RAIS NA KIONGOZI WA MHIMILI MWINGINE 'HANA IMANI'
SPIKA AMEPOTEZA IMANI YAKE KWA BUNGE NA CHAMA
Jana Jumatatu Spika wa Bunge la JMT Mh Ndugai alifafanua kauli ya 'mikopo na mnada wa nchi'
Spika alijitokeza baada ya 'kushukiwa vikali' na makundi ya chama na viongozi wa serikali
Spika alisema 'amenukuliwa vibaya, kipande cha video kinachozunguka si sahihi kwa alichosema'
Mwisho wa ufafanuzi ,Spika alimuomba radhi Mh Rais na Wananchi kwa ''usumbufu'' uliojitokeza bila ufafanuzi ikiwa atawachukulia hatua gani waliosambaza kipande cha video.
Mh Spika hakukana sauti ya video au kutilia shaka iwapo video imechezewa
Alichosema imepotoshwa bila kuonyesha wapi na kwa vipi.
Swali linafuata, je, alichukua hatua gani dhidi ya vyombo husika? na kwanini ilimchukua muda mrefu kujibu hoja yenye hisia kama ilivyo?
Mh Spika anasema alikuwa mgonjwa na kutoweza kujitokeza, hata hivyo ofisi ya Spika ni kubwa ingeliweza kutoa taarifa za awali ikisubiri hali ya Mh kuimarika. Hili halikutokea
Kabla ya mkutano mitandaoni kulikuwa na mazungumzo kwamba atapojitokeza atasema 'amenukuliwa vibaya' Huu ni utamaduni wa viongozi wanapokwepa kukiri au kuomba msamaha kwa matendo au kauli zao
Jumanne ya leo ndani ya Ikulu kulifanyika hafla ya taarifa ya utekelezaji wa mpango wa serikali unaohusiana na pesa za mkopo unaozungumziwa kwa utata
Viongozi wote wa serikali na chama walisomeka kwa kauli zao 'kumshambulia' Mh Spika
Mh Rais alionekana kukereka na ukweli kwamba 'taarifa za mikopo zinapita katika nyumba ' na kisha mtu anasema yaliyosemwa
Mh Rais anasema nguvu yake ni kutokana na kuungwa mkono na Wananchi katika sakata hili
Na kwamba ''wanaotazama 2025' waondoke wakajiandae vizuri
Ukifuatilia kwa undani msamaha wa Mh Spika haukupokelewa na mhimili wa serikali achilia mbali Chama chake
Mh Spika alikuwa na machaguo mawili.
Kwamba asimame na kile alichosema akiamini ni maoni yake, au
Kutoomba radhi asubiri kutetea hoja zake kwa mantiki bila kujali nini kitafuata
Kitendo cha kutochukua hatua dhidi ya ''wapotoshaji' na kitendo cha kuomba msamaha kinamwacha na chaguo moja 'Ajiuzulu'
Mh Spika atakuwa amepoteza ''vote of confidence' kutoka ''Caucus'' ambayo ni asilimia 90+
Mh Spika amepoteza 'Vote of confidence' katika Chama kufuatia matamko ya viongozi
Mh Spika amepoteza 'vote of confidence' kwa kiongozi wa Mhimili mwingine, hakusimama na kauli yake
Katika nchi nyingine hili la mihimili kutofautiana ni la kawaida, kwa nchi yetu ambako kuna mihimili imejichimbia, hili si la kawaida na linamwcha pagumu
Katika mazingira hayo Mh Spika hana pa kusimama tena kwa maana ya kwamba haungwi mkono na sehemu yoyote ya jamii japo kwa uwazi na amebaki kisiwani
Spika alipaswa kufanya alichofanya Waziri wa fedha enzi hizo bwana Edwin Mtei.
Mtei alipotofautiana na Mwl Nyerere kuhusu sera za nchi kwendana na matakwa ya IMF na WB, alijiuzulu. Miaka mingi baadaye ilibainika Mtei alikuwa Sahihi kwa maamuzi
Hadi leo Mzee Mtei anabaki heshima yake na ''role model'' ya namna gani viongozi wanapaswa kusimama na hoja zao kwa kuamini kile wanachoamini
Spika Ndugai hana uungwaji mkono ,hata kama ataendelea, kazi itakuwa ngumu sana
Kila kauli yake itakuwa sawa na kutembea juu ya miba.
Hii italiacha Bunge kupoteza nguvu zake zote kwasababu Spika ni 'symbol' ya Bunge
Mh Spika ni wakati wa Kujiuzulu, hakuna ajuaye nini kitatokea ndani ya chama chako.
Ikitokea vinginevyo aibu itakuwa kubwa kuliko ilivyo sasa.
Ni wakati ufanye tathmini na uchukue uamuzi mgumu
Jiuzulu, usimame na kile unachoamini , siyo dhambi wala kosa! ni ukomavu na ubaki mbunge
Sehemu II tutaangalia ufafanuzi wa deni na kauli za nchi duniani zinakopa
Tusemezane