Rais2020
JF-Expert Member
- Jul 14, 2016
- 3,248
- 5,532
Mods bhana. Uzi wangu wameuleta tena hapa. Dah!Wakuu amani iwe kwenu.
Nimeshawishika kununua bastola maana naona vibaka wanatishia sana amani hii mitaa yetu. Na hali hii imepelekea hadi sisi wanaume wa Dar kudharaulika kuwa tunaogopa vijana wanaojiita taifa jipya. Na mpaka Waziri wa mambo ya ndani naye kashangaa kuona wanaume wa Dar tunakimbilia chumbani pindi tunapowaona hawa vijana wanaojiita taifa jipya na panya roads.
Naomba mnifahamishe bastola inauzwa bei gani na zinapatikana maduka gani?
Je, kuna masharti gani au vigezo gani natakiwa kukidhi ili kuinunua?
Nawasilisha.
Rais2020