Nape: Dhambi ya ubaguzi inaimaliza CHADEMA!

Nape: Dhambi ya ubaguzi inaimaliza CHADEMA!

Wito:
Naomba John Mnyika ubuni kamati ya siasa za propaganda na majitaka ili sasa tuanze kuwageuzia kibano kwani naona mchezo wa siasa hoja CCM wameushindwa.

mKUU Shardcole hiyo kamati ya nini wakati tuliopo hapa JF tunawamudu hawa vibaraka? kuna hoja gani imewahi kuja hapa tukashindwa? hakuna sababu ya kumuumiza kichwa mnyika kwa sababu ya hawa vibaraka wa lumumba.
 
Last edited by a moderator:
Atuambie kwa nini jina lake halipo hapa

BrigGen+NnauyeKisw.jpg

Eeh! kweli hayupo.
 
CDM hamutaiweza CCM tena mtajinyonga wengi sana 2015 maana hamutaamini macho yenu pindi tutakavyoshinda kwa kishindo.....Nape na Mwigulu ni kiboko yenu mbona sisi Mnyika hatumnangi maana hawezi kazi yake ya uenezi? Mumeamua kumchagua wenyewe Mnyika na kumrundikia vyeo kibao kumbe munamkimoa huyu ndugu yangu. MNYIKA take my word CDM hawakupendi majibu yake utayaona 2015

mwigulu ni nani? au ndio lile chemba la choo kinachotumika pindi watu wanapoenda kujisaidia pindi wanaposhuka sekenke kuelekea shelui? au mwigulu aliyefumaniwa igunga? au mwigulu aliyenunua jina la mwanafunzi huko kyengege?
 
Wenzenu ccm hatujalala, kuna kazi mbili tu.
Moja ni kujenga nchi na kuongoza
Pili ni kujibu mashambulizi ya vyama vingine kama CDM, CUF nk, na kwa maoni yangu yote yanafanyika vizuri sana tu.
Tutapingana katika hoja , lakini tutaijenga Tanzania yetu

Kwanza kabisa masopakyindi nikufahamishe kwamba ccm haijengi nchi na wala haiongozi hii nchi, kinachofanyika ni kwamba mnaitafuna na kuitawala. Katika hili mmeshapoteza legitimacy yenu kwa watanzania.

Pili usidanganye watu kwamba mnajibu mashambulizi ya vyama vingine kama Chadema na cuf. Hawa cuf mnashirikiana kuendesha serikali kule zenji na tangu wakati huo hatujawahi kuwasikia viongozi wenu wa ccm wakipanda kwenye majukwaa ama mashabiki wa ccm kwenye mitandao wakiishambulia cuf.

Tunachoshuhudia kila kukicha si kwa viongozi tu bali hata wapenzi, mashabiki pamoja na vibaraka wa ccm ni kuishambulia Chadema tu kila uchao. Kiongozi yeyote wa ccm akizungumza na wanaccm wenzake bila kuitaja Chadema anaweza kupondwa mawe. Hata mzee wassira alijipatia kura za kishindo akiwania ujumbe wa nec kwa ahadi kwamba yeye ndiye kiboko ya Chadema!! kwamba imefika mahali wanaccm wakiisikia Chadema wanaumwa matumbo ya kuhara!!

Kama haitoshi ccm mmeamua kutenga fungu maalum la kuendesha propaganda chafu dhidi ya Chadema kwa kuwalipa waandishi wa habari wa magazeti, televison na wamiliki wa mitandao ya kijamii ili wawasaidie kufanya propaganda chafu. Mmekwenda mbali kiasi cha kuajiri vijana na kuwapatia vitendea kazi (computer) ili wakeshe mitandaoni kuwatukana viongozi wa Chadema.

Kwanini hizo nguvu msizielekeze kwenye kutekeleza ilani yenu ya uchaguzi ili wananchi wenyewe wajionee maendeleo mliyowaletea badala ya kuzungusha mawaziri mikoani kuyatetea maendeleo yasiyoonekana? hivi kweli kiongozi mzima na akili yake anawaambia wananchi kwamba ccm imeleta maendeleo mwanza kwakuwa sasahivi kuna mabugando mengi tofauti na ilivyokuwa hapo awali!!??
 
Last edited by a moderator:
mKUU Shardcole hiyo kamati ya nini wakati tuliopo hapa JF tunawamudu hawa vibaraka? kuna hoja gani imewahi kuja hapa tukashindwa? hakuna sababu ya kumuumiza kichwa mnyika kwa sababu ya hawa vibaraka wa lumumba.
Mkuu mbona unaanza kuongea kama wale sans culote.
Na ukitaka kueleweka jibu maswali na tuhuma kwa ufasaha maana hapa unaongea na dunia.
 
ZITTO ameisha wajibu. Mradi wa gesi duniani kote ni 1.2mill/mile,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,Tanzania chini ya ccm ni 2.2mill/km

aaaaaah masihara hayooo!!!mile si ndo kubwa kuliko km?so why ndogo bei juu ya hiyo kubwa?kama Taifa tunatakiwa kuingia kwenye mjadala coz hii me naamini ni mbinu mbadala ili tuupinge mradi waendelee kula kwenye mafuta mazito!!yaani hadi naona kama miaka inarudi nyuma hiyo 2015 inazidi kwenda mbaali
 
aaaaaah masihara hayooo!!!mile si ndo kubwa kuliko km?so why ndogo bei juu ya hiyo kubwa?kama Taifa tunatakiwa kuingia kwenye mjadala coz hii me naamini ni mbinu mbadala ili tuupinge mradi waendelee kula kwenye mafuta mazito!!yaani hadi naona kama miaka inarudi nyuma hiyo 2015 inazidi kwenda mbaali

Hela wanazotumia kuzunguka na kuchafua wenzao zinatoka wapi? hawajali maneno wanayosema wanajali kula na kuchonganisha
 
Katibu wa NEC-CCM Nape NNauye ambaye vile vile ni Mkuu wa Itikadi na Uenezi, ametoboa siri ya kifo cha CHADEMA kuwa kitatokana na ubaguzi kati ya wananachama wake.

Ingalau magazeti mawili yamemnukuu akikomelea msumari katika tofauti zinazojitokeza hivi sasa ndani ya CHADEMA.Gazeti la Majira (21/1/2013) lenyewe limedai kwamba :

"Nape afichua siri za kifo cha CHADEMA, na kudai-hakuna dawa ya kutumia lazima kife-ameendelea kudai ni laana ya Nyerere, wasitafute mchawi"

Page 4 ya gazeti hili linaendelea

"Alisema(NAPE) ubaguzi ulioota mizizi kwa muda mrefundio unakimalizachama hichoambao umelelewa na waasisi pamoja na viongozi wa kitaifa hivyo kina haki ya kufa kutokana na dhambi hiyo"

Aliendelea...

"Hamuwezi kuwa na chama ambacho kinaendekeza ubaguzi..ili kiongozi wake adumu na kuheshimika lazima atoke ukanda fulani au ukoo fulani vinginevyo anasukiwa mizengwe na kutimiliwa. Walianza na marehemu Wangwe.... hivi sasa wameanza kumuandama Zitto Kabwe(Naibu Katibu Mkuu CHADEMA) na wanaoitwa vijana wake, nasikia wiki ijayo wamejipanga kumfukuza Shibuda(Bunge wa Maswa)"

Nnauye akamalizia kwa msumari mzito

"CHADEMA ni chama kidogo kinabaguana kiasi hicho, wakipewa dhamana ya kutawala nchi hali itakuwa mbaya zaidi"


My take

Wana CHADEMA huo ni msumari unaoweza kuwa mkuki moyoni.
Jisahihisheni kabla hamjafa kweli.
(NB wale wenye matusi chukueni likizo)

Siku zote nasema a dying horse always kick hard! Ccm is dying so hawawezi kufa bila kusema chochote why are they busy with cdm matters? Nape ni tunda la ubaguzi kwani nani angempa cheo kama babake asingekuwa comrade wa jk? Aache siasa za maji taka
 
Tatizo liko kwenye vyama vya upinzani au chama tawala?Kama Chama tawala kitaridhia kwa uhakika kwamba vyama vingi ni haki ya kila raia basi hakuna matatizo ya vyama vya upinzani.
 
Ndo mnapukutika hivo , wakati gari kubwa linachnja mbuga.
Chama chenu kitajiua chenyewe.

Ni kama kisu kinakata koo lakini mateke yanapigwa. Kwa wasiojua hilo wanaweza wakapatwa na kifo kutokana na mateke. Nape anajihami na mradi uliogarambuka.
 
sasa yeye ikifa si ndio atafurahi? sasa wasiwasi wake nini? au hajui alisemalo?
 
Sioni jipya. Kama mtazamaji,naona hayo yanayotokea CHADEMA ni matatizo "cosmetic". Sijaona hata mtu mmoja amechambua sera za CHADEMA na kusema ya kuwa ni mbaya na au hazitufai kupeleka Tanzania huko tunakotaka iende. Sanasana ninayoona ni vijimananeno vya kijiweni na au maneno yanayostahili kuitwa maneno udaku. Hivi, leo hii watu wenye akili timamu wanaweza kukaa chini na kuanza kujadili swala la Dr. Slaa kuwa na kadi ya CCM kama ni issue inayopaswa kujadiliwa? Au kukaa chini na kujadili mamboya kupandikizapandikiza au ya kuhisihisi anayosema Nape? . Eti walianza na Wangwe ... na sasa wanamuandama Zitto Kabwe. Halafu ukiuliza ushahidi hamna. This is preposterous!!. Are we this low and light headed?

Hii inadhihirisha ni kwa jinsi gani Tanzanania tumewekeza kwenye mambo ya kipuuzi na kuzalisha watu wapuuzi ambao kila kukicha kazi yao ni kuchambua na kujenga hoja za kipuuzi. Mambo ya kipuuzi
 
Mkuu Bigaraone , big up for the analysis.
Mimi ni mmoja sitafurahi CDM ikifa, CDM inafanya kazi nzuri ni wale wajinga wajinga tu ambao huchukulia criticisms kama matusi na hivyo ku argue in kind.

Wana CDM kama wewe mkuu mpo wachache, wachache sana.
Kwanza kabisa tupo katika dunia ya multipartysm, dunia ya vyama vingi katika nchi karibu zote barani Africa.
Sasa leo vyama mbadala kwa chama tawala huwa inaleta a fresh breath of air in politics.
Kama kuna makosa katika vyama hivyo basi hayo ni makosa yao yanayoweza kutokea kwa kila chama.
Ni lazima tujipambanue kuwa chama kioja kinapofanya makosa, basi kingine kina capitalise makosa hayo na kuyashambulia vilivyo.

Huwa mimi ni mpezi wa kipindi cha PMQ(Prime Ministers Questions time), kipindi cha House of Commons Uingereza.

Jamaa wale wanavyoshambuliana utafikiri watashikana mashati punde!
Lakini mwisho wa siku wako pamoja kwa masuala ya mshikamano wa kitaifa.

Kama nilivyosema hapo nyuma makosa ya kisiasa hayako CDM tu, bali hata CCM, NCCR, CUF n.k.
Kwa upande mmoja bango lilishikwa na CDM wakati wa EPA,RICHMOND , Kagoda na kasha nyingine naweza kusema zilikuwa na taifa hili at heart.
Tuna kumbuka vizuri wengine ilibidi tuishambulie CCM wazi wazi kwa kushindwa kuchukua hatua kwa kashfa hizo, wale ambao watapinga fungueni archives za JF ili mjiridhishe-hakuna anayependa kuibiwa.

On the otherhand CDM imeanza kubweteka na umaarufu wake, imekuwa complacent, and complacency breeds laisszes faire, watu wameanza kujiona miungu watu, they cant do no bad.

Na hapo ndipo CCM inawa-nail!
Piga msumari haswa.

Kwamba kuna matumizi mabaya ya ruzuku
Kwamba kuna ubaguzi
Kwamba hakuna utawala bora ndani ya chama
Kwamba chama kilianza kuvuka hata mipaka ya madaraka yake na kujiona kinaweza kupambana na dola kutokana na wingi wa wapenzi

Sasa hayo ni makosa megine yanayotokana na hiyo complacency, na kujiona kujua.

Wenzenu ccm hatujalala, kuna kazi mbili tu.
Moja ni kujenga nchi na kuongoza
Pili ni kujibu mashambulizi ya vyama vingine kama CDM, CUF nk, na kwa maoni yangu yote yanafanyika vizuri sana tu.

Nakushukuru Bigaraone kwa kuonyesha jinsi ya kujenga hoja mtandaoni ili facts zionekane badal ya wale wenye matusi yanayotokana na utupu wa vichwa vyao.

Tutapingana katika hoja , lakini tutaijenga Tanzania yetu


Masopakyindi niseme always pleasure.

Umeelezea vizuri na kwa ufasaha why you want strong party to exist side by side. However, ili ukishambulie chama kinachotoa opposition ya kweli kwako unahitaji facts amabazo zinahitaji conceptual framework ambayo ina umakini ili kwamba usije ukajikuta ulichosema jana kinaingana na unachosema leo. Nape naona framework yake ni ya hatari sana maana inaleta maswali mengi ambayo anaweza kushindwa kuyajibu. Nimesema huko kwenye internationa fora tunajisifia kuwa nchi ya amani ambayo imechangiwa na ukarimu wa Watanzania CDM wakiwemo, undugu ambao hauna chembe ya udini wala ukabila wala ukanda. Sasa kama CDM are labouring all the vices inaonyesha viongozi wetu hawasemi ukweli bali wanapaka uongo wanja ili kuvutia wawekezaji. Lakini kama si kweli basi single hii ya udini, ukabila na ukanda tuiache.

Nakubaliana na wewe kuwa complacency, oversatisafaction and megalomenia sio mambo mazuri katika medani sio ya siasa bali katika hali yote ya maisha kiuchumi, kisiasa na kiutamadaduni. Tunatakiwa kuendeleza mafanikio n kubuni mambo mapya. Sijui sasa complancency inahalalisha tuhuma alizosema Nape na nyingine ulizoongeza. Kwa sababu Nape hajajiunga ili ajibu mambo niliyosema nampa muda. Labda kwa kifupi turudi kwa yale uliyosema.

Matumizi mabaya ya ruzuku- sijui kuna ukweli kiasi katika hili maana na wewe umeliweka limebaki skeleton calling to be stuffed by fresh interms of cost and profit analysis. CAG ambaye kisheria anakagua mahesabu ya vyama sijui kama aliwahi kutoa dirty certificate kwa CDM na leo kikawa branded of embezzlement. Tunaoma ushahidi usio na shaka katika hili.

Ubaguzi-naona umelirudia ambalo nimemwomba mwenye kusema hayo aje na researched facts. Mpaka sasa ni uzushi tu

Dola- inapata legitimacy kutoka kwa watu. Dola indiyo inajidhalilisha inapotumia ammunitions excessively kupambana na watu ambao hawako armed na huku ikijua ina supress haki ya kujumuika. Nafikiri unaoongelea ya Arusha, Morogor na Iringa. La Iringa ni kichekesho maana unazuia chama kimoja mikutano tena ya ndani lakini kingine kinaruhusiwa kupiga kampeini waziwazi
 
source yenyewe ya kipuu eti uhuru gazeti.mtasubiri sna cdm kufa.ilikufa CCJ ikiwa bado mimba na wbsisi wake ni wanafiki ndani ya CCM.
 
Wacha kife kwanza ni sacoss ya wa kaskazini
 
Soma vizuri wewe sio una kurupuka Majira imekuwa uhuru mtajinyea sana.
source yenyewe ya kipuu eti uhuru gazeti.mtasubiri sna cdm kufa.ilikufa CCJ ikiwa bado mimba na wbsisi wake ni wanafiki ndani ya CCM.
 
Senior MemberArray


Join Date : 3rd July 2012
Posts : 219
Rep Power : 372
Likes Received24
Likes Given22


[h=2]
icon1.png
Npe aanza kufunga virago[/h]
nape nauye rudi ccj mapema maana unaona kasi ya mheshimiwa mtarajiwa edward lowassa anavyong'ara.wahenga walisema usitukane wakunga na uzazi ungalipo,ulimkashifu sana lowasa ukamuuta fisadi,ukamuta gamba ndani ya chama ukampa siku 90. Sasa nape kikwete anaondoka 2015 na lowasa anongoza ngome ya ccm kwa ukweli weka hii taarifa vizuri utasahaulika ndani ya ccm na utajutia domo kaya lako,if u don't believe call me na nikupe data zako zote.pole sana maana chadema hawatakuchukua maana wewe na nchemba ni member wa masalia labda cuf tu.lowasa ni kiongozi jasiri aakayeweza kufukuza wapuuzi wote ndani ya ccm viva lowasa. ccm mnajua bila ya lowassa na kundi lake hamna pesa za kuendesha chama.[COLOR=#49535A !important] +447534130796


[/COLOR]
 
Back
Top Bottom