WAZIRI MWIGULU , WANAODAIWA NI WALIPA KODI SI SERIKALI
Laiti Ndugai angesimama na hoja yake kungelikuwa na mjadala mzuri na endelevu
Kwa mfano, Mawaziri na watu wanaosema nchi zote zinakopa hawaelezi ukweli ulivyo
Nchi kama Marekani inakopa lakini deni lao linakuwa ''monitored'' na Mabunge
Mara zote utasikia mgogoro wa 'debt ceiling' kwa maana ukomo wa kukopa
Hatuwezi kukopa bila kuwa na utaratibu na hapa Spika Ndugai ana hoja
Hoja yake inajijibu, mikopo na Bajeti zinapita mikononi mwake, mbona hakuyasema Bungeni? Hii haimaanishi hana hoja, ipo lakini amejivuruga vuruga sana kwa njia nyingi
Hakulaumu Bunge kupitisha miswada ya pesa! hakuongelea mikopo bungeni
Huko nje alipoongelea amekenguka na kuomba misamaha
Leo Waziri Mwigulu kasema hakuna Mtanzania atakayegongewa au kuchukuliwa ng'ombe kwa ajili ya kulipa deni. Deni linalipwa na serikali.Kauli ya Waziri ni upotoshaji mkubwa.
Serikali haina chanzo kingine cha mapato isipokuwa Wananchi.
Japo hawatogongewa hodi milangoni , watagongewa hodi za kulipa madeni kupitia Miamala, sukari, mabati, chumvi, dawa n.k. Hivyo wananchi wanalipa deni na si serikali
Hoja nyingine ya Waziri Nchemba ni kuhusu watu kumsingizia Rais kwamba anakopa.
Waziri kasema Rais hakopi ni serikali. Hili ni kweli kabisa kwamba serikali ndiyo inayokopa
Anachosahau Waziri Nchemba ni kuwa Viongozi ndio wanamsingizia Rais pale wanapowaambia wananchi Rais katoa pesa za madawati, vyumba, Hospital n.k na kwamba Wamshukuru yeye si Serikali.
Sasa inakuwaje tabu au tatizo kwa watu wale wale wanaoamini kuwa Rais kawaletea kitu fulani kutoamini Rais huyo kaenda kukopa?
Viongozi wanambebesha Rais mzigo huu unaoitwa ''kukopa' badala ya serikali kwasababu viongozi hao kwa kujipendekeza husema ''Rais kawaletea abcd au katoa pesa abcd''
Kauli zote za kujichanganya ni katika kumjibu Spika Ndugai na hoja ya kukopa
Kwa bahati mbaya wengi hawajibu hoja wanajibu kisiasa, lakini Spika ajilaumu kwa ''kuuza ghala la silaha'' kwa kuomba msamaha kwa jambo lenye tija, hana pa kusimama anapigwa kutoka kona zote, anadhalilishwa na kabaki tu kama Spika lakini heshima hakuna
Katika sintofahamu hii hakuna namna nyingine ni Spika ajiuzulu
Kawavuruga wenzake na msamaha wake '' hajapokelewa'
Spika Ndugai it's time to go!
Alinda