Nashukuru Mungu mwaka 2023 nimetimiza ndoto yangu ya kuishi Masaki japo ni chumba kimoja

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
16,053
35,951
Nilizaliwa nikajikuta niko mitaa ya Chole Oysterbay,

Mwaka 1988 kufumba na kufumbua roli aina ya Bedford limekuja nyumbani kutuhamisha kuelekea Tabata, huwezi amini mizigo haikufika hata nusu ya roli lile, enzi hizo watumishi ukihamia nyumba ya Serikali unakuta vitanda, magodoro, sofa, dinning table and chairs. Etc.

Kuja kugundua kumbe mzee amehamishwa kupelekwa Tabora kikazi, aliona asiende na familia kwa sababu fulani fulani hususani masomo na mama yake aliyekuwa ana clinic pale Muhimbili. Wiki nzima tulikuwa tunalia tu huko kwenye makazi mapya, nyumba haikuwa na umeme tuliozoea, mazingira hatukuyaelewa sababu ya utoto.

Wazee wa bata, Tabata imetoka mbali, mwaka huo 1988 hakukuwa na lami, mji ukiishia Tabata magengeni opposite na kanisa la Kristo Mfalme, maeneo ya Liwiti, Baracuda mpaka Segerea ilikuwa ni machimbo rasmi ya mchanga, mchanga wote wa kujengea daslama yote ulitoka Segerea, maeneo ya Liwiti kulikuwa na kota za TAZARA, mbele kidogo kota za kiwanda cha sigara, hapo Baracuda kulia kota za chuo cha ufundi Chang'ombe sasa VETA, Kinyerezi na Kifuru ilikuwa msitu mkubwa sana na Simba walikuwepo

Ukiwa mgeni utachanganya na haya majina, maana Tabata kuna posta, Chang'ombe na sigara, majina ambayo yanapatikaña maeneo mengine ya jiji.

Tabata enzi hizo ikiwa na baa kubwa mbili tu, Hai bar ya mzee Mushi na Camp bar ya mzee Mmari, wachaga shikamooni mlijua kuchungulia fursa kitambo.

Hakukuwa na bar ya maana zaidi ya gloceries., hapo Hai bar walikuwa wakionyesha sinema za bluce lee, mithun chakrabot, govinda ,etc,

Tabata nyumba zenye umeme zilikuwa za kuhesabu, maji ya bomba ilikuwa anasa ni visima kwenda mbele, kutoka Mandela road mpaka Liwiti ungetumia takriban lisaa lizima kwa gari, barabara ilijaa mashimo.

Dalili njema ilianza kwa kupata jengo la Aroma, timu ya pamba ikiwa na akina Fumo Felician, George Masatu, Hussein Masha, Khalfan Ngassa ilikuwa ikifikia hapo na kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Tabata shule au Tabata shooting Stars, siku hizi kuna shule ya St Marrys.

Simba pia walikuwa wakifikia kwenye guest house ikijulikana kama sparkland maeneo ya ubayaubaya.. Tabata Kimanga ilikuwa ni mapori tu, viwanja vya Serikali vikiuzwa kwa sh 1200 lakini watu walikataa eti ni porini, ni mpaka Juma ikangaa na National Housing walipoanza kujenga maeneo ya Mawenzi watu wakaanza kupaelewa.

Shule ya msingi Kimanga walisomea chini ya mwembe mpaka gazeti la mfanyakazi liliporipoti hali hiyo ndio mfadhili wa Simba Azim Dewji akajenga madarasa mawili, mpaka leo kwa wazawa ukitamka Kimanga kwa Dewji wanaelewa ni wapi.

Tabata siku hizi ina mastaa akina Ally Kiba, Dully Sykes, Mr Blue, Tunda man, Erasto Nyoni, Kapombe, Domayo.

Hali hii ya mazingira ilinisononesha sana japo nilikuwa mdogo nikasema ipo siku nitarudi Masaki iwe isiwe, imenichukua miaka 35 kutimiza ndoto yangu.

Mwaka huu mwezi March nilipata servant Quarter room moja ba choo ndani kwa laki mbili, nitaishi humo mpaka nizeeke au nifie humo maana uwezo wa kulipia nyumba nzima kwa dola 1000 kwa mwezi siuoni kwa siku za karibuni japo yote yanawezekana, Kumbuka nina makazi rasmi somewhere in town kwa ajili ya watoto na mama yao ambaye tulishatengana

Kumbuka enzi zile maeneo kama Mbweni na Mbezi Beach hayakuchukuliwa kuwa maeneo ya kifahari so akili yangu haikuyazingatia mpaka leo.

Kupanga ni kuchagua Usinipangie.
 
Kumbuka enzi zile maeneo kama mbweni na Mbezi Beach hayakuchukuliwa kuwa maeneo ya kifahari so akili yangu haikuyazingatia mpaka leo
Kuna wastaafu walipewa hayo maeneo miaka ya 1980 wakaanza kuyauza kwa bei ya chini wengine hawakwenda kabisa

Baadhi ya wenyeji wa Dar hasa wa Magomeni na Ilala miaka hiyo walikuwa na mashamba ya mihogo, mpunga na ndizi kule Mbezi Beach, Mbweni, Tegeta, Salasala waliishia kuyauza kwa bei ya kutupa.

Leo yamekuwa hot cake
 
Nilizaliwa nikajikuta niko mitaa ya Chole Oysterbay,
Mwaka 1988 kufumba na kufumbua roli aina ya Bedford limekuja nyumbani kutuhamisha kuelejea Tabata huwezi amini mizigo haikufika hata nusu ya roli lile,enzi hizo watumishi ukihamia nyumba ya serikali unakuta vitanda,nagodoro,sofa ,dinning table and chairs.Etc.
Kuja kugundua kumbe mzee anehamishwa kupelekwa Tabora kikazi,aliona asiende na familia kwa sababu fulani fulani hususani masomo na mama yake aliyekuwa ana clinic pale muhimbili.Wiki nzima tulikuwa tunalia tu huko kwenye makazi mapya,nyumba haikuwa na umeme tuliozoea,mazingira hatukuyaelewa sababu ya utoto

Wazee wa bata,Tabata imetoka mbali,mwaka huo 1988 hakukuwa na lami,mji ukiishia Tabata magengeni opposite na kanisa la Kristo Mfalme,maeneo ya Liwiti,Baracuda mpaka Segerea ilikuwa ni machimbo rasmi ya mchanga ,mchanga wote wa kujengea daslama yote ulitoka segerea,maeneo ya liwiti kulikuwa na kota za TAZARA,mbele kidogo kota za kiwanda cha sigara ,hapo baracuda kulia kota za chuo cha ufundi chang'ombe sasa VETA,.Kinyerezi na Kifuru ilikuwa msitu mkubwa sana na Simba walikuwepo

Ukiwa mgeni utachanganya na haya majina,maana Tabata kuna posta,chang'ombe na sigara,majina ambayo yanapatikaña maeneo nengine ya jiji.

Tabata enzi hizo ikiwa na baa kubwa mbili tu,Hai bar ya mzee Mushi na Camp bar ya mzee Mmari,wachaga shikamooni mlijua kuchungulia fursa kitambo.hakukuwa na bar ya maana zaidi ya gloceries.hapo Hai bar walikuwa wakionyesha sinema za bluce lee,mithun chakrabot,govinda ,etc,
Tabata nyumba zenye umeme zilikuwa za kuhesabu,maji ya bomba ilikuwa anasa ni visima kwenda mbele,kutoka mandela road mpaka liwiti ungetumia takriban lisaa lizima kwa gari,mbarabara ilijaa mashimo.

Dalili njema ilianza kwa kupata jengo la Aroma,timu ya pamba ikiwa na akina Fumo Felician,George Masatu,Hussein Masha,khalfan Ngassa ilikuwa ikifikia hapo na kufanya nazoezi kwenye uwanja wa Tabata shule au Tabata shooting Stars ,siku hizi kuna shule ya St Marrys.
Simba pia walikuwa wakifikia kwenye guest house ikijulikana kama sparkland maeneo ya ubayaubaya..tabata kimanga ilikuwa ni mapori tu,viwanja vya serikali vikiuzwa kwa sh 1200.lakini watu walikataa eti ni porini,ni mpaka Juma ikangaa na National Housing walipoanza kujenga maeneo ya mawenzi watu wakaanza kupaelewa.
Shule ya msingi kimanga walisomea chini ya mwembe npaka gazeti la mfanyakazi liliporipoti hali hiyo ndio mfadhili wa Simba Azim Dewji akajenga madarasa mawili,mpaka leo kwa wazawa ukitamka kimanga kwa dewji wanaelewa ni wapi.
Tabata siku hizi ina mastaa akina ally kiba,dully sykes,mr blue,tunda man,erasto nyoni,kapombe,domayo

Hali hii ya mazingira ilinisononesha sana japo nilikuwa mdogo nikasema ipo siku nitarufi masaki iwe isiwe,imenichukua miaka 35 kutimiza ndoto yangu

mwaka huu mwezi March nilipata servant Quarter room moja ba choo ndani kwa laki mbili,nitaishi humo mpaka nizeeke,au nifie humo maana uwezo wa kulipia nyumba nzima kwa dola 1000 kwa mwezi siuoni kwa siku za karibuni japo yote yanawezekana

Kumbuka enzi zile maeneo kama mbweni na Mbezi Beach hayakuchukuliwa kuwa maeneo ya kifahari so akili yangu haikuyazingatia mpaka leo

Kupanga ni kuchagua
Kubwa jinga
 
Sasa kama kumbe Lengo lako Kuu ( Mama ) lilikuwa ni kutaka tu Kutuambia na Kutuonyesha ( Kuturingishia Kimtindo ) kuwa Umezaliwa Oysterbay ( Ushuani ) kwanini umetumia njia hii ndefu na usingeenda tu Straight ili usitupotezee muda Kusoma huu Mkeka wako?
 
Mimi mpaka Leo mtu akisema anaishi Tabata bado simuelewi..namuona mtu wa starehe Sana aliekataa kukua...
Wengi starehe zimewakuta Tabata, hawakufuata starehe, mtoa mada ameielezea vizuri Tabata ninayoijuwa Mimi.

Kuna mshua mmoja marehemu Joseph Kessy inatakiwa awepo kwenye historia ya Tabata yeye ndio alikuwa mwenyekiti wa kamati ya wananchi kuboresha miundombinu ya Tabata mwanzoni mwa 90's.
 
Back
Top Bottom