Nape: Dhambi ya ubaguzi inaimaliza CHADEMA!

Nape: Dhambi ya ubaguzi inaimaliza CHADEMA!

Sasa ndio umeongea nini?Na wewe unajua kuwa hapo ueposti utumbo!

Najua huwezi kukubali lakini ndio ilivyo kwa jambo leo,majira,na sasa mwananchi,lengo ni kuongeza wigo katika propaganda,naomba mungu nipashe hisiingie huko,na nasali pia mwanahalisi irudishwe maana makala zile za dr.ulimboka zilizokuwa zinachambualiwa kwa akili za kiintelegensia (sio kama za kuzuia maandamo na kuuwa raia wa kigeni na kuwapa majina ya kitanzania) zimeliponza,najua mungu atasikia sala zangu.
 
nape acha kudanganya watz zito hata kidogo haandamwi cdm ila bwana shibuda nimtu wenu
 
Hizi siasa za Nape za ajabu sana..hivi hamuwezi kufanya mkutano bila kuitaja cdm,kweli dr slaa kawashika pabaya
 
Kwanza kabisa masopakyindi nikufahamishe kwamba ccm haijengi nchi na wala haiongozi hii nchi, kinachofanyika ni kwamba mnaitafuna na kuitawala. Katika hili mmeshapoteza legitimacy yenu kwa watanzania.

Pili usidanganye watu kwamba mnajibu mashambulizi ya vyama vingine kama Chadema na cuf. Hawa cuf mnashirikiana kuendesha serikali kule zenji na tangu wakati huo hatujawahi kuwasikia viongozi wenu wa ccm wakipanda kwenye majukwaa ama mashabiki wa ccm kwenye mitandao wakiishambulia cuf.

Tunachoshuhudia kila kukicha si kwa viongozi tu bali hata wapenzi, mashabiki pamoja na vibaraka wa ccm ni kuishambulia Chadema tu kila uchao. Kiongozi yeyote wa ccm akizungumza na wanaccm wenzake bila kuitaja Chadema anaweza kupondwa mawe. Hata mzee wassira alijipatia kura za kishindo akiwania ujumbe wa nec kwa ahadi kwamba yeye ndiye kiboko ya Chadema!! kwamba imefika mahali wanaccm wakiisikia Chadema wanaumwa matumbo ya kuhara!!

Kama haitoshi ccm mmeamua kutenga fungu maalum la kuendesha propaganda chafu dhidi ya Chadema kwa kuwalipa waandishi wa habari wa magazeti, televison na wamiliki wa mitandao ya kijamii ili wawasaidie kufanya propaganda chafu. Mmekwenda mbali kiasi cha kuajiri vijana na kuwapatia vitendea kazi (computer) ili wakeshe mitandaoni kuwatukana viongozi wa Chadema.

Kwanini hizo nguvu msizielekeze kwenye kutekeleza ilani yenu ya uchaguzi ili wananchi wenyewe wajionee maendeleo mliyowaletea badala ya kuzungusha mawaziri mikoani kuyatetea maendeleo yasiyoonekana? hivi kweli kiongozi mzima na akili yake anawaambia wananchi kwamba ccm imeleta maendeleo mwanza kwakuwa sasahivi kuna mabugando mengi tofauti na ilivyokuwa hapo awali!!??
Mkuu Mwita Maranya , a.k.a "Murra", umechanganyikiwa.

Inaelekea toka umeingia DSM hujawahi kurudi kwenu kutambika.
Na ndio maana unashindwa kuona hata maendeleo yanayoonekana dhahiri hata kwenu.

Haijapita hata miaka kumi, na umesahau kuwa kufika Musoma mlikuwa mkipitia Sirari mkitokea Kenya.
Na hii ni kwa vile barabara zilikuwa mbovu kiasi cha kutopitika, meshaambiwa andamaneni tena sana katika barabara zilizojengwa na serikali ya CCM.

Mkuu look around you na utaona jinsi ilani ya CCM inavyotekelezwa.

Maendeleo utayaonaje na wewe ni kinara wa M4C?
Kutwa kuchwa kupanga mipango isiyoendelevu ya maandamano?

Tembelea miji ya Mwanza, Singida hata Arusha na uone jinsi unavyoweza kufika kwenu haraka kwenye ngoma za mababu huko Musoma.
Na hii si barabara tu, hata nauli ya 32,000 ya Fastjet inakushinda mkuu?
Na huduma hiyo ingekujaje kama si sera nzuri za maandalizi kuvutia wawekezaji?

Kama wewe na chama chako mkiamua kufumbia macho maendeleo ya wazi nchini, hatuna budi kuwahurumia tu, maana nyie mawazo yote yako kwenye maandamano.

Ni sehemu chache sana mlizoweza kuhumiza maendeleo, hata zile mlizo shinda katika viti vya ubunge.

,baya zaidi chama chenu kinakosa mvuto kwa kasi.Kelele na shutuma za uongozi mbaya ndani ya chama chenu hazikuasisiwa na CCM.

Ccm haikumtuma Dr Slaa kujichotea mapesa ya ruzuku kwenye hazina ya chama chenu, na sasa mnaanza kuona kuwa ni rahisi kulaumu tu na kutoa shutuma zisizo na mashiko.

Kuendesha chama noma!
Mnajifunza the harsway kuwa chama si cha waliokianzisha bali kinatakiwa kuwa chama cha wanachama.
No wonder watoto wadogo umri wa watoto wenu wanawavua nguo hadharani.
Narudia, hakuna mtu anayependa kuibiwa.

Hili la ubaguzi sitaliongelea sana maana limeshajadiliwa kwa kirefu sana hapa , kama mna masikio na msikie.

Sasa hivi upende usipende, CHADEMA is under a shadow cast of doubt.
Dr Slaa anjinafasi na fungu la chama
Mkewe anajinadi kisiasa mikoani kwa fungu la chama
Chama kinatimua wale wanohoji mwelekeo hasi
M4c yenyewe ilianza kuwa kiwanda cha mauaji
Mwenyekiti Mbowe , kimya utafikiri ana muogopa katibu wake
Mzee Mtei ndo kabisa amedozi, anaamshwa akiambiwa Zitto anataka kugombea uraid!

Mkuu hiyo limelight ya chama chenu ilishafika peak, na sasa inzidi kuporomoka kwa kasi.
 
Last edited by a moderator:
cdm mmekwisha nawaambia . na mrema aje na majibu jins mlivyotumia mil 500 za m4c au ndio mlikopesha baba junior

watu wengine bwana! "ok katito ka mbi madi magneto okwuo munn" sisiem ! Kwishaaaa kwasababu mmepractice vizuri "propaganda" na kuzidi kuipa cdm nafasi! Trust me! You gonna remember this yoo!
Nape & co!
 
wale waliokuwa wanambagua salim wakati wa kugombea urais 2005 kwa tiketi ya ccm walikuwa hawana dhambi au ndio walikuwa wanatekeleza wosia wa baba wa taifa Nape aache kuropokakwani kauli zake ni kama anajitusi ubaguzi,ukanda,umeshamiri baada ya uchaguzi wa ccm mwaka 2005
 
yaelekea CDM inawanyima usingizi hasa hawa jamaa maana hawafanyi mengine zaidi ya kuishitaki CDM kila kukicha wananchi wa leo sio wa miaka ya nyuma wa kudanganywa tena kama watoto
 
Mmmh... hivi ni rahisi kuona moto unaowaka nyumba ya jiranikuliko wa nyumbani kwako? Yetu macho, tataendelea kuona rangi zote za huyu jamaa maana tangu ashindwe kuwawajibisha mafisadi ndani ya sisiemu ndani ya siku 90 sasa kila kukicha anaanzisha sinema. Mara ageuke kuwa mkuu wa watumishi wa umma serikalini kwa kuamrisha watumishi kuhudhuria mikutano ya sisiemu, mara mshauri wa CDM n.k. Tatizo lake ni kuwa sinema zake huwa hazikai sokoini muda mrefu. Tunaendelea kusubiri sinema nyingine ambayo nayo hatakaa muda.... kwa kifupi huyo jamaa ni mwepesi kuliko upepo wa kisulisuli. Period!
 
Kama issue ni laana toka kwa Mwl Nyerere basi waliyo na laana ni CCM!

Rejea:
Nyerere ALIKATAA KUUZWA KWA BENKI YA NBC
Nyerere alikataa ubinafishaji
Nyerere alikataa kujilimbikizia mali
Nyerere alikataa rushwa na Chenge na wenzake wasingepona angekuwepo hai
Nyerere ASINGERUHUSU kuuzwa nyumba alizoshiriki kuzijenga kwa mikono yake mwenywe
Nyerere ASINGEWEZA MTEUA NAPE kuwa kiongozi wa kitaifa CCM!
NK:::::
Wenye laana ya Nyerere ni CCM
 
Nape ulipoomba uwe mgombea wa CHADEMA Ubungo sio kwamba Mnyika alipendelewa bali uwezo wako ulikuwa mdogo ukilinganisha na Mnyika.
 
Katika Medani za siasa huyu bwana huwa hanivutii kabisa sijui kwa nini? I hate him. nahisi ni kwa sababu ya mdomo wake. Anahuruka mbaya sana na huwa hana break. Haongei kwa staha na kutoa hoja kama redio Tanzania. Anafanana na redio inayoitwa clouds FM. Hoja alizotoa hapo chini kwa mtu aliyepevuka kiakili ni hoja dhaifu sana. Kaka N, jitahidi kuwa na akili sasa umekuwa!!!


Katibu wa NEC-CCM Nape NNauye ambaye vile vile ni Mkuu wa Itikadi na Uenezi, ametoboa siri ya kifo cha CHADEMA kuwa kitatokana na ubaguzi kati ya wananachama wake.

Ingalau magazeti mawili yamemnukuu akikomelea msumari katika tofauti zinazojitokeza hivi sasa ndani ya CHADEMA.Gazeti la Majira (21/1/2013) lenyewe limedai kwamba :

"Nape afichua siri za kifo cha CHADEMA, na kudai-hakuna dawa ya kutumia lazima kife-ameendelea kudai ni laana ya Nyerere, wasitafute mchawi"

Page 4 ya gazeti hili linaendelea

"Alisema(NAPE) ubaguzi ulioota mizizi kwa muda mrefundio unakimalizachama hichoambao umelelewa na waasisi pamoja na viongozi wa kitaifa hivyo kina haki ya kufa kutokana na dhambi hiyo"

Aliendelea...

"Hamuwezi kuwa na chama ambacho kinaendekeza ubaguzi..ili kiongozi wake adumu na kuheshimika lazima atoke ukanda fulani au ukoo fulani vinginevyo anasukiwa mizengwe na kutimiliwa. Walianza na marehemu Wangwe.... hivi sasa wameanza kumuandama Zitto Kabwe(Naibu Katibu Mkuu CHADEMA) na wanaoitwa vijana wake, nasikia wiki ijayo wamejipanga kumfukuza Shibuda(Bunge wa Maswa)"

Nnauye akamalizia kwa msumari mzito

"CHADEMA ni chama kidogo kinabaguana kiasi hicho, wakipewa dhamana ya kutawala nchi hali itakuwa mbaya zaidi"


My take

Wana CHADEMA huo ni msumari unaoweza kuwa mkuki moyoni.
Jisahihisheni kabla hamjafa kweli.
(NB wale wenye matusi chukueni likizo)
 
Katika Medani za siasa huyu bwana huwa hanivutii kabisa sijui kwa nini? I hate him. nahisi ni kwa sababu ya mdomo wake. Anahuruka mbaya sana na huwa hana break. Haongei kwa staha na kutoa hoja kama redio Tanzania. Anafanana na redio inayoitwa clouds FM. Hoja alizotoa hapo chini kwa mtu aliyepevuka kiakili ni hoja dhaifu sana. Kaka N, jitahidi kuwa na akili sasa umekuwa!!!
Unahitaji msaada,
Chuki binafsi si part of politics.

You have a personality problem.
Jaribu kumwona Kakobe.
 
Unajua mile ni kubwa kuliko km yaani ni hivi

1mile = 1.6093km (source >>>Miles to Kilometers conversion)

Kwa pesa halali ya ujenzi bomba la gesi kama Zitto alivyoeleza katika vipimo vya km (kilometre) ni U$.745,667.00 kwa kilometre moja (U$745,667.00/km). Wakati kwa viwango visivyo halali vinavyoelezwa hapa ni kuwa U$ 2,200,000.00 kwa kilometre moja (U$2,200,000.00/km).

Kwa hiyo kwa kila kilometre moja itakayounganishwa bomba la kusafirisha gesi basi kuna hela isiyo halali itakayo liwa na wajanja ambayo ni U$ 1,454,334.00, (U$1,454,334.00/km)

Sasa jiulize ni kilometre ngapi zitajengwa za bomba la gesi kutoka Ntwara mpaka Daslaam. Ukizipata hizo kilometre uzidishe na hizo hela zitakazoliwa na wajanja kwa kila kilometre ili upate jumla kuu ya pesa zitakazo liwa na wajanja. Na ukishakupata jumla kuu hiyo ifikirie ingeweza kutataua kwa kiwango gani kero za watanzania kwenye afya na elimu.

Siyo wajanja ni wauwaji, wabakaji, wahuni na wezi wakubwa
 
Mkuu siasa ndivyo zilivyo dunia nzima, usitegemee kwamba watu watadiscuss mambo magumu tu, hata mepesi yaweza kubadili mwelekeo wa siasa.

Nakumbuka miaka kadhaa iliyopita Reaga alipokutana na Gorbachev baada ya kutambiana kwa muda muda mrefu, Dorbachev alipepesa macho na hiyo ilimpa ushujaa wa kutosha Reagan.

Reagan alitamba" He blinked first"
Na ikawa issue kubwa kisiasa.

Wa kumwelewa walimwelewa.

Mahali pa mambo ya utani au mzaha unaweka utani au mzaha na pahala ambapo kunahitaji seriousness kadhalika unafanya vivyo hiyo. Tatizo letu sisi kuwa tunawekeza sana kwenye mambo ya kipuuzi na kuyavuvia maisha kana kwamba ni mambo ya kweli na ya msingi na mbaya zaidi kufanya masihara katika mambo ya msingi. Mimi sikubaliani na dhana ya kuyapa mambo mepesi nafasi ya mambo ya msingi. Hapo lazima utapotea tu. Na haya mambo siyo magumu kama ulivyosema wewe, hapana ni mambo ya msingi na mambo ya msingi. Na nikatoa mfano kuwa kujadili swala Dr. Slaa kuwa na kadi ya CCM si swala,lakini swala ni kama je sera na mipango ya CHADEMA inaweza ikatutoa hapa tulipopokwama kama taifa na kutupeleka mbele? La kwanza ni jepesi lisilo na mashiko na la pili ni la msingi. Na si busara kusema kuwa dunia nzima ndivyo ilivyo. Hiyo ni kauli ya jumlajumla sana. Hao unaosema huko duniani hawana mzaha wala masihara katika mambo ya msingi. Kwa mfano haitapata kutokea kwa Seniour Cabinet Secretary(Waziri Mwandamizi) wa Rais Obama kusema maneno aliyosema Waziri Wassira kwamba atahakikisha kuwa anaisambaratisha CHEDEMA ndani ya mwaka mmoja(kwa maana na makusudi aliyosema yeye Wassira). Maneno ambayo kwa mazingira ya kisiasa ya Tanzania inaeleweka kwamba Wassira alilenga nini. Kwa maneno kama hayo, Waziri huyo wa Obama angeiona ofisi yake kuwa chungu kesho yake! Huko ndiko duniani unakosema- ndivyo mambo yalivyo

Mimi nachosema ni kuwa mambo ya msingi yana nafasi yake na yale mepessi pia. Lakini ni makosa kujadili mambo mepesi kwa kutumia lensi ya yale mambo ya msingi. Ni makosa.
 
Mahali pa mambo ya utani au mzaha unaweka utani au mzaha na pahala ambapo kunahitaji seriousness kadhalika unafanya vivyo hiyo. Tatizo letu sisi kuwa tunawekeza sana kwenye mambo ya kipuuzi na kuyavuvia maisha kana kwamba ni mambo ya kweli na ya msingi na mbaya zaidi kufanya masihara katika mambo ya msingi. Mimi sikubaliani na dhana ya kuyapa mambo mepesi nafasi ya mambo ya msingi. Hapo lazima utapotea tu. Na haya mambo siyo magumu kama ulivyosema wewe, hapana ni mambo ya msingi na mambo ya msingi. Na nikatoa mfano kuwa kujadili swala Dr. Slaa kuwa na kadi ya CCM si swala,lakini swala ni kama je sera na mipango ya CHADEMA inaweza ikatutoa hapa tulipopokwama kama taifa na kutupeleka mbele? La kwanza ni jepesi lisilo na mashiko na la pili ni la msingi. Na si busara kusema kuwa dunia nzima ndivyo ilivyo. Hiyo ni kauli ya jumlajumla sana. Hao unaosema huko duniani hawana mzaha wala masihara katika mambo ya msingi. Kwa mfano haitapata kutokea kwa Seniour Cabinet Secretary(Waziri Mwandamizi) wa Rais Obama kusema maneno aliyosema Waziri Wassira kwamba atahakikisha kuwa anaisambaratisha CHEDEMA ndani ya mwaka mmoja(kwa maana na makusudi aliyosema yeye Wassira). Maneno ambayo kwa mazingira ya kisiasa ya Tanzania inaeleweka kwamba Wassira alilenga nini. Kwa maneno kama hayo, Waziri huyo wa Obama angeiona ofisi yake kuwa chungu kesho yake! Huko ndiko duniani unakosema- ndivyo mambo yalivyo

Mimi nachosema ni kuwa mambo ya msingi yana nafasi yake na yale mepessi pia. Lakini ni makosa kujadili mambo mepesi kwa kutumia lensi ya yale mambo ya msingi. Ni makosa.

Mkuu whether ni utani au mambo mgumu, yote ni relative.

Utani waweza kueleza na kufikisha ujumbe kwa njia iliyo rahisi na isiyoudhi kwa jamii.
Lakini utani vile vile inaweza kuonyesha ufinyu wa mantiki ya argument iliyotolewa ndani ya mada.

Na kwa vyovyote vile wananchi wote nchini si wasomi,lakini ni waelewa sana wa mantiki katika utani unaoleta ujumbe.

Na kwa taarifa yako ukifikiri utani ni upuuuzi basi nakutaarifu kuwa linaweza kuwa somo zima katika somo la psychology na logic.

Kwa mtu makini sana atatambua point kubwa na ujumbe unaoletwa na utani huo.
 
Nape ni mtu mdogo(si kiumri,ni kiakili)angekua amepevuka angejiuliza nini kinasababisha mafuta ya taa kuuzwa bei moja na diesel,wakat ni westproduct,pia angehoji nin kinasbabisha unga wa sembe kuuzwa 1400 kwa kg,ni mvivu wa kusoma historia angejua kua hata afanyaje hawez kufikia hadhi y hayat Korimba ndan y ccm...
 
Usishangae sana masika kuwa na mbu wengi, ndio kawaida yake!
CDM kikiacha sera za ubaguzi kinaweza kujikongoja hadi 2015, kisipoacha sera hizo achilia mbali kufa , KITAUWAWA na wanachama wake wenyewe.

Sisi, mimi kama CCM natambua mchango wa sera za vyama vingi.
Kwa kuendekeza ubaguzi CHADEMA ina kosa relevance ya kuwa chama makini kisiasa.

vyama viko zaidi ya 18 siyo ? kwanini unahofia kifo cha CDM ?
 
Kinachonisikitisha ni kwamba mpaka sasa ccm hawataki kutambua madhara ya kuwaita wenzao wadini,wakabila ,wanaendekeza ukanda na kila aina ya ubaguzi wanaowapandikizia wenzao.

HAKIKA hawajui kadri wanavyotangaza ndivyo inavyokuwa .Warejee mfano wa CUF ,hadi leo hii ni rahisi sana muisilamu kujiunga na chama hicho kuliko CDM ,sasa kwa bahati mbaya wameanza kuandaa chama kingine cha kusajili wakristo kirahisi kuliko waislamu.

HAKIKA vyama vinaweza kufa kirahisi lakini makundi haya wanayoyatengeneza hayatakufa kirahisi.Juhudi wanayotumia kuyajenga,kuyatambua na kuyatukuza makundi haya haitakidhi haja ya ya kuyabomoa,kwani itahitajika nguvu mara mia.

Kifupi ,mfikishieni taarifa nape kwamba atambue kuwa kukitangaza chama fulani kuwa ni cha watu fulani ndivyo anavyokisaidia chama hicho kupata watu wa namna hiyo.
 
Back
Top Bottom