Nape: Lowassa ameanza kufanya kampeni, yuko hatarini kuenguliwa

Tusubiri mwisho wa sinema wakati wa uteuzi. Nina uhakika ccm hakuna mwenye ubavu wa kumnyooshea kidole Lowassa. Maamuzi magumu kama hayo yanawezekana kwa CDM tu.
 
NAPE fahamu kuwa CCM ilishajiengua yenyewe kwenye kinyanganyiro cha urais, sio EL tu ni CHAMA KIZIMA hakina rais
 
Hali isiyo ya kawaida amefikia kuudanganya summa kwamba yeye yuko mzima wa afya kwa kumuarika mpiga ampige picha akifanya mazoezi kitu ambacho kiliandaliwa huku wananchi wakijua kabisa kuwa hayuko sawa kiafya....hahahahaaa jamaa kapania kiukweli
 
lowa jembe wananchi tumesha mkubali nape ninani?
 
napekapewa kazi na membe ya kumchafuwa lowasa kwa makubaqliano kwamba nape ataachiwa jimbo na membe,ridhiwani mama yake naye wanampotosha baba jk,membe amekuwa akimtumia riz kupeleka majungu kwa baba yake
 
Habari wapendwa.

Akihojiwa kupitia kituo cha Radio cha Clouds FM kwenye kipindi cha Power Breakfast juu ya makundi mbalimbali ya kijamii kumtaka Lowasa kutangaza nia yamkugombea nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2015, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Nape Moses Nnauye amesema kuwa kimsingi Lowasa ameonesha na ametangaza nia ya kugombea nafasi hiyo kwa muda mrefu na ndo maana chama kilimwadhibu kwa kuanza kampeni kabla ya wakati wake. Anasema kuwa kinachofanyika kwa sasa ni usanii na ulaghai wa kisiasa wa mwanasiasa huyo ambaye anausaka urais kwa udi na uvumba na kwamba kinachofanyika kwa sasa ni muendelezo wa kampeni za mapema zinazovunja kanuni na misingi ya chama.

Anasema kuwa si kweli kuwa makundi hayo ndiyo yanayomtaka Liwasa agombee bali watu hao wanaandaliwa na gharama zote zinalipwa na Lowasa ikiwa ni pamoja na nauli, malazi, chakula pamoja na fedha zinazotolewa kwa lengo la kugharamia uchukuaji wa fomu. Nape anaongeza kwa kusema kuwa wanazo taarifa kuwa makundi mbalimbali yanaendelea kuandaliwa ambayo yataenda Dodoma siku si nyingi. Anasema kuwa wakiwa Kilimanjaro, wamepata taarifa za baadhi ya watu walioombwa na Team Lowasa kwenda Dodoma. Ameyataka makundi hayo kuwa ni pamoja na Walemavu na Wafanya Biashara ndogo ndogo maarufu kama Wamachinga.

Akitoa ufafanuzi zaidi anasema kuwa nyumbani kwa Lowasa yamewekwa mahema na viti vya kutosha muda mrefu hata kabla ya kundi la kwanza kwenda. Anasema kuwa kama kweli wageni hao hawakutokana na jitihada zake Lowasa, maandalizi hayo ya nini? Kwa nini waitwe waandishi wa habari na pia maandalizi ya chakula cha wageni hao kufanyika hata kabla ya ujio wa wageni hao? Anahoji Nape Nnauye.

Kwa msingi huo, Nape anasema kuwa hatua ambayo amefikia Lowasa haivumiliki na kwamba mwanasiasa huyo amejiondoa mwenyewe kwenye kinyang'anyiro cha urais kwa Tiketi ya CCM labda kama jitihada zake zinalenga kugombea nafasi hiyo kupitia chama kingine ambacho Nape hakukibainisha.

My Take: Naamini kuwa Nape hakukurupuka kusema aliyosema na bila shaka amepata baraka za viongozi wake akiwemo Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ambaye yupo naye sambamba kwenye ziara zake pamoja na Mwenyekiti, Jakaya Kikwete. Lowasa ujumbe ndio huo. Harakati zako ni sawa na mtu anayetwanga maji huku akitaraji kupata unga. Nakuhurumia sana

Lowassa anaudharau uongozi mzima wa ccm hivyo awahi kujitoa maana huko mbele ni maumivu makali.
 
Kwa ccm hakuna wa kumzuia lowasa kugombea urais wanamuogopa sana huyu fisad na wamezungukaga nae sanaa mala vua gambaa mgonjwaa nk mwakahuu hatoki mtu wataanza wao
 
Lowasa atakuja kulia kama mwanake mjane aliyefiwa na mume anachofanya ni uvunjifu wa kanuni.

Huo siyo mfano mzuri! Mwanamke ndo analia sana kuliko mwananume?

Hata hivyo CCM hawana kanuni za kudumu. Kila mwaka wanatunga mpya zinazoendana na upepo.
 
Habari wapendwa.

Akihojiwa kupitia kituo cha Radio cha Clouds FM kwenye kipindi cha Power Breakfast juu ya makundi mbalimbali ya kijamii kumtaka Lowasa kutangaza nia yamkugombea nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2015, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Nape Moses Nnauye amesema kuwa kimsingi Lowasa ameonesha na ametangaza nia ya kugombea nafasi hiyo kwa muda mrefu na ndo maana chama kilimwadhibu kwa kuanza kampeni kabla ya wakati wake. Anasema kuwa kinachofanyika kwa sasa ni usanii na ulaghai wa kisiasa wa mwanasiasa huyo ambaye anausaka urais kwa udi na uvumba na kwamba kinachofanyika kwa sasa ni muendelezo wa kampeni za mapema zinazovunja kanuni na misingi ya chama.

Anasema kuwa si kweli kuwa makundi hayo ndiyo yanayomtaka Liwasa agombee bali watu hao wanaandaliwa na gharama zote zinalipwa na Lowasa ikiwa ni pamoja na nauli, malazi, chakula pamoja na fedha zinazotolewa kwa lengo la kugharamia uchukuaji wa fomu. Nape anaongeza kwa kusema kuwa wanazo taarifa kuwa makundi mbalimbali yanaendelea kuandaliwa ambayo yataenda Dodoma siku si nyingi. Anasema kuwa wakiwa Kilimanjaro, wamepata taarifa za baadhi ya watu walioombwa na Team Lowasa kwenda Dodoma. Ameyataka makundi hayo kuwa ni pamoja na Walemavu na Wafanya Biashara ndogo ndogo maarufu kama Wamachinga.

Akitoa ufafanuzi zaidi anasema kuwa nyumbani kwa Lowasa yamewekwa mahema na viti vya kutosha muda mrefu hata kabla ya kundi la kwanza kwenda. Anasema kuwa kama kweli wageni hao hawakutokana na jitihada zake Lowasa, maandalizi hayo ya nini? Kwa nini waitwe waandishi wa habari na pia maandalizi ya chakula cha wageni hao kufanyika hata kabla ya ujio wa wageni hao? Anahoji Nape Nnauye.

Kwa msingi huo, Nape anasema kuwa hatua ambayo amefikia Lowasa haivumiliki na kwamba mwanasiasa huyo amejiondoa mwenyewe kwenye kinyang'anyiro cha urais kwa Tiketi ya CCM labda kama jitihada zake zinalenga kugombea nafasi hiyo kupitia chama kingine ambacho Nape hakukibainisha.

My Take: Naamini kuwa Nape hakukurupuka kusema aliyosema na bila shaka amepata baraka za viongozi wake akiwemo Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ambaye yupo naye sambamba kwenye ziara zake pamoja na Mwenyekiti, Jakaya Kikwete. Lowasa ujumbe ndio huo. Harakati zako ni sawa na mtu anayetwanga maji huku akitaraji kupata unga. Nakuhurumia sana
ocampo four na laki si pesa mgombea wenu hatakiwi na viongozi wa chama
 
Last edited by a moderator:
Hali isiyo ya kawaida amefikia kuudanganya summa kwamba yeye yuko mzima wa afya kwa kumuarika mpiga ampige picha akifanya mazoezi kitu ambacho kiliandaliwa huku wananchi wakijua kabisa kuwa hayuko sawa kiafya....hahahahaaa jamaa kapania kiukweli

hivi mnakumbuka jk wakati anagombea ccm nape alisema jk ana ukimwi?na jk mpaka leo anadunda,ndicho hicho hicho kinachotokea kwa lowassa,jiandaeni kisaikolojia lowaasa ndiye rais ajaye
 
kwa kundi kubwa la watu wakiwa wanakuja kwako lazima watakutaarifu kwanza kabla hawajafika.hawawez kuja bila kuwasiliana nawe
 
  • Thanks
Reactions: Bob
CCM wakimteua mtu mwenye tamaa na mlafi wa aina hii itakuwa ni aibu sana. Bora wamfukeze ...ngoja tuone kama CCM wana guts kama waliyokuwanayo CDM kwa Zitto!

Hivi nikikuulizia ni kosa gani Lowasa mpaka afukuzwe ccm unaweza kujibu ni kosa gani?

Pili, Kuna kosa gani watu kwenda kumuomba Lowasa agombee uraisi? Si wale ni watu wazima na wana akili? sasa hizo porojo ni za nini?

Tatu, Mh.Raisi alivyosema nendeni mkawashawishi wale mnaoona wanafaa kuwa wagombea uraisi kwahiyo na yeye alikosea? Tuacheni kufikilia kidogo Ebu twende next miles tuone huyu Nnape power ya kwenda against na Mwenyekiti wa chama anaitoa wapi?

NNE, kuombwa kutangaza nia siyo kuanza kampeini kama nape anavyowaaminisha watu, kampeni ziko wapi pale? Hakuna kampeni yoyote pale, wale waliochapisha vitabu wakasambaza nchi nzima hatukusikia malalamiko, hizi double standard zinatoka wapi?

Tano, wanasema watu wameandaliwa chakula na Mahema, kwani wale wanaokwenda kumshawishi so lazima watoe taarifa kwanza? mbona kuna uoga mwingi mnatuletea??? Lowasa mwacheni kama mungu amempangia kwenda ikulu atatenda tu....

Mungu Mbariki Edward Ngoyayi Lowasa.....
 
Back
Top Bottom