Nape: Lowassa ameanza kufanya kampeni, yuko hatarini kuenguliwa

Nape: Lowassa ameanza kufanya kampeni, yuko hatarini kuenguliwa

Suala hili linaweza kuwa na mshindo mkuu,ila bado naamini serikali ipo haijaenda likizo na itajua tu kumaliza harakati hizi za watu kwa misingi ya kisheria,hatupaswi kutoka povu sana
 
Wana JF,

Nilikuwa kifuatilia Katibu mwenezi Nape akitoa angalizo la kumzuia kada mwezake Mh. Lowasa kuacha maigizo ya kuwapa fedha na kurudishiwa tena na makundi mbali mbali kwake. Mashambuliza yalimlenga moja kwa moja kwa kujiteua kuwa msemaji wa chama kwa kujifanyisha mikutano na kutoa tamko kuwa kuendelea kupokea wageni feki wanaomuunga Lowasa kunaweza kumsababishia kukatwa jina lake kwenye kiny'anganyiro cha kugombea urais. Nape amekuwa wa kwanza kusahau maigizo wanayoyafanya yeye na Kinana kuvutia watu au kuwavuta watu waje kwa wingi kwenye mkutano, mfano wametumia fisi, wamesomba watu kwa malori, wamewasimika wanachama hewa waliofukuzwa zamani chadema.

Vita ya urais haiwezi kuisha kiurahisi hivyo kwani hii taasisi ni mzito muno, mwacheni Lowasa agawe vipesa vyake angalau atakayeambulia vijisenti avipate tu, nyie mnaowapa T-shirt , kofia na kanga wakati wa kampaini sio kujipendekeza?

Mbwa ni mnyama ambaye hupenda sana vitu vizuri, ni mjanja sana katika kumpokea na kumshawishi boss wake ampende , katika kujipendekeza kwake huwa hapendi mnyama yoyote amsogelee , yupo tayari kuua kwa sababu ya kumlinda bosi wake au kwa sababu ya wivu boss asikalibiwe, lakini panapotokea paka akaanza tunyimbo twake boss umfuata na kumbeba na kumpa maziwa wakati mbwa anamwambia toka nenda wakakurudishe kwenye kamba. Hivyo kujipendekeza muhimu na si kila ukijipendekeza utapendwa bali unaweza usithaminiwe.

NB : Mfano wa Mbwa haumhusu mtu yeyote.
 
Binafsi nilikwenda Monduli kwa gharama zangu na pia nilimchangia Lowasa pesa ya kuchua fomu bila kushawishiwa na mtu.
 
k mmaam ..keeeeee........ hapatakalika,. Ole wenu.

Lowassa Raisi
 
Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema kitendo cha mgombea mmoja anayepokea makundi ya watu ili wamshawishi kupiga kura huko Dodoma ni kuanza kampeni na yuko hatarini kuenguliwa.

Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa ndiye anayepokea makundi ya watu wakiwemo masheikh, maaskofu na wanafunzi wakimshawishi kugombea.

Akizungumza na radio VOA, Nape alisema: "Labda niweke vizuri hili, mtu yoyote anayekiuka kanuni hatapitishwa labda kamaa anakwenda kugombea kwa chama kingine.

"Kinachofanyika Dodoma cha watu kuchukuliwa na magari huku wengine wakiwa hawajui, halafu wakifika wanakuta viti vimeshapangwa na vyakula;halafu eti wanamshawishi kugombea, ni kukiuka kanuni na anaweza kuondolewa," alisema Nape.

Mimi nashangaa kwa nini Nape alalame kuhusu mwenzake Lowassa kutembelewa nyumbani kwake. Yaani mgeni akija kwako hasinywe hawezi kunywa soda? Huu ndio utaratibu CCM mmekuwa mnautumia kukodi magari kupeleka watu kwenye mikutano yenu huku mkiwaandalia ubwabwa!! Kama yeye ni mwanachama wa CCM, kuna ubaya gani kama akitumia SOP (Standard Operating Procedure) ya chama? Hizi pics hapa chini zinawakilisha that particular chama's SOP.

attachment.php


attachment.php


attachment.php


attachment.php
 

Attachments

  • Capture1.JPG
    Capture1.JPG
    91.5 KB · Views: 583
  • Manjee2.JPG
    Manjee2.JPG
    92.4 KB · Views: 573
  • Manjee1.JPG
    Manjee1.JPG
    82.9 KB · Views: 574
  • Manjee.JPG
    Manjee.JPG
    74.8 KB · Views: 560
Haya yote yanaaeleweka vizuri kabisa.Ni uchovu tu wa wanasiasa.

Nape ni CCJ.
Livingstone Lusinde ni ni Chadema .
J.Makamba amebebwa kwa nguvu ya baba yake.
Samwel sita ni CCJ
Benard Membe ni CCJ
Makonda ni CCM madaraka.Bila madaraka atahama na kujiunga na ACT ili apate angalau udiwani.
Mwakyembe ni CCJ
Wasira ni NCCR Mageuzi.
Magufuli ni CCM asiye na histori ndefu ya kukitumikia chama katika shida na raha.
Sumaye ni CCM madaraka.Mana alishasema akienguliwa atatafuta chama kingine.
Hawa wote wanacheza ngoma na nyimbo za Chadema.
Tumeona Nape na hilo Kundi lake wakifurahia kifo cha marehemu capt Komba huku wakisahau mazuri yote aliyoyafanya kukijenga chama cha mapinduzi katika uhai wake wote. Hawa ndio watu wanaosema wanakipigania chama.

Kinana ni CCM halisi ndio maana anajua mbinu za kukijenga chama.

Lowassa ni kati ya makada wa kweli wa CCM waliobakia. Kumuengua Lowassa kwa sababu ya kusikiliza kelele za wapita njia litakua ni jambo la kipuuzi na lisilokubalika.

Eti wanasema kwa nini watu wanakuja na kukuta viti vimepangwa na chakula.Ni akili za ajabu kabisa. Kwa ulimwengu wa sasa hivi wageni waje bila kutoa taarifa.
Hata kwa mila zetu za kiafrika mtu akienda kuposa anatoa taarifa kwa wakwe ili wajiandae kupokea ujumbe unaoletwa wa posa.Na usipotoa taarifa basi linakua ni jambo lisilokubalika.

Simu na mitandao iko kila mahali halafu mtu aende kwa mtu bila taarifa.
Ndio maana viongozi wa dini kwa muda mrefu wamepima wakagundua kuwa Lowassa ana hekima kuliko hawa waruka njia ,Nape na kundi lake.Kwani hata hoja zao za kumshambulia Lowassa ni za kijinga na chuki tu.
Eti watu wanazolewa bila kujua kinachoendelea halafu wanapelekwa kwa Lowasa kupewa hela.Hivi kweli inaingia akilini Msomi wa Chuo kikuu azolewe bila kujua anakoenda?

Hivi kweli unaweza ukamzoa mchungaji au shehe ukampeleka asikokujua na akakubali kwenda.
Viongozi wa dini siku zote wanapenda viongozi wasikivu.Na wamegundua kuwa Lowassa hana makuu.

Nape muda Mrefu amekua akionekana dhahiri sio kutumia nafasi aliyo nayo kuhakikisha kuwa anatumia Muda mwingi kupambana na Lowasa ili alete Mtu wake anayemtaka.

Mnafiki na Joka la Mdimu siku zote hawana jema.
Ingetokea wale wachungaji ,mashehe na wanafunzi wa vyuo wakaenda kimya kimya kwa Lowassa bila taarifa na kufika bila hata mashahidi ikiwemo waandishi wa habari basi leo hii Lowasa angekua ameshaitwa kwenye kamati ya maadili na kuhojiwa kuwa anafanya kampeni na vikao vya siri.Ingekua ni ishu kubwa kweli kweli.
Hii ndio tabia ya wanafiki walovamia ndani ya CCM na sasa wanataka kuwaengua makada wa komavu wa chama na serikali ili wapitishe wanachama wenzao wa CCJ!!!

Membe kaamua kufukua yale Mabilioni ya marehemu Gadafi aliyokwapua kisha akamua balozi ili kuficha ushahidi, hizo pesa sasa zinatumika kumchafua Lowasa hata Nape sasa ni Mtumwa wa Membe kila analowambia na Membe yeye huropoka pasipo kujua kuwa kuna leo na kesho.
 
Upepo wa kisiasa umeanza kumwendea vibaya Mh Lowassa hasa baada ya makundi mbalimbali kwenda kumshawishi agombee urais. Baadhi ya viongozi wa chama wanasema ameanza kampeni kabla ya kingenga kupulizwa. Je, ikitokea jina lake likaenguliwa na vikao vya chama na ilhali "anakubalika kwa wananchi", ni kitu gani kinaweza kutokea kwake binafsi na kwa CCM?
Ni mwendo wa KANU kule Kenya CCM itakuwa chama cha Upinzani kwa itagawanyika na kuwapa mwanya Chadema kuchukua Nchi kisha Lema atakuwa Waziri wa mambo ya ndani, sikilizia balaa lake kila mkutano wa CCM Polisi watatoa vipigo ile mbaya.
 
Kikwete katika vita hii ya URAIS anasukumwa na jinsi gani anaweza kumpata mgombea ambae atamjenga mwanae Ridhwani na mkewe kisiasa baada ya yeye kung'atuka mwezi wa kumi; kigezo hicho ndio kinachonifanya niamini kuwa Kikwete atamtosa Edward na kumpigia debe Membe ambae katika MOU yao atamuachia mkewe ubunge huko Lindi na atamlea Ridhwani kisiasa ili baadae nae aje apate uongozi!! Dhaifu akumbuke tu kwamba hakuna sitting president aliyefanikiwa kuwachagulia wananchi mrithi wake na yeye is no exception!! I stand to be proven wrong!! Hata kama watamtosa Edward lakini kwa hakika magamba hawawezi kumpa Membe.!!!!
Membe si Chaguo la JK alishamtosa kitambo hawamtaki baada ya kugundua kuwa alimuua balozi wa Libya kisha akachukuchia mapesa ya marehemu Gadafi, hawataki Rais ajae awe Rais wa Mahakama ya The Hague kwa Uhalifu juu ya binadamu, wanamjua Membe ni mpenda Visasi atawafunga na kuwaua wapinzani wake, chagua la Jk ni pinda au kinana na akishindwa atakuwa kwa Lowasa au Wasira.
 
napekapewa kazi na membe ya kumchafuwa lowasa kwa makubaqliano kwamba nape ataachiwa jimbo na membe,ridhiwani mama yake naye wanampotosha baba jk,membe amekuwa akimtumia riz kupeleka majungu kwa baba yake

Membe na Riz kwa sasa hawapo pamoja kabsa familia ya JK wote sasa hawamtaki Membe licha ya kujipendekeza na kushinda kwa Masangoma akiwanga, wao chagua lao ni Kinana, pinda na Lowasa endapo machaguo yao yatadunda wataelekea kwa wasira, huyo Membe mwizi wa pesa za Gadafi hawamtaki kabsa.
 
Membe licha ya kumnunua Nape ana kikundi kikubwa kinachoshinda kwenye mitandao Kazi yao kubwa ni kuwachafua wale wote wenye nia ya kuutaka Urais tu, kila mwenye kutangaza nia anakuwa Adui wa Membe, yupo busy mda mwingi
Akibuni Fitina mbali mbalimbali juu ya Lowasa na wengineo wenye nia ya kuelekea ikulu, yale mapesa ya marehemu Gadafi ambayo aliyafukia kwenye Handaki nyumbani kwake kaamua kuyafukua na Kumpatia Nape, Dialo wa mwanza na wengine Wengi ili wamsaidie kumchafua Lowasa kwa speed kubwa, Membe ana Laana kubwa toka kwa marehemu balozi wa Libya ambaye alimdhulumu mapesa kisha akamuua ili kupoteza ushahidi, Hii laana ndiyo imemfanya Membe akose Mvuto wa kisiasa na pia JK na familia yake wamtose Kwani wanajua kuwa akipewa Nchi atakuwa kama iddy Amini wa Uganda na kupelekwa The Hague .
 
Lowassa asipogombea ccm,wemekwisha.
Hakuna Presidential candidate ccm anayemkaribia Lowassa hata kwa mbali."Quote my words"

Mkuu naamini maneno yako hakika wakimuengua itakula kwao vibaya,hakuna mtu mwenye nyota ya huyo mzeee
 
Kuna hakika gani kama ni masheikh au wachungaji wameenda kwa Lowasa. Tupewe majina ya ha watu na taasisi zao kisha tuwaulize kulikoni
 
anachokosea lowasa ni timing,,angesubiri mda mwafaka na afanye anachofanya sasa angefaulu.[/QUOTE
katika baadhi ya makundi ya What'sapp niliona pendekezo moja la Kiongozi wangu mmoja wa dini ambaye Baadaye niliamua kuwasiliana naye kwa UFAFANUZI.
AMETOA USHAURI UFUATAO KWA VYAMA VYA SIASA
VIWE NA FOMU MAALUM YENYE MASWALI MUHIMU KWA WAGOMBEA WOTE. KILA CHAMA KITENGENEZE MASWALI YAKE.
WANANCHI TANGU MWANZO WAONE UMAKINI WA MASWALI YA KILA CHAMA NA JINSI KILIVYOJIRIDHISHA NA MAJIBU YA WAGOMBEA. Haya ni nje na sera, ilani NA mipango ya CHAMA. ( haya ni yale niliyoweza kuandika wakati wa mawasiliano. Kama nitakuwa nimepunguza natumaini atanielewa.

Mfano wa MASWALI
1. Ni kwa nini unagombea nafasi kubwa hii? Unafuata NINI ikulu ambacho huwezi kukifanya ukiwa nje ya Ikulu? Je ikitokea hatukukuteua kisha akateuliwa mwingine tutakayemuona Ana uwezo wa KAZI HII wewe utafanyaje?

2.Utafanya NINI kuinua Uchumi wa nchi yetu

3, Mahusiano yako na majirani zako yakoje?
4. Tafadhali eleza juu ya uadilifu wako na uaminifu wako kwa maisha ya na mahusiano ya NDOA
5. Je umewahi kuwa na tuhuma zozote za rushwa, udanganyifu, ubadhirifu au kuhojiwa juu ya uadilifu wako KWA mambo ya fedha?
6. Endapo watu wangeulizwa kuhusu mke/ mume wako au watoto unadhani wanasema NINI kukuhusu? Tunaomba uweke sahihi Hapa chini kuruhusu uchunguzi wa kina juu ya Maisha yako.

7. Utafanyaje kuondoa udini, ukabila unaonyemelea taifa letu , Je utafanya NINI kuzuia ubaguzi mwingine wowote KATIKA taifa?
8. TAIFA hili hupoteza mamilioni ya Fedha KWA njia mbalimbali umewahi kufanya NINI kuzuia upotevu wa FEDHA ? Utafanya NINI kubana matumizi ya Serikali ? Utafanya NINI kuhakikisha ufisadi unakoma Tanzania?
9. Ni NINI Tafsiri yako ya ucha Mungu? Je wewe waweza kuitwa mcha Mungu?
10. Utatumia mbinu gani kuhakikisha raslimali za taifa hili hazipotei na zinatumika sawa sawa-
11. TUPE MPANGO WAKO WA MIAKA MITANO
12. Tueleze mambo ambayo unadhani una udhaifu kwayo. ( UDHAIFU WAKO NI NINI?).

13. Una mpango wa KUTOA NINI KWA taifa lako. Una hakika kutoka moyoni mwako hakuna unachotafuta kupata Kutokana NA nafasi hiyo? Kama kipo unachotaka kupata tafadhali eleza.
KULINGANA NA MAONI YAKE HAPO TUTAONEKANA TUNAELEWA THAMANI YA KAZI YA URAIS KWAMBA SIO URAHISI.

Majibu ya wagombea yawekwe wazi kabla ya uteuzi.

 
Nape,wakati wa uchaguzi mdogo kule Igunga,kulitokea mjadala humu JF,uchaguzi mdogo huo ndio ule uliomuweka Kafumu mjengoni.
Mjadala ulikuwa ni wewe kwenda ama kutokwenda Igunga,kumbuka nikiandika na kukuhakikishia kwamba,kamwe usingeenda Igunga kukisaidia chama chako kwa kuwa ndogo kwanza ulikuwa kwenye kasi ya kiwango cha lami kumshambulia Lowasa,nikikwambia wazi hutokanyaga Igunga,ilifikia kipindi nikikuahidi dola mia kama utakanyaga Igunga.pili niliwahi kukuahidi kipindi cha kutaka kumvua gamba EL kufuatia kashfa ya Richmond,nilisema na niliendelea kisema wewe na maccm wenzio hamna ubavu wa kumvua gamba EL,yote hayo yalitimia kama nilivyokuahidi,na hii kutokana na ukweli usiopingika kwamba chama chako ccm ni cha wapiga dili na wala si kwa masilahi ya watanzania,vivyo hivyo leo nakuahidi tena,tunza sana post hii na wengine mnaopenda kudandia mambo ya wenye ccm yao,amini amini nakuambia Nape,wewe na chama chako ccm kamwe hakuna mwenye ubavu wa kulikata jina la EL kwenye kinyang'anyiro cha urais ndani ya ccm hii ya leo,hakika nawaambieni hakuna atakaelikata jina la EL.
NAPE time will tell.
 
Nani alipaswa kumweka Lowassa gerezani na kwa nini anamwacha mwizi anawakisha watu wa Monduli mpaka leo?
Kwa nini anapowakilisha watu wa Mondili anakua Jembe na mchapa kazi lakini anapoombwa kuchukua tu form anakua fisadi na mwizi?

Tuliogundua kuwa hii ni michezo ya wanasiasa tu kusaka madaraka basi tuna chambua pumba na mchele.
Lowasa aligundulika ni mwizi tangu Baba wa taifa yupo hai na mwalimu mwenyewe aliacha wosia kuwa huyu mtu asipewe uongozi wa nchi atauza kila Kitu kwa hiyo tunafuata wosia wa baba wa taifa.
 
Back
Top Bottom