Nape: Lowassa ameanza kufanya kampeni, yuko hatarini kuenguliwa

Nape: Lowassa ameanza kufanya kampeni, yuko hatarini kuenguliwa

Mwalimu nyerere alisema huyu lowasa ni Mwizi asipewe nchi.tunafuata wosia wa baba wa taifa.

Angekua Mungu kasema tungemwelewa maana mabilioni yaliibwa na utawala wa mkapa na alikua chaguo la mwalimu Tanzania ndo nchi pekee duniani inaongozwa na mawazo ya wafu
 
Eti Nyerere alisema,who is Nyerere! Alitupatia benjamini na EPA na Radar na kila uchafu ulishamiri Nyerere sio Mungu kutuchagulia kiongozi ndo maana mmelaaniwa kama nchi kumwacha baba wa kweli wa mbingu nakumwita nyerere baba wa taifa
 
February 22, 2015 ... baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka wanachama kuwashawishi watu wenye sifa wajitokeze kugombea.

Hiyo ni kauli ya Rais Kikwete mapema mwaka huu.sasa wale wanaomiminika kwa Lowassa si wanaitikia wito wa mwenyekiti wao wa chama? labda mimi sikumwelewa rais.
 
Angekua Mungu kasema tungemwelewa maana mabilioni yaliibwa na utawala wa mkapa na alikua chaguo la mwalimu Tanzania ndo nchi pekee duniani inaongozwa na mawazo ya wafu

EPA, ubinafusishaji wa Hatari na mbaya, na uuzaji wa nyumba za Serikali ni moja ya mambo mabaya ya Mkapa ambaye alikuwa Chaguo la Nyerere, hata Fitna juu ya Lowasa zilipandikizwa kwa Nyerere na wabaya wake kipindi kile alikuwa na Ugonvi na mengi wakaamua kumuundia Zengwe kwa Nyerere, lakini baadae Nyerere aligungua kuwa zilikuwa ni Fitina.
 
february 22, 2015 ... Baada ya rais jakaya kikwete kuwataka wanachama kuwashawishi watu wenye sifa wajitokeze kugombea.

hiyo ni kauli ya rais kikwete mapema mwaka huu.sasa wale wanaomiminika kwa lowassa si wanaitikia wito wa mwenyekiti wao wa chama? Labda mimi sikumwelewa rais.

hongera mkuu,nimekusoma
 
Hao walioandika majina yao kwenye mawe na madaraja Dar mpaka Mza mbona hatusikii wakipigwa biti.

Mamvi atawatagisha this time aisee ni diet tosha kwa wapinzani wake.

Nimeona jina la Mwigulu kwenye Daraja flani Maeneo ya DAWASA.
 
Aliyeiba si huyo lowasa.mwizi mkubwa.
m

Lowasa ndiye aliuza nyumba za serkali? Ndiye aliua viwanda kwa ubinafusishaji? Ndiye alihamisha mapesa kwenda A/C Nje ya Nchi? Ndiye aliuza Migodi kwa wageni?
 
Mbona kampeni kazianza muda mrefu na kuna vijana wake wanafanya vikao kila mwezi dodoma kwa pesa zake.
 
Kwaiyo watz hawana ruhusa ya kwenda kumuomba mtu wanayehisi anafaa kugombea uraisi? Au wakienda kumuomba hawaruhusiwi kumpa taarifa kabla ili ajiandae kuwapokea mf. viti. Au ukiwa mgombea ukipata wageni nyumbani kwako utawaambia wakatafute sehemu ya kula maana ww ni mgombea? Wadau wekeni hapa hicho kifungu cha sheria ya ccm tukijadili.





Haya yote yanaaeleweka vizuri kabisa.Ni uchovu tu wa wanasiasa.

Nape ni CCJ.
Livingstone Lusinde ni ni Chadema .
J.Makamba amebebwa kwa nguvu ya baba yake.
Samwel sita ni CCJ
Benard Membe ni CCJ
Makonda ni CCM madaraka.Bila madaraka atahama na kujiunga na ACT ili apate angalau udiwani.
Mwakyembe ni CCJ
Wasira ni NCCR Mageuzi.
Magufuli ni CCM asiye na histori ndefu ya kukitumikia chama katika shida na raha.
Sumaye ni CCM madaraka.Mana alishasema akienguliwa atatafuta chama kingine.
Hawa wote wanacheza ngoma na nyimbo za Chadema.
Tumeona Nape na hilo Kundi lake wakifurahia kifo cha marehemu capt Komba huku wakisahau mazuri yote aliyoyafanya kukijenga chama cha mapinduzi katika uhai wake wote. Hawa ndio watu wanaosema wanakipigania chama.

Kinana ni CCM halisi ndio maana anajua mbinu za kukijenga chama.

Lowassa ni kati ya makada wa kweli wa CCM waliobakia. Kumuengua Lowassa kwa sababu ya kusikiliza kelele za wapita njia litakua ni jambo la kipuuzi na lisilokubalika.

Eti wanasema kwa nini watu wanakuja na kukuta viti vimepangwa na chakula.Ni akili za ajabu kabisa. Kwa ulimwengu wa sasa hivi wageni waje bila kutoa taarifa.
Hata kwa mila zetu za kiafrika mtu akienda kuposa anatoa taarifa kwa wakwe ili wajiandae kupokea ujumbe unaoletwa wa posa.Na usipotoa taarifa basi linakua ni jambo lisilokubalika.

Simu na mitandao iko kila mahali halafu mtu aende kwa mtu bila taarifa.
Ndio maana viongozi wa dini kwa muda mrefu wamepima wakagundua kuwa Lowassa ana hekima kuliko hawa waruka njia ,Nape na kundi lake.Kwani hata hoja zao za kumshambulia Lowassa ni za kijinga na chuki tu.
Eti watu wanazolewa bila kujua kinachoendelea halafu wanapelekwa kwa Lowasa kupewa hela.Hivi kweli inaingia akilini Msomi wa Chuo kikuu azolewe bila kujua anakoenda?

Hivi kweli unaweza ukamzoa mchungaji au shehe ukampeleka asikokujua na akakubali kwenda.
Viongozi wa dini siku zote wanapenda viongozi wasikivu.Na wamegundua kuwa Lowassa hana makuu.

Nape muda Mrefu amekua akionekana dhahiri sio kutumia nafasi aliyo nayo kuhakikisha kuwa anatumia Muda mwingi kupambana na Lowasa ili alete Mtu wake anayemtaka.

Mnafiki na Joka la Mdimu siku zote hawana jema.
Ingetokea wale wachungaji ,mashehe na wanafunzi wa vyuo wakaenda kimya kimya kwa Lowassa bila taarifa na kufika bila hata mashahidi ikiwemo waandishi wa habari basi leo hii Lowasa angekua ameshaitwa kwenye kamati ya maadili na kuhojiwa kuwa anafanya kampeni na vikao vya siri.Ingekua ni ishu kubwa kweli kweli.
Hii ndio tabia ya wanafiki walovamia ndani ya CCM na sasa wanataka kuwaengua makada wa komavu wa chama na serikali ili wapitishe wanachama wenzao wa CCJ!!!
 
Si kweli CCM ina wagombea wengi wazuri kuliko Lowassa ambaye ni aina ya kiongozi anayependa kutumia ukwasi wake kujinufaisha kisiasa wakati hana uwezo wa kuongoza.

Hafai kwa misingi ipi?? na anaefaa ni nani na kwa misingi ipi??
 
Ki ukweli hata mimi nashindwa kuelewa, wagombea ambao wako ccm ni wengi mno ambao wamesimamishwa na wananguvu ya kumudu kufuturisha kipindi hiki cha kwaresma kama bwana edo anavyofanya ila kutokana na kanuni za chama, wameamaua kutulia. Mimi nashindwa kuelewa kitu gani kinamsumbua huyu mzee, nadhani atulie tu

wananchi ndio wanamtaka...unataka awazuie? huna hoja.
 
Hoja yako haiswii, coz' kauli ya JK ni hii hapa:
"Nyerere alisema bila CCM imara nchi itayumba, viongozi tusikubali tuwe wa kwanza kukiuka wosia huu, laana yake itakuwa kubwa kwa Taifa na nchi itayumba, watu wazuri CCM wapo na kama walioanza kujitokeza sasa hawafai, tuwashawishi wajitokeze wengine wakachukue fomu, hata sisi tulishawishiwa japo hatukuwa na mpango wa kuwania urais,
Lowassa anadondokea hapo kwenye RED (whether anafaa au hafai)... yeye tayari alishajitokeza tangu zama hizo na kauli ya kuwashawishi ni kwa ajili ya wale ambao hawajajitokeza!
 
Kilitokana na Membe ili afiche Ushahidi juu ya mapesa ya marehemu Gadafi ambayo walikuwa wamepora pamoja na Balozi kwa nia ya kugawana baadae, lakini Membe akaingia Tamaa akaamua kumteketeza kininja kisha wakazuga kuwa kajiua Mwenyewe, Laana hiyo Ndiyo imepelekea hata JK na familia yake kumtosa na kuhamia kwa Pinda au Kinana na ikishindikana watakaa kwa Lowasa tu hakuna jinsi.

Last week fest ledi alikua Lindi niliona picha zake zikigaiwa kwa wabachi kwa chini ilikua ya Joka la Mdimu
 
Upepo wa kisiasa umeanza kumwendea vibaya Mh Lowassa hasa baada ya makundi mbalimbali kwenda kumshawishi agombee urais. Baadhi ya viongozi wa chama wanasema ameanza kampeni kabla ya kingenga kupulizwa. Je, ikitokea jina lake likaenguliwa na vikao vya chama na ilhali "anakubalika kwa wananchi", ni kitu gani kinaweza kutokea kwake binafsi na kwa CCM?
 
Mwenyekiti wa CDM nasikia kahongwa na Lowassa kitita cha Tshs. 5 Bilioni ili wasifukunyue mafaili ya lowassa tangu alipokuwa AICC, MAJI mpaka RICHMOND...! Ndo maana wapo kimya!

UKAWA wapo kimya kwa kuwa wanaujua udhaifu wa EL. Wanaomba miCCM imteue EL wampige makonzi kwenye uchaguzi.
 
Back
Top Bottom