Wauzaji official na unofficial.
Hapana mke wangu mie haniuzii, sawa nampa huduma zote hizo je namgonga kila siku? Kila siku anakula hela yangu, matumizi mengineyo, na mpaka likitokea jambo kwao mie nasimama kidete, je kila nikimhudumia namkula!?
Mke nilipewa bure!!??:
Jibu ni HAPANA,nilitoa mahari, je mahari ni kumnunua!?
Jibu pia HAPANA.
Mahari ni nini, according na mafundisho ya dini na imani yangu mimi, nilivyoelewa,
Mahari ni zawadi itokayo kwa mume kwenda kwa mke, baada ya kunikubali.
Mfano.
Nakuja kukuposa, we unanikubalia,huenda umekataa mengi, lakini pia kuja kukubali kuishi kwangu ni jambo kubwa kuna mengi, na ndio maana katika kuzunguka kwangu we ndio nikakuuona unanifaa. pale nakuuliza unataka zawadi gani, unanitajia ng'ombe, hela,hereni kiwanja, ama kitabu cha dini ama chochote kile...
Sasa hiyo zawadi 🎁 ndio mahari yenyewe, na ikiwa kweli una mapenzi nami wala mara nyingi mtu hataji zawadi ya kukomoana..
Ila mahari imetafsirika vibaya, imepokewa vibaya, imebadilishwa, mara wanataja wazee, mara mabinti ndio wanaona pakuvunia etc