Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,857
- 3,105
Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema kitendo cha mgombea mmoja anayepokea makundi ya watu ili wamshawishi kupiga kura huko Dodoma ni kuanza kampeni na yuko hatarini kuenguliwa.
Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa ndiye anayepokea makundi ya watu wakiwemo masheikh, maaskofu na wanafunzi wakimshawishi kugombea.
Akizungumza na radio VOA, Nape alisema: "Labda niweke vizuri hili, mtu yoyote anayekiuka kanuni hatapitishwa labda kamaa anakwenda kugombea kwa chama kingine.
"Kinachofanyika Dodoma cha watu kuchukuliwa na magari huku wengine wakiwa hawajui, halafu wakifika wanakuta viti vimeshapangwa na vyakula;halafu eti wanamshawishi kugombea, ni kukiuka kanuni na anaweza kuondolewa," alisema Nape.
Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa ndiye anayepokea makundi ya watu wakiwemo masheikh, maaskofu na wanafunzi wakimshawishi kugombea.
Akizungumza na radio VOA, Nape alisema: "Labda niweke vizuri hili, mtu yoyote anayekiuka kanuni hatapitishwa labda kamaa anakwenda kugombea kwa chama kingine.
"Kinachofanyika Dodoma cha watu kuchukuliwa na magari huku wengine wakiwa hawajui, halafu wakifika wanakuta viti vimeshapangwa na vyakula;halafu eti wanamshawishi kugombea, ni kukiuka kanuni na anaweza kuondolewa," alisema Nape.
Habari wapendwa.
Akihojiwa kupitia kituo cha Radio cha Clouds FM kwenye kipindi cha Power Breakfast juu ya makundi mbalimbali ya kijamii kumtaka Lowasa kutangaza nia yamkugombea nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2015, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Nape Moses Nnauye amesema kuwa kimsingi Lowasa ameonesha na ametangaza nia ya kugombea nafasi hiyo kwa muda mrefu na ndo maana chama kilimwadhibu kwa kuanza kampeni kabla ya wakati wake. Anasema kuwa kinachofanyika kwa sasa ni usanii na ulaghai wa kisiasa wa mwanasiasa huyo ambaye anausaka urais kwa udi na uvumba na kwamba kinachofanyika kwa sasa ni muendelezo wa kampeni za mapema zinazovunja kanuni na misingi ya chama.
Anasema kuwa si kweli kuwa makundi hayo ndiyo yanayomtaka Liwasa agombee bali watu hao wanaandaliwa na gharama zote zinalipwa na Lowasa ikiwa ni pamoja na nauli, malazi, chakula pamoja na fedha zinazotolewa kwa lengo la kugharamia uchukuaji wa fomu. Nape anaongeza kwa kusema kuwa wanazo taarifa kuwa makundi mbalimbali yanaendelea kuandaliwa ambayo yataenda Dodoma siku si nyingi. Anasema kuwa wakiwa Kilimanjaro, wamepata taarifa za baadhi ya watu walioombwa na Team Lowasa kwenda Dodoma. Ameyataka makundi hayo kuwa ni pamoja na Walemavu na Wafanya Biashara ndogo ndogo maarufu kama Wamachinga.
Akitoa ufafanuzi zaidi anasema kuwa nyumbani kwa Lowasa yamewekwa mahema na viti vya kutosha muda mrefu hata kabla ya kundi la kwanza kwenda. Anasema kuwa kama kweli wageni hao hawakutokana na jitihada zake Lowasa, maandalizi hayo ya nini? Kwa nini waitwe waandishi wa habari na pia maandalizi ya chakula cha wageni hao kufanyika hata kabla ya ujio wa wageni hao? Anahoji Nape Nnauye.
Kwa msingi huo, Nape anasema kuwa hatua ambayo amefikia Lowasa haivumiliki na kwamba mwanasiasa huyo amejiondoa mwenyewe kwenye kinyang'anyiro cha urais kwa Tiketi ya CCM labda kama jitihada zake zinalenga kugombea nafasi hiyo kupitia chama kingine ambacho Nape hakukibainisha.
My Take: Naamini kuwa Nape hakukurupuka kusema aliyosema na bila shaka amepata baraka za viongozi wake akiwemo Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ambaye yupo naye sambamba kwenye ziara zake pamoja na Mwenyekiti, Jakaya Kikwete. Lowasa ujumbe ndio huo. Harakati zako ni sawa na mtu anayetwanga maji huku akitaraji kupata unga. Nakuhurumia sana