Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema kitendo cha mgombea mmoja anayepokea makundi ya watu ili wamshawishi kupiga kura huko Dodoma ni kuanza kampeni na yuko hatarini kuenguliwa.
Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassandiye anayeppkea makundi ya watu wakiwemo masheikh, maaskofu na wanafunzi wakimshawishi kugombea.
Akizungumza na radio VOA, Nape alisema: "Labda niweke vizuri hili, mtu yoyote anayekiuka kanuni hatapitishwa labda kamaa anakwenda kugombea kwa chama kingine.
"Kinavhofanyika Dodoma cha watu kuchukuliwa na magari huku wengine wakiwa hawajui, halafu wakifika wanakuta viti vimeshapangwa na vyakula;halafu eti wanamshawishi kugombea, ni kukiuka kanuni na anawezakuondolewa," alisema Nape.