Umeshapanga nyumba ngapi mpaka sasa?

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Harakati za maisha ya kujitegemea zinamambo mengi sana na tunapitia mengi sana hususani kwenye nyumba za kupanga.

Kwa ujumla Mpaka hivi sasa tangu nimeanza kupanga nyumba Kwa miaka 10 nimefanikiwa kuhama nyumba zaidi ya Saba ikiwa Kwa sababu mbalimbali

Nyumba ya Kwanza
Nakumbuka nyumba ya Kwa kuishi ni maeneo ya tabata BIMA Karibu na Kota za nssf ambapo nilipanga chumba kimoja kama msela Tu sina mke, mwenye nyumba ni mama mjane wa kichaga nilikaa Kwa muda wa Mwaka mmoja tukashindwana Baada ya kunipandishia Kodi kiholela nikahama

Nyumba ya pili
Liwiti tabata Karibu na barakuda hii nyumba ilikuwa ya urithi nayo Ila wamiliki ni watoto wa Marehemu nyumba ilikuwa nzuri Tu na sio mbali na road Ila Shida ilikuwa haina msimamizi kila mtoto anakudai Kodi wew ukishindwa kuwabananisha ndugu utalipa Kodi mara mbili sijui walikuwa wanafanya makusudi au la.

Nyumba ya tatu
Hii ilikuwa maeneo ya tabata shule Kwa nyuma mwenye nyumba ni mtu wa dini sana nakumbuka hii nyumba nilikaa miezi miwili Tu nikapewa notes ya kuhama Kwa kigezo cha Mimi kuingiza mwanamke ndani ya nyumba
Mwenye nyumba alikuwa hataki uzinzi ndani ya nyumba yake nikahama.

Nyumba ya nne
Hii nilikaa Kwa siku 6 nikashindwa nakaomba niludishiwe hela yangu nikaambiwa na mwenye nyumba hela Hana nikaongea na dalali akaleta mpangaji mwingine akanilipa pesa nikaondoka Shida chumba kilikuwa kidogo kupelekea baadhi ya vitu vyangu kubaki nje.ingawa nyumba ni mzuri maana hii nilionyeshewa kwenye WhatsApp na dalali Baada ya Mimi kuwa bize na kazi

Nyumba ya tano
Hii nilikaa maeneo ya tabata BIMA pale nyuma ya st Mary nyumba hii nilihamia Wakati wa kiangazi bila ya kujua kuwa nimeingia cha kike Kwa sababu Wakati kiangazi ni sehemu nzuri sana Ila ikinyesha mvua Bana maji yote ya barabarani yanaingia ndani kipindi hiko Ile Njia haijapigwa lami na haina mitaro yaani kufumba na kufumbua unaamka asubuhi maji yamejaa chumbani. Hii nyumba nilikaa miezi minne nikasamehe Kodi ya miezi miwili

Nyumba ya sita
Hii nyumba nilihamia Baada ya kutoka kwenye mafuriko nikakaa hapa Kwa muda ya miezi sita ya Kwanza ilikuwa na Amani tatizo lilikuja Baada ya binti ya mwenye nyumba kuhamia hapo ndani yeye maisha yalimpiga pamoja na Bwana wake ikabidi warudishe mpira Kwa kipa .akatengeneza mazingira ya kunizoea akafanikiwa sasa ikawa mazoea yamepita mipaka maana alikuwa anapenda kitonga mnoo anakuja kuomba chumvi,sabuni mara sukari ikawa maisha Yao Mie ndio nayaendesha na akiazima kitu harudishi nikapiaga hesabu nikaona hii nyumba hainifai nikahama

Nyumba ya Saba
Nyumba hii nilikaa Kwa Mwaka mmoja na nusu mwenye nyumba jamaa mmoja anapiga mishe kariakoo Ila mkewe ni mganga hili sikujua Wakati nahamia,nilikuja kujua Baada ya kusikia harufu za ubani na udi zilizokuwa zinafukizwa ndani ya nyumba nikajua labda ni dawa za mbu,Kumbe mama alikuwa anapandisha maruhani
Nakumbuka kwenye hii nyumba niliishi Kwa misukosuko sana na màmbo yangu mengi yalikuwa hayaendi huyu mwenye nyumba hapendi mpangaji awe na maendeleo nilikuja na friji akataka nimuuzie nikagoma akanipandishia hela ya umeme Wakati na yeye Pia anafriji mbili na anauza barafu,juice na ice cream ndipo nikashikwa sikio na wadau wa mtaa nikaambiwa huyo mama mwenye nyumba ni jau na anatabia ya kuroga wapangaji. Duh nikahama

Nyumba ya mwisho
Hii nyumba ilikuwa ni mpya kabisa wapangaji tulikuwa watatu tu na mwenye nyumba haishi na Sisi. nimeishi Kwa Amani sana tena ilikuwa kama yangu nakumbuka Wakati nahamia dalali aliniambia hapa utaishi kama kwako na ukitoka hapa utahamia kwako na kweli nilikaa hii nyumba takribani miaka minne na nusu nikafamikiwa kujenga yangu na kuoa na kupata na mtoto mpaka nahama kuna watu walijua pale ni kwangu Kumbe ni nyumba ya kupanga Tu.

Hii ndio experience yangu kwenye nyumba za kupanga sijui kwako mdau ikoje
Nawasilisha
 
Sitajibu swali lako ila ushauri kwa wasomaji :unapotafuta nyumba/chumba cha kupanga hakikisha mwenye nyumba anaishi mbali sana na nyumba yake ikiwezekana nje ya mkoa pia awe na kazi yake ya kumuingizia kipato sio kutegemea pesa ya vyumba ndoitatue shida zake.Hapo utakataa mpaka utakapokuja kujenga au kuhama mji
 
Nilipoanza chuo nilihangaika sana kutafuta nyumba ya hivyo, nikaipata na mpaka namaliza chuo sijawahi kumuona mwenye nyumba wala kuongea naye. Ni kutoa hela kwa msimamizi wake mambo mengine mtajua wenyewe
 
Niliwahi kupanga nyumba moja muda kidogo maeneo ya Buguruni karibu na spenko. Ile nyumba kwanza ilikuwa na vyumba zaidi ya 30 alafu vidogo kama stoo, mwenye nyumba hana time na mtu we rudi muda wowote unaotaka utakuta mlango wazi haufungwi, mwenyewe anakwambia me nipe tu kodi yangu nikalewe ila ulinzi wa chumba chako utajua mwenyewe

Ilikuwa na watu kinoma! Waha walikuwa kibao wamejaa chumba kimoja. Ile nyumba ilikuwa imepigwa machata "Meli ya wagiriki" kila kona. Nikasema hapa sio pa kuishi inabidi nisepe tu, nikachil miezi 6 nikasepa
 
Mimi nlienda kujiendeleza kielimu ukubwani. Nkapata chuo makao makuu.
Kwanza nlikaa lodge siku 10 natafta nyumba. Hizo changamoto ni za siku nyingine. After 10 days ndo nkapata nyumba. Chumba na sebule self.

Maza house n mlokole, ana sheria kama 2. Hapangishi waislamu, na pili hapangishi singo boi. Bas nkampeleka mchumba wangu kuiangalia, alivoskia hyo sheria akasa hapa hapa hakuna kwenda kwingine usije niletea vimada. Nkahamia.

Kwakweli nmekaa pale kwa starehe zote. Mwanzon nililipa kodi ya miez 4. Ilivoisha nkapauka kbsa nkakosa hadi nauli. Mungu ni mwema nkapata kibarua huku nkiwa shule, ikabd nimchane maza haus kua nkilipa kodi ya miez 3 ndo mshahara wangu wote na kazi nmepata mkoa mwingine, anivumilie hata miez 2 nimlipe kwa mwezi mwezi wakat najipanga.

Akasema subr atajadili na mumewe. Kesho yake nkapokea text kua amekubaliana na mumewe nilipe kwa mwezi hadi mwezi wa 9 (hapo ilikua mwezi wa 3).

Nmelipa kwa mwezi kama bili ya maziwa, kufikia mwez wa 9 akanitumia text ingine kua ntaendelea hvo hvo hadi ntakapoona nna uwezo wa kulipa miez 3 mitatu.

Nlisoma mpka nkamaliza na hadi leo bado nipo. Kila tar 30 mwenyewe bila kuulizwa naenda kuweka hela benki. Nmekua kama mwanae, hata vijana wake wakizingua naitwa mimi nkawashauri.

Hakuna mambo ya leo zamu yalo umeme sijui maji, kila kitu nalipa mwisho wa mwezi imeisha hyo. Kuna miti ya matunda nakula kama kwetu, nkisafiri lazma nimfungashie mazagazaga, naeza ondoka hata miez 6 na ufunguo nmeacha dirishani na ntaukuta hvo hvo hakuna chochote kimeguswa.

Mungu awape maisha marefu
 
Wapangaji na nyinyi kwenye nyumba za watu mnakuja na tabia zenu! Uzinzi mwingi ujuaji, kutokutaka kujishughulisha na chochote unapoishi zaidi ya kulipa Kodi! Bili zingine una malalamiko yasiyoishaHii hasa Hawa masela wanaotaka chumba kimoja! Unampangisha mmoja kesho unakuta wapo watatu au zaidi! Eneo la kistaarabu wao mziki mkubwa hata usiku! Mambo kama hayo huwezi kudumu kwenye nyumba moja! Mwenye nyumba awe anaishi karibu au anaishi mbali kama ni mstaarabu utaishi tu vizuri!
 
Sitajibu swali lako ila ushauri kwa wasomaji :unapotafuta nyumba/chumba cha kupanga hakikisha mwenye nyumba anaishi mbali sana na nyumba yake ikiwezekana nje ya mkoa pia awe na kazi yake ya kumuingizia kipato sio kutegemea pesa ya vyumba ndoitatue shida zake.Hapo utakataa mpaka utakapokuja kujenga au kuhama mji
@Mpwayungu Village leo umeongea kwakifupi ila kwakina sana, wewe ni Great thinker
 
Niliwahi kupanga nyumba moja muda kidogo maeneo ya Buguruni karibu na spenko. Ile nyumba kwanza ilikuwa na vyumba zaidi ya 30 alafu vidogo kama stoo, mwenye nyumba hana time na mtu we rudi muda wowote unaotaka utakuta mlango wazi haufungwi, mwenyewe anakwambia me nipe tu kodi yangu nikalewe ila ulinzi wa chumba chako utajua mwenyewe

Ilikuwa na watu kinoma! Waha walikuwa kibao wamejaa chumba kimoja. Ile nyumba ilikuwa imepigwa machata "Meli ya wagiriki" kila kona. Nikasema hapa sio pa kuishi inabidi nisepe tu, nikachil miezi 6 nikasepa
 
Nimepanga nyumba 2.

1, hii nilipanga wakati ndo naanza chuo, hapa mwenye nyumba alikuwa mkoa huu ila wilaya nyingne, tulikua wapangaji 5, palikua vizuri tyuuh, shida ni mke wa mpangaji m1 ni mama wa nyumbani, duuh yule mdada sijui wa wapi, yaan alikua kero tupu kwangu, afu alikua km ana gubu fulan kwangu, na alikua mswahili pia, nkawa navumilia, ila baada ya kunusurika kuporwa na vibaka, sikulaza damu nkahama, wakat huo bado kodi ya miez 4, nkaaongea na mwenye nyumba akanambia kwa kuwa mie ndo nakatisha mkataba sikupaswa kupewa chochote, ila kwa yeye ustaarabu wake atanipa kodi ya miezi 2, kweli akanipa nikasepaaa, yeye akabakiwa na kodi ya miezi 2 pia, tuligawana pasu pasu.

2, hii ndo naishi hadi sasa, tupo wapangaji wa 4, mwenye nyumba yuko mkoa, hatujawahi kumuona wala hatumjui, mambo ya kodi tunamalizana kwa miamala ya cm, km ikitokea shida ana toa maelekezo tyuuh, hapa napapenda wote wana kazi zao tena nzuri, ila Jobless ndo mie pekee angu, hakuna kitu cha kushare, na kila mtu yuko buzzy na life lake, yaan inaweza pita hata week hujaonana na jirani, tatizo likitokeaa km linahusu kwa wote tunajulishana kwa cm, hapa bado nipo sanaa.

.......
 
Sitajibu swali lako ila ushauri kwa wasomaji :unapotafuta nyumba/chumba cha kupanga hakikisha mwenye nyumba anaishi mbali sana na nyumba yake ikiwezekana nje ya mkoa pia awe na kazi yake ya kumuingizia kipato sio kutegemea pesa ya vyumba ndoitatue shida zake.Hapo utakataa mpaka utakapokuja kujenga au kuhama mji
Kweli kabisa nyumba za kupanga kero ikiwa mwenye nyumba anategemea kodi kuendesha maisha yake
 
Sitajibu swali lako ila ushauri kwa wasomaji :unapotafuta nyumba/chumba cha kupanga hakikisha mwenye nyumba anaishi mbali sana na nyumba yake ikiwezekana nje ya mkoa pia awe na kazi yake ya kumuingizia kipato sio kutegemea pesa ya vyumba ndoitatue shida zake.Hapo utakataa mpaka utakapokuja kujenga au kuhama mji
Sure. Ndio nakaa nyumba ya ivyo. Yaani hakuna shida kabisa jamaa nilimuona juzi juzi tu alikuja kwaajili ya ukarabati. Ndani ya miaka miwili ndio nimemuona mwezi uliopita.
 
Nimepanga nyumba 2.

1, hii nilipanga wakati ndo naanza chuo, hapa mwenye nyumba alikuwa mkoa huu ila wilaya nyingne, tulikua wapangaji 5, palikua vizuri tyuuh, shida ni mke wa mpangaji m1 ni mama wa nyumbani, duuh yule mdada sijui wa wapi, yaan alikua kero tupu kwangu, afu alikua km ana gubu fulan kwangu, na alikua mswahili pia, nkawa navumilia, ila baada ya kunusurika kuporwa na vibaka, sikulaza damu nkahama, wakat huo bado kodi ya miez 4, nkaaongea na mwenye nyumba akanambia kwa kuwa mie ndo nakatisha mkataba sikupaswa kupewa chochote, ila kwa yeye ustaarabu wake atanipa kodi ya miezi 2, kweli akanipa nikasepaaa, yeye akabakiwa na kodi ya miezi 2 pia, tuligawana pasu pasu.

2, hii ndo naishi hadi sasa, tupo wapangaji wa 4, mwenye nyumba yuko mkoa, hatujawahi kumuona wala hatumjui, mambo ya kodi tunamalizana kwa miamala ya cm, km ikitokea shida ana toa maelekezo tyuuh, hapa napapenda wote wana kazi zao tena nzuri, ila Jobless ndo mie pekee angu, hakuna kitu cha kushare, na kila mtu yuko buzzy na life lake, yaan inaweza pita hata week hujaonana na jirani, tatizo likitokeaa km linahusu kwa wote tunajulishana kwa cm, hapa bado nipo sanaa.

.......
Hapo usihame, ni nadra sana kupata makazi hayo
 
Kiukwel Toka nifike dar nimeama nyumba 6

Hapa hii nyumba ya 6 niliyopo Kwa ss mmilikii n mama aliyepitiaa kilaa aina ya tabu Kwenye maishà yake (Kwa mujibu wake alinisimulia) Toka niamie n mwaka wa 2 ss hakikaa tometoka kuelewana Sanaa na nimemfanya km mama yangu maana daaaa cjui nisemejee
 
Back
Top Bottom