Nape: Lowassa ameanza kufanya kampeni, yuko hatarini kuenguliwa

Nape: Lowassa ameanza kufanya kampeni, yuko hatarini kuenguliwa

Usijifanye kwamba hujui kiswahili.

Kwanza Lowasa hajajitangaza kuwania urais ni woga tu wa wale wasio na sifa na ushawishi kwenye jamii.

''JK alisema '' KAMA waliojitokeza hawafai ''

Neno ''kama'' limetumika kuonyesha kuwa kama wanafaa waacheni.
Hata hivyo wananchi baada ya kuona wengine wanasambaza vitabu nchi nzima,wengine kutumia matamasha ya krismas ,pasaka na wasanii mbalimbali kujinadi kuwa wao ni wasafi na kutumia matamasha hayo kuwakashfu na kuwapaka matope wenzao ;kadhlika wengine wakitumia nyadhfa zao za uwaziri na uwaziri mkuu kujitangaza na kutangaza nia. Wananchi wakaamua kumfuata Lowassa ambaye hajajitangaza bado ili wamshawishi kama alivyoelekeza mwenyekiti wa CCM Taifa.
Kosa liko wapi kama sio unafiki wa Nape na makuwadi wake.
Hivi ulikuwa na sababu za kutumia nguvu zote hizo? Nani amesema Lowassa au yeyote kafanya kosa? By the way, nani amesema suala la kutangaza? Yaani unaamini kujitangaza na kujitokeza ni kitu kimoja? Yaani kabisa unaamini kwamba Lowassa hajajitokeza kuutaka Urais? By the way, ni nani amesema hao waliojitokeza hawafai?
 
Habari wapendwa.

Akihojiwa kupitia kituo cha Radio cha Clouds FM kwenye kipindi cha Power Breakfast juu ya makundi mbalimbali ya kijamii kumtaka Lowasa kutangaza nia yamkugombea nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2015, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Nape Moses Nnauye amesema kuwa kimsingi Lowasa ameonesha na ametangaza nia ya kugombea nafasi hiyo kwa muda mrefu na ndo maana chama kilimwadhibu kwa kuanza kampeni kabla ya wakati wake. Anasema kuwa kinachofanyika kwa sasa ni usanii na ulaghai wa kisiasa wa mwanasiasa huyo ambaye anausaka urais kwa udi na uvumba na kwamba kinachofanyika kwa sasa ni muendelezo wa kampeni za mapema zinazovunja kanuni na misingi ya chama.

Anasema kuwa si kweli kuwa makundi hayo ndiyo yanayomtaka Liwasa agombee bali watu hao wanaandaliwa na gharama zote zinalipwa na Lowasa ikiwa ni pamoja na nauli, malazi, chakula pamoja na fedha zinazotolewa kwa lengo la kugharamia uchukuaji wa fomu. Nape anaongeza kwa kusema kuwa wanazo taarifa kuwa makundi mbalimbali yanaendelea kuandaliwa ambayo yataenda Dodoma siku si nyingi. Anasema kuwa wakiwa Kilimanjaro, wamepata taarifa za baadhi ya watu walioombwa na Team Lowasa kwenda Dodoma. Ameyataka makundi hayo kuwa ni pamoja na Walemavu na Wafanya Biashara ndogo ndogo maarufu kama Wamachinga.

Akitoa ufafanuzi zaidi anasema kuwa nyumbani kwa Lowasa yamewekwa mahema na viti vya kutosha muda mrefu hata kabla ya kundi la kwanza kwenda. Anasema kuwa kama kweli wageni hao hawakutokana na jitihada zake Lowasa, maandalizi hayo ya nini? Kwa nini waitwe waandishi wa habari na pia maandalizi ya chakula cha wageni hao kufanyika hata kabla ya ujio wa wageni hao? Anahoji Nape Nnauye.

Kwa msingi huo, Nape anasema kuwa hatua ambayo amefikia Lowasa haivumiliki na kwamba mwanasiasa huyo amejiondoa mwenyewe kwenye kinyang'anyiro cha urais kwa Tiketi ya CCM labda kama jitihada zake zinalenga kugombea nafasi hiyo kupitia chama kingine ambacho Nape hakukibainisha.

My Take: Naamini kuwa Nape hakukurupuka kusema aliyosema na bila shaka amepata baraka za viongozi wake akiwemo Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ambaye yupo naye sambamba kwenye ziara zake pamoja na Mwenyekiti, Jakaya Kikwete. Lowasa ujumbe ndio huo. Harakati zako ni sawa na mtu anayetwanga maji huku akitaraji kupata unga. Nakuhurumia sana
Lizaboni
Kama taifa na kwa kuheshimu na kuipa hadhi ya juu kabisa kiti cha uraisi kama ofisi kuu nchini, tujiulize na kutafakari ni kwanini EL na washirika wake wanaonekana kutumia kila njia kuingia ikulu kwa NGUVU na propaganda.
 
Last edited by a moderator:
Nape ni nani ndani ya Chama.... Huyu huyu sii ndiyo alimtukana Jakaya 2005? Leo hii yuko wapi?
Urais kwa hakika ni taasisi yenye mamlaka ya juu kabisa ya kiutendaji katika nchi yetu. Kwa mawazo yangu, tuki-assume kwamba CCM watatoa rais (which is POSSIBLE) basi bora awe Lowassa maana anaroho na uwezo wa kuthubutu kuamua na kutenda. Ukweli ni kwamba sote tungependa kuwa na rais asiyekuwa na doa hata kidogo. Naamini tunaweza kumpata lakini kwangu mimi sifa moja tu hiyo haitoshi kutupeleka mbele kimaendeleo hasa kipindi hiki cha usoni ambacho changamoto ya wajomba na mashangazi wa magharibi itakuwa kubwa kuliko wakati wowote nchi yetu imepitia kutokana na hifadhi kubwa ya rasilimali ya gesi na madini. Lowassa anaweza kusimamia maneno yake. Nikumbushe kuwa nimesema CCM wanaweza kutoa rais. Imani yangu ni kubwa pia kuwa UKAWA watapata wabunge wengi kuliko muda wowote katika historia ya nchi hii. Bunge linalojenga hoja kisawasawa haliwezi kuruhusu rais akafanya upuuzi mbele yake. Hata huyo rais akishaona majority ya wabunge ni upinzani, hawezi kufanya upuuzi kama ambavyo angefanya akiwa na wabunge wengi. Ushauri wangu kwa wasomi wenzangu ni kukubali kachumbari hili endapo litatokea maana itakuwa nchi imepiga hatua.
 
maneno yake mbofumbofu na jeuri yake ya kumtukana lowassa hadharani yatamtokea puani oktoba. wewe muache amalizie kwanza hii miezi michache iliyosalia kabla hajarejea nyumbani kwao masasi akalime korosho. hata ukuu wa tarafa atausikia redioni tu.

Teh teh teh mtumbo ule utayeyuka wote ngoja tusubiri tu.
 
Hivi ulikuwa na sababu za kutumia nguvu zote hizo? Nani amesema Lowassa au yeyote kafanya kosa? By the way, nani amesema suala la kutangaza? Yaani unaamini kujitangaza na kujitokeza ni kitu kimoja? Yaani kabisa unaamini kwamba Lowassa hajajitokeza kuutaka Urais? By the way, ni nani amesema hao waliojitokeza hawafai?

Hizo ni Lugha za wanasiasa na zote zina maana ile ile.

Labda mimi na wewe ndio hatujaelewana.
 
Urais kwa hakika ni taasisi yenye mamlaka ya juu kabisa ya kiutendaji katika nchi yetu. Kwa mawazo yangu, tuki-assume kwamba CCM watatoa rais (which is POSSIBLE) basi bora awe Lowassa maana anaroho na uwezo wa kuthubutu kuamua na kutenda. Ukweli ni kwamba sote tungependa kuwa na rais asiyekuwa na doa hata kidogo. Naamini tunaweza kumpata lakini kwangu mimi sifa moja tu hiyo haitoshi kutupeleka mbele kimaendeleo hasa kipindi hiki cha usoni ambacho changamoto ya wajomba na mashangazi wa magharibi itakuwa kubwa kuliko wakati wowote nchi yetu imepitia kutokana na hifadhi kubwa ya rasilimali ya gesi na madini. Lowassa anaweza kusimamia maneno yake. Nikumbushe kuwa nimesema CCM wanaweza kutoa rais. Imani yangu ni kubwa pia kuwa UKAWA watapata wabunge wengi kuliko muda wowote katika historia ya nchi hii. Bunge linalojenga hoja kisawasawa haliwezi kuruhusu rais akafanya upuuzi mbele yake. Hata huyo rais akishaona majority ya wabunge ni upinzani, hawezi kufanya upuuzi kama ambavyo angefanya akiwa na wabunge wengi. Ushauri wangu kwa wasomi wenzangu ni kukubali kachumbari hili endapo litatokea maana itakuwa nchi imepiga hatua.

Kama una hoja vile.... Great
 
Hivi kupata wageni ni vibaya? Huyo Nape huyo kama hana wageni akaw kimya
 
Tunamjua Nape Hapatani na Lowassa tena ni paka na panya nahisi Hawa watu wanajua walichomfanyia Lowassa ndio maana wanakuwa wakali! Kambi ya JK inakufa kabisa sasa, maana kuna kambi pia ya Rais wazamani Mkapa iliyosheheni wachapa kazi akina magufuri akina sheni bado wanapiga jaramba hawajachukua maanuzi bado na Lowassa huyoooo, yupo kwenye Run-way sasa kazi kwenyu CCM tunataka siasa safi za ushindani, kila la heri. yetu macho.
 
Mzee wa Mvi endapo atakalia kiti hivi makonda na Nape sijui wataenda wapi Mzee katengeneza Movie yake ya kushawishiwa na hao anaowajua yy Nape unamkataza na Kauli yake ya juzi kua Kamwambien rais nitaendeleza pale alipoachia kweli siasa sanaa nyie pambaneni tu sie tupo
 
tajiri kwa wizi wa mali ya umma? Lowasa inatakiwa awe gerezani muda huu.

Nani alipaswa kumweka Lowassa gerezani na kwa nini anamwacha mwizi anawakisha watu wa Monduli mpaka leo?
Kwa nini anapowakilisha watu wa Mondili anakua Jembe na mchapa kazi lakini anapoombwa kuchukua tu form anakua fisadi na mwizi?

Tuliogundua kuwa hii ni michezo ya wanasiasa tu kusaka madaraka basi tuna chambua pumba na mchele.
 
Vuteni subira jamani. Hizo siasa za vyombo vya habari (Propaganda) zinajulikana na hazijawahi kuwa na mashiko sana katika uhalisia wa matukio.
Mda utatujuza kitakachojiri hapo baadae. Sentiments zenu zitulizeni kwanza
 
Urais kwa hakika ni taasisi yenye mamlaka ya juu kabisa ya kiutendaji katika nchi yetu. Kwa mawazo yangu, tuki-assume kwamba CCM watatoa rais (which is POSSIBLE) basi bora awe Lowassa maana anaroho na uwezo wa kuthubutu kuamua na kutenda. Ukweli ni kwamba sote tungependa kuwa na rais asiyekuwa na doa hata kidogo. Naamini tunaweza kumpata lakini kwangu mimi sifa moja tu hiyo haitoshi kutupeleka mbele kimaendeleo hasa kipindi hiki cha usoni ambacho changamoto ya wajomba na mashangazi wa magharibi itakuwa kubwa kuliko wakati wowote nchi yetu imepitia kutokana na hifadhi kubwa ya rasilimali ya gesi na madini. Lowassa anaweza kusimamia maneno yake. Nikumbushe kuwa nimesema CCM wanaweza kutoa rais. Imani yangu ni kubwa pia kuwa UKAWA watapata wabunge wengi kuliko muda wowote katika historia ya nchi hii. Bunge linalojenga hoja kisawasawa haliwezi kuruhusu rais akafanya upuuzi mbele yake. Hata huyo rais akishaona majority ya wabunge ni upinzani, hawezi kufanya upuuzi kama ambavyo angefanya akiwa na wabunge wengi. Ushauri wangu kwa wasomi wenzangu ni kukubali kachumbari hili endapo litatokea maana itakuwa nchi imepiga hatua.

Umekuwa Gwajima wakutaka kutuaminisha kile unachokiamini ww.....mm nko tofauti na fikra zako
 
Ninyi wapambe wa Mh.Lowassa mnapoanza kujenga hoja za kuitisha CCM haziwezi kuwasaidia katika harakati zenu.

CCM haikujengwa katika msingi wa kutikisika achilia mbali kutikiswa na mwanachama.

CCM haiopopi kuanguka katika chaguzi, ndiyo maana inaingia katika chaguzi zote nchini.

CCM haiwezi kuwekwa rehani na wanachama achilia mbali mwanachama.

CCM na KANU wapi na wapi achilia mbali siasa za Kenya na Tanzania.

Fanyeni siasa safi ndani ya chama na siyo siasa za kuitisha CCM.

Mbona Mkapa alitishwa na kundi la Mtandao 2005 na akasalimu amri? Muulize Mzee Mangula lile file la maadili la Mwenyekiti wa sasa lililokuwa lisomwe ili kumzuia asipitishwe liliishia wapi kama CCM haikuogopa kuanguka? Au unadhani tumesahau?
 
Back
Top Bottom