Nape: Dhambi ya ubaguzi inaimaliza CHADEMA!

Nape: Dhambi ya ubaguzi inaimaliza CHADEMA!

KIla siku nawaza sana ni kwa nini chadema ina vijana smart sanaa kuliko ccm.... akiongea mnyika au lissu au lema au zitto inakubidi ukae vizuri utafakarii.. hawa wengne (ccm) kila wakijaribu kuongea ni pumbaa.. sisiemu haina jembe ata mmoja wa kushindana na makamanda wa chadema... sijui inatokana na nini? Je ni kweli ccm imejaa mabogus? Je ni tamaa zinawasukuma wakina nape????
 
Hizi elfu 20 mnazopewa vijana wa magamba kwa kazi moja ya kuleta upuuzi humu kila kukicha zitawafikisha pabaya,mmeacha ndugu zenu wanateseka kijijini kwa sababu ya hii serikali ya chama mnachoshabikia humu,mnategemea kufanya kazi gani baada ya 2015? Hamtakua na familia? Au mnategemea maisha yenu yataishia kupanga foleni Lumumba?
cna cha kuongeza
 
Mipasho hii sasa ni sera rasmi ya ccm, watu wamechoka na uhuni huu wa ccm. bahati mbaya ccm hawasomi nyakati
 
Kwani nape ni nani ktk nchi hii mimi namfananisha na mtu ambaye hajui lakini kwa bahati mbaya hajitambui kama hajui.Udini na ukanda unaosemwa mbona haupo hizi propaganda utaacha lini wewe nnauye uliyepewa cheo hicho kwa fadhila ya baba ako?.
 
Mipasho hii sasa ni sera rasmi ya ccm, watu wamechoka na uhuni huu wa ccm. bahati mbaya ccm hawasomi nyakati
Kwa taarifa nilizosoma hapa JF muda kidogo ni kwamba Mwanza watu wamewapiga mawe, wao wanadai ni wafuasi wa CHADEMA!!! Sijui watakwenda wapi sasa, MTWARA PIA HAWATAKIWI wajaribu waone, watu wamechoka na uongo wa CCM, kazi yao ya wizi na uongo imefikia mwisho!!!!

 
cdm mmekwisha nawaambia . na mrema aje na majibu jins mlivyotumia mil 500 za m4c au ndio mlikopesha baba junior

Mchange nenda CHAUMA au nccr ,utabaki hapo na masalia wako hadi Kristo anarejea, wewe jiondoe kwenye orodha ya wanasiasa labda ukapate ubunge ukiwa gerezani lakini uraiani ni BIG NO.
 
Kuna haja gani ya kujadili alichoandika huyu mchumia tumbo wa gambaz.
Katibu wa NEC-CCM Nape NNauye ambaye vile vile ni Mkuu wa Itikadi na Uenezi, ametoboa siri ya kifo cha CHADEMA kuwa kitatokana na ubaguzi kati ya wananachama wake.

Ingalau magazeti mawili yamemnukuu akikomelea msumari katika tofauti zinazojitokeza hivi sasa ndani ya CHADEMA.Gazeti la Majira (21/1/2013) lenyewe limedai kwamba :

"Nape afichua siri za kifo cha CHADEMA, na kudai-hakuna dawa ya kutumia lazima kife-ameendelea kudai ni laana ya Nyerere, wasitafute mchawi"

Page 4 ya gazeti hili linaendelea

"Alisema(NAPE) ubaguzi ulioota mizizi kwa muda mrefundio unakimalizachama hichoambao umelelewa na waasisi pamoja na viongozi wa kitaifa hivyo kina haki ya kufa kutokana na dhambi hiyo"

Aliendelea...

"Hamuwezi kuwa na chama ambacho kinaendekeza ubaguzi..ili kiongozi wake adumu na kuheshimika lazima atoke ukanda fulani au ukoo fulani vinginevyo anasukiwa mizengwe na kutimiliwa. Walianza na marehemu Wangwe.... hivi sasa wameanza kumuandama Zitto Kabwe(Naibu Katibu Mkuu CHADEMA) na wanaoitwa vijana wake, nasikia wiki ijayo wamejipanga kumfukuza Shibuda(Bunge wa Maswa)"

Nnauye akamalizia kwa msumari mzito

"CHADEMA ni chama kidogo kinabaguana kiasi hicho, wakipewa dhamana ya kutawala nchi hali itakuwa mbaya zaidi"


My take

Wana CHADEMA huo ni msumari unaoweza kuwa mkuki moyoni.
Jisahihisheni kabla hamjafa kweli.
(NB wale wenye matusi chukueni likizo)
 
Kuna wakati na wewe unakerwa na CCM hii hii unayoishabikia

Ee bwana sisi huko sijui tuna tatizo gani, hata waziri mkuu hatembelei huko.
JK angefika tu na kutoa ahadi kama anavyotoa kwingine tungefarijika sana.

Itungi Port inaendelea kuzama ndani ya ziwa Nyasa na hakuna juhudi zozote za kuiokoa.

Kugomea rasilmali zetu Mbeya?Rungwe/Kyela hilo litakuja tu baada ya kuona sakata la gesi ya Mtwara linaendaje.
Watu wanasahau kuwa sisi tumekuwa na gesi ya carbon dioxide kule Kyejo kwa miaka mingi ikipelekwa DSM.
Wakifanikiwa Mtwara kuzuia yao na sisi tutafuata.


View attachment 79123
Karavari iliyoharibiwa na mvua za karibuni-Interchick


Magufuli ni mmoja wa Mawaziri makini kwa kufuatilia kazi zake na kuzisifia kwa takwimu hadi nukta ya mwisho.

Ili afanye kazi yake vizuri ni vyema akatonywa na wananchi madudu yanayoonekana wazi wakati vyombo chini yake vinasua sua kufanya hivyo.

Katika barabara ya Bagamoyo(Mwenge -Wazo) madudu ya wazi yanajitokeza hata kabla barabara haijamalizika.

Mvua za hivi karibuni na vile vile mwaka jana kwenye mwezi wa kumi na moja zimetoa kielelezo cha uhafifu mkubwa wa ujenzi wa barabara hii inyotekelezwa na kampuni makini ya KONOIKE.

Nionavyo mimi matatizo makubwa ni katika udhibiti wa maji ya mvua na miundo mbinu yake.
Matatizo hata yapo sehemu kuu tatu:
  • pale Samaki wabichi/Goig-ambapo hakuna miundo mbinu yoyote kudhiti na kupokea mto unaotoka sehemu za juu kule Goig.
  • Interchick-mto Ndumbwi bado unatamba, kile kimfereji cha mawe ni usanii tu!
  • Africana/Salasala junction-maji yanayotoka juu Salasala haina miundombinu inayoeleweka

Kuokana na matatizo hayo barabara hii katika mvua za juzi ilikuwa balaa!
Pale Interchik barabara nzima ingebomolewa kama mvua zingeendelea.

Mimi simlaumu mkandarasi, bali wasanifu wa barabara hii na TANROADS wanopaswa kusimamia na kupitisha michoro ya ujenzi.

Kwa hakika kama wakiondoka hao wakandarasi na kukabidhi bila kufanyia marekebisho usanifu wa miundombinu ya maji ya mvua, basi barabara hii haitodumu hata miaka miwili.

Kwa kweli tuache siasa za ushabiki.
CCM Mbeya is a lost case.
Chama kimepigwa vita sana kwa msaada wa makada wenyewe toka makao makuu.
CHADEMA wanajiokotea wafuasi.

Umeeleza ukweli.
Ila tatizo hili si la unafiki ni RUSHWA.
Wachina wanatoa rushwa sana kila wanapoenda.

TANROADS iko hoi kwa vijisenti wanavyopewa na hawasimamii hao wachina.
 
ajiulize vzur huyu bwn ne.pi,ni kwa nini wananchi wajipange barabarani ni kuwazomea yeye na magamb.a wenziwe??
tutaizika sisiem kabla ya 2015 .

CDM hamutaiweza CCM tena mtajinyonga wengi sana 2015 maana hamutaamini macho yenu pindi tutakavyoshinda kwa kishindo.....Nape na Mwigulu ni kiboko yenu mbona sisi Mnyika hatumnangi maana hawezi kazi yake ya uenezi? Mumeamua kumchagua wenyewe Mnyika na kumrundikia vyeo kibao kumbe munamkimoa huyu ndugu yangu. MNYIKA take my word CDM hawakupendi majibu yake utayaona 2015
 
Atuambie kwa nini jina lake halipo hapa

BrigGen+NnauyeKisw.jpg
 
Katibu wa NEC-CCM Nape NNauye ambaye vile vile ni Mkuu wa Itikadi na Uenezi, ametoboa siri ya kifo cha CHADEMA kuwa kitatokana na ubaguzi kati ya wananachama wake.

Ingalau magazeti mawili yamemnukuu akikomelea msumari katika tofauti zinazojitokeza hivi sasa ndani ya CHADEMA.Gazeti la Majira (21/1/2013) lenyewe limedai kwamba :

"Nape afichua siri za kifo cha CHADEMA, na kudai-hakuna dawa ya kutumia lazima kife-ameendelea kudai ni laana ya Nyerere, wasitafute mchawi"

Page 4 ya gazeti hili linaendelea

"Alisema(NAPE) ubaguzi ulioota mizizi kwa muda mrefundio unakimalizachama hichoambao umelelewa na waasisi pamoja na viongozi wa kitaifa hivyo kina haki ya kufa kutokana na dhambi hiyo"

Aliendelea...

"Hamuwezi kuwa na chama ambacho kinaendekeza ubaguzi..ili kiongozi wake adumu na kuheshimika lazima atoke ukanda fulani au ukoo fulani vinginevyo anasukiwa mizengwe na kutimiliwa. Walianza na marehemu Wangwe.... hivi sasa wameanza kumuandama Zitto Kabwe(Naibu Katibu Mkuu CHADEMA) na wanaoitwa vijana wake, nasikia wiki ijayo wamejipanga kumfukuza Shibuda(Bunge wa Maswa)"

Nnauye akamalizia kwa msumari mzito

"CHADEMA ni chama kidogo kinabaguana kiasi hicho, wakipewa dhamana ya kutawala nchi hali itakuwa mbaya zaidi"


My take

Wana CHADEMA huo ni msumari unaoweza kuwa mkuki moyoni.
Jisahihisheni kabla hamjafa kweli.
(NB wale wenye matusi chukueni likizo)

Sasa, kama Chadema inakufa, si ndiyo ahueni kwa Nape na kwako pia? Makelele yote hayo ni ya nini?
 
Sasa we na cheo kikubwa alafu unasema propaganda za ukanda kama vile CCM hakuna watu wa moshi na Arusha? Jaman hizi hoja za kipuuzi kweli CCM mtasalimika kweli 2015? Sisi tunaishi huku mtaani tunashuhudia hasira ya wananchi juu ya sera za CCM au umesahau ile pressure ya igunga na arumeru?

Wito:
Naomba John Mnyika ubuni kamati ya siasa za propaganda na majitaka ili sasa tuanze kuwageuzia kibano kwani naona mchezo wa siasa hoja CCM wameushindwa.
 
Last edited by a moderator:
CDM hamutaiweza CCM tena mtajinyonga wengi sana 2015 maana hamutaamini macho yenu pindi tutakavyoshinda kwa kishindo.....Nape na Mwigulu ni kiboko yenu mbona sisi Mnyika hatumnangi maana hawezi kazi yake ya uenezi? Mumeamua kumchagua wenyewe Mnyika na kumrundikia vyeo kibao kumbe munamkimoa huyu ndugu yangu. MNYIKA take my word CDM hawakupendi majibu yake utayaona 2015

Ww pimbi acha kuongea ujinga.
 
Sasa kwanini Nape hataki CHADEMA ife? Hivi mbona huwa hawatoagi ushauri kwa akina DP, TLP, SAU, NCCR, na kile chama cha cheyo, sasa ndio naelewa maana ya ule msemo "MTI WENYE MATUNDA NDIO UNAOPIGWA MAWE"
 
Mkuu wangu Chitambikwa miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakijitahidi humu JF kutoa Comment zenye mvuto tena zilizosheheni hoja,lakini katika hili mkuu wangu naona umeteleza kabsaaa!!!!!!,yawezekan kwa ababu ya jazba na nini lakini Pole sana.

Kama nimekuelewa vizuri WABHEJASANA ni kwamba unabishana na hiyo takwimu inayohusiana na gharama ya ujenzi wa bomba la gesi sio? Wala usiende mbali tumia google tu utapata kila kitu mathalani pakistan gas pipe project ili uone madudu yanayofanywa na serikali yako ya ccm katika huu mradi wa bomba la gesi mtwara-dsm.

Ukiona mawaziri na rasi wanakuwa wakali sana juu ya harakati za wananchi zinazoendelea ujue wameshawekewa 10% kwenye account zao huko uswisi!!
 
Last edited by a moderator:
Ukweli unauma huo ndio ukweli msipoukubali mpende msipende mta dead,tutawasau .ubaguzi na udini ni janga cdm ingawa mnajifanya hamuoni

Vitegemezi camp.na mtahangaika sana mpaka midomo itawashuka
 
Mkuu wakati nataka kureply pale ulipodai unataka CDM kisife ili kipate kutoa changamoto kwa CCM nikakutana na jibu lako juu kuwa hutaki kife kwa sababu utakuwa huna chama cha kukishambulia humu JF. Natumai hili jibu kwa Aweda should be taken as sense humour taking into consideration that you belong to the caliber that analyse issues with objective and unprejudiced mind. Lakini palepale mtu mwenye hizo virtues kwanini unampa kichwa na jeuri mtu ambaye ujengaji wake wa hoja haukisi level ya elimu aliyokuwa nayo? Kuhalalisha kufa kwa CDM kwa sababu ya kundi masalia na forged cum fabricated expulsion allegations za Shibuda na Zitto ni kushindwa mtu kuitendea taaluma yake haki na siasa kwa ujumla.

Kama kweli CDM itakufa kwa sababu Zitto na Shibuda watafukuzwa basi CDM hakipashwi kuwepo maana mnataka kutuaminisha kuwa toka Tanga mpaka Sumbawanga na Mutukula mpaka Mtwara ni watajwa wawili na kundi lao na masalia ndio CDM. Kwamba wanabaguliwa kwa sababu za kidini na ukanda na hivyo CDM kitakufa. Sijui labda Zitto ajiunge ili apate kufanya supplement kwa hiki kilichoandikwa. Halafu ili ukweli udhihiri kwanini ndugu Nape asiende awahoji au aongee nao waheshimiwa hawa ili waonyeshe kweli wanabaguliwa kwa sababu ya dini,kabila au sehemu wanakotoka? Wakisema hivyo basi atujuze through public communication channels at disposal ambazo zitaturuhusu kuwahoji na sisi pamoja na yeye. Na hapo tunakuwa na balanced story.


Lingine labda nimkumushe Nape kuwa ili utoe tuhuma nzito kama za ukabila, udini na ukanda lazima uwe umefanya tafiti za kutosha ili kukuwezesha kutoa conclusion ya namna hiyo. Lazima atuambie population ya utafiti wake, study areas na samples na sisi tukapime ili tuone kweli zinawakilisha wananchi wote wa Tanzania na hapo tuhuma zionekane zina ukweli ndani yake. Lakini pili tuhuma anazozitoa aangalie zisiwe zinapingana na tambo zetu kimataifa kwenye international fora. Tunajitambulisha kuwa kisiwa cha amani, hatuna ukabila, udini wala ukanda au tofauti zozote. Sasa kama CDM kina hayo yote je wanachama wa CDM sio sehemu ya Tanzania? Ni kweli wana CDM sio integral component ya peace and tranqulity constodians? Naomba anipe majibu haya kwa ufasaha bila jaziba na mimi na wengine tutasema mengine.


Jingine wanasema first put your house in order before turning to your neighbour's. Sijui kama ndani ya nyumba ya Nape kama hakuna moto unaowaka maana mengi yamesemwa kiasi watu wanatishiana pistols, mwenyekiti wake alisema wengine hawaachiani birauri mezani wakiogopa sumu na mengine mengi. Sasa kuna grand corruption kama za EPA, Meremeta, Buzwagi, Richmond/Dowans, Rada ya kuongpzea ndege, ndege ya rais, mikataba ya madini na ukaguzi wake na mengine mengi. Hivi nyumba yenye haya yote mwenye nayo anaweza kwenda kujaribu kusafisha nyumba ya jirani yake/ Kama affirmative basi inahitaji ujasiri wa hali ya juu
Mkuu Bigaraone , big up for the analysis.
Mimi ni mmoja sitafurahi CDM ikifa, CDM inafanya kazi nzuri ni wale wajinga wajinga tu ambao huchukulia criticisms kama matusi na hivyo ku argue in kind.

Wana CDM kama wewe mkuu mpo wachache, wachache sana.
Kwanza kabisa tupo katika dunia ya multipartysm, dunia ya vyama vingi katika nchi karibu zote barani Africa.
Sasa leo vyama mbadala kwa chama tawala huwa inaleta a fresh breath of air in politics.
Kama kuna makosa katika vyama hivyo basi hayo ni makosa yao yanayoweza kutokea kwa kila chama.
Ni lazima tujipambanue kuwa chama kioja kinapofanya makosa, basi kingine kina capitalise makosa hayo na kuyashambulia vilivyo.

Huwa mimi ni mpezi wa kipindi cha PMQ(Prime Ministers Questions time), kipindi cha House of Commons Uingereza.

Jamaa wale wanavyoshambuliana utafikiri watashikana mashati punde!
Lakini mwisho wa siku wako pamoja kwa masuala ya mshikamano wa kitaifa.

Kama nilivyosema hapo nyuma makosa ya kisiasa hayako CDM tu, bali hata CCM, NCCR, CUF n.k.
Kwa upande mmoja bango lilishikwa na CDM wakati wa EPA,RICHMOND , Kagoda na kasha nyingine naweza kusema zilikuwa na taifa hili at heart.
Tuna kumbuka vizuri wengine ilibidi tuishambulie CCM wazi wazi kwa kushindwa kuchukua hatua kwa kashfa hizo, wale ambao watapinga fungueni archives za JF ili mjiridhishe-hakuna anayependa kuibiwa.

On the otherhand CDM imeanza kubweteka na umaarufu wake, imekuwa complacent, and complacency breeds laisszes faire, watu wameanza kujiona miungu watu, they cant do no bad.

Na hapo ndipo CCM inawa-nail!
Piga msumari haswa.

Kwamba kuna matumizi mabaya ya ruzuku
Kwamba kuna ubaguzi
Kwamba hakuna utawala bora ndani ya chama
Kwamba chama kilianza kuvuka hata mipaka ya madaraka yake na kujiona kinaweza kupambana na dola kutokana na wingi wa wapenzi

Sasa hayo ni makosa megine yanayotokana na hiyo complacency, na kujiona kujua.

Wenzenu ccm hatujalala, kuna kazi mbili tu.
Moja ni kujenga nchi na kuongoza
Pili ni kujibu mashambulizi ya vyama vingine kama CDM, CUF nk, na kwa maoni yangu yote yanafanyika vizuri sana tu.

Nakushukuru Bigaraone kwa kuonyesha jinsi ya kujenga hoja mtandaoni ili facts zionekane badal ya wale wenye matusi yanayotokana na utupu wa vichwa vyao.

Tutapingana katika hoja , lakini tutaijenga Tanzania yetu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom