sifa zako zote nazikataa na nakurudishia mwenyewe.

Mimi zitanifunga tu.

Unajuaje hapa ni kushindana na hapa ni kueleweshana?

Na inakuwaje hutaki kujibizana lakini bado unanijibu?

Na kwa nini unanijibu bila kujibu swali langu, imani ni nini na kujua ni nini?
 
Natabiri yakuwa jaribio lolote la kubadili katiba nakurefusha ukomo wa Rais litazuwa Moto wa kisiasa ambao haukuwahi kutokea tangu kuwepo kwa Taifa hili.

Yani hamtoamini wala kudhania. Itakuwa ni siku mbaya na nzito kwa Taifa ndipo sote tutaamini kweli kuna deep state in side state.

Nasali Jambo hili lisitokee wala kusemwa tu. Madhara yake yatatutesa sana kama Taifa.

Mungu ibariki Tanzania.
Mkuu wananchi hawa unaohofia hali zao hawajali madhila yakiwafika bali wanajali kuganga njaa zao!!
 
Back
Top Bottom