Machungu ya kufungwa mabao 5 na Yanga ni moja ya matukio mabaya sana katika maisha yangu hapa duniani kwa mwaka 2023

1979Magufuli

JF-Expert Member
Feb 20, 2023
438
1,752
Huu mwaka sitousahau ktk maisha yangu, nimezaliwa mwaka 1979 hospital ya Ocean Road, nimeishi Chang'ombe, nimeishi Keko, nimeishi Mtoni kwa Aziz Ally, nimeanza kwenda uwanjani nikiwa darasa la pili mwaka 1989 nikitoroka madrasa keko nakimbia hadi uwanja wa shamba la Bibi nikipitia shule ya msingi Mgulani, naingilia chuo cha TTC ss hivi chuo cha DUCE, napitia kamlango kadogo cha chuo karibu na mnara ulikoanguka ndege ambako ss hv kuna uwanja wa mkapa, enzi hizo sisi watoto hatukupata shida kuingia uwanjani tofauti na ss hv, niliwashuhudia askari matata kabisa akina Mkama Sharp akiwa na kila silaha mwilini mwake huku akitembea kwa madaha, nimewaona akina Malboro na farasi wake akiwakimbiza wale waliokuwa wanaruka ukuta, enzi hizo uwanja wa uhuru ukuta ulikuwa mfupi sana, mwanaume akijiachia mbio akifika kwenye ukuta yuko ndani, nimemshuhudia askari mmoja akiitwa Charles yeye kumuachia mbwa akukimbize sio ishu kwake.Enzi zile kulikuwa na vioja sana.

Nimezishuhudia Nyota Nyekundu, Pilsner, Sigara, Tukuyu Stars, African Sports, Coastal Union, Yanga ya akina Joseph Fungo, Abubakary Salum, Issa Athuman, Said Zimbwe, Simba ya Mosses Mkandawile, Adam Seleman, Omary Hussein, John Makelele, Edward Chumila, Malota Soma, Adof Kondo, Juma Limonga, Rafael Paul, Twaha Hamidu, we acha.

Nimeshuhudia Simba ikiifunga Yanga mabao 5, nimeshuhudia Simba ikinusurika kushuka daraja kwa uzembe wa marehemu Sahau Kambi akimpa goli marehem John Makelele Zig Zag.Mpira wa Tanzania hanidanganyi mtu yoyote na niko tayar kukaa na mtu yoyote isipokuwa Gentamycine tu.

Simba ameonewa sana na yanga enzi za akina Ngozoma Matunda, akipigwa mabao 3 mara 2 lakini sio kufungwa 5.Simba ndio imekuwa na kawaida ya kumbabua Yanga mabao 4 na mwisho hv karibun mabao 5 tena yanga ilipokuwa na gogoro na Mwenyekiti wake Lloyd Nchunga.

MIGOGORO yoyote ya Simba enzi za akina marehemu Jimmy David Ngonya, cjui akina Bamchawi, cjui Juma Salum, cjui Priva Mtema niko hai, haya yanayotokea leo ya wachezaji kufungwa kishirikia wasicheze vzr hayakuanza leo, wengine ukisema haya wananiona mm sina hoja, mm napenda ushirikina, hayo yanayofanyika pale Avic sio madogo, utavaa hirizi hutaki hama timu, sio sisi huku uchale uchale mwingi tu ss hv.

Sasa yote kwa yote tunamaliza mwaka 2023, kiukweli kufungwa mabao 5 na wapuuzi wale kumeniuma sana, yaan kama ningekuwa na uwezo wale viongozi wote wa Simba ningewapeleka jela wakakae miaka miwili bila kesi, Bodi mzima ingejuta kuzaliwa, ila naendelea kumuomba mungu wale wote walioshiriki kuuza mechi hadi tukadhalilishwa namna ile yawakute yoyote yale, watajua wenyewe.

Mwaka 2023 sitousahau kamwe maishani mwangu.
 
Basi sawa; katika round ijayo nitamwambia Gamondi apunguze kidogo, ila sasa na nyinyi muwe na adabu mchunge midomo yenu mnapoizungumza Yanga
 
Bado mechi ya marudiano mkuu. Jiandae Tena kisaikolojia
 
kuna mzee alipata hypertension kisa mechi, kaanza kuangalia tena mpira match ya wydad wakiwa kwa mkapa. hizi team zinabeba hisia za watu wengi sana
 
watatumia nguvu sana mechi ijayo kocha itabidi aonyeshe ukocha wake awaache watumie nguvu halafu sisi tufunge kimkakati...
Hawana kingine Cha kutumika, zaidi ya nguvu. Maana kwasasa unyumbulifu na akili hawana. Tena mzunguko wa pili wakisema watumie nguvu, ndio watachezea nyingi.
 
Lakini hii JERO imewaumiza wengi sana.
Nina jirani yangu mzee flani kiherehere sana mpenzi wa simba, huwa akinikera Yanga tukifanya vibaya...ninamkumbusha kipigo cha 5:1 anapotea ghafla😂😂😂
 
Back
Top Bottom