Nape ajibu makombora ya Marando

Nape ajibu makombora ya Marando

Nimejaribu kufuatilia mikutano yake, na mmoja hapa jamii forums kanikonyezea niende Facebook nione comments zake kuhusu Jamii forums, nimekuja kugundua kitu kimoja muhimu kuhusu Nape Mnauye.

Kama amepitia university, alipuuzi kozi ya rhetorics ambayo kwa lugha nyepesi wanasema effective speaking, na hata kama alipitia tu shule ya msingi na sekondari, alipuuzi somo la fasihi ya kiswahili au english composition. Ningemshauri back to school apate msasa vinginevyo ataharaibu zaidi.

Kwa cheo chake cha DC na Katibu mwenezi wa CCM Kitaifa katu sikutegemea anaweza kuandika kitu kama hiki hadharani ambako kila kuku hupita kudonoa mtama. Kama hotuba zake hata kule Masasi alikokabidhiwa District Commission kama anatoa lugha kama hizi basi naona CCM wameishiwa watu wanaofaa katika uongozi.

Nisaidieni DC anaweza ongea au andika hadharani kauli zifuatazo alivyofanya Nape?
  • CHANDIMU AIBUUUU KALIPENI KODI YA MSHAHARA WA BOS WENU
  • UKINYANG"ANYWA TAULO CHUTAMA MNACHOFANYA JF AIBU.....nimefurahi mnakuja huku pia>>> HAYA ONENI AIBU YENU
  • NADHANI MNATANGAZA UBABE SASA,TOENI NA HIII
  • HAKIKA CHANDIMU NA JF WAO WAMECHANGANYIKIWA SANA....hahahaaa MPAKA WANACHONGA PICHA KUHALALISHA UONGO WAO?......DAWA YA DENI KULIPA JAMANI...KALIPIENI KODI YA BOSS WENU
  • MTOTO WACHA KUPIGA MAYOE ACHA WATU WAONE WENYEWEEE
Samahani huyu ni mtanzaniea na kijana mwenzetu tunahitaji kumsaidia kwani ni kiongozi mmojawapo katika taifa letu na watu wale wale tunaoongea na kufanyakazi pamoja kila siku.

Wazee wa CCM msaidieni kijana wenu, kuacha hivi hivi mnaumbua utamaduni wa kitanzania.
Akikua ataacha
 
Huyu jamaa anatia aibu, naona anajiandaa kuwa bosi wa TOT. Lugha za ajabu, chama kwisha. Nazidi kumkumbuka ndugu yangu Mangula.
 
Mkuu Candid Scope,

Tatizo siyo lugha, tatizo ni chama kukosa hoja za maana ambazo zitaweza kukirejeshea chama haiba ambayo imepotea mbele ya wananchi/wapiga kura.

Nape Nnauye alianza kwa kishindo sana. Wiki mbili za mwanzo tangu alipoteuliwa kuwa Katibu wa Uenezi na Itikadi, alionekana kuanza kurejesha imani kwa wananchi.

Baada ya kufungwa mdomo amekosa cha kuongea na hivyo imebidi tu aanze kuleta vioja na lugha za kejeri. Hizo lugha za kejeri ndizo zinazidi kuongeza matope na haiba ya CCM inazidi kupotea. Hata wale waliokuwa na imani japo kidogo, ndiyo watazidi kuipoteza kabisaaa.

Kwa sasa Nape Nnauye amejiweka kwenye kona mbaya kwa sababu ya mambo yafuatayo:

1. Aliahidi kwamba mafisadi wataondoka na kuwaachia CCM iliyo safi (hapa aliwalenga Lowassa, Chenge na Rostam). Hoja hiyo imeenda na maji na sasa hivi haiongelewi tena maana amegundua kwamba hilo haliwezekani.

2. Alitamba kwamba mafisadi wataandikiwa barua, na alisema baada ya Pasaka barua wangepelekewa. Mpaka leo hakuna fisadi hata mmoja aliyepewa barua.

3. Nape Nnauye alisema mafisadi wamepewa siku 90 za kujitazama then wajiondoe na wasipoondoka watafukuzwa. Katibu Mkuu (boss wa Nape) akasema hakuna cha siku tisini na wala hilo halimo kwenye majumuisho ya makubaliano ya kikao cha NEC.

Hoja ambayo ilikuwa inampa nguvu Nape ilikuwa imejengwa kwenye msingi wa hoja ya ufisadi, lakini hoja hiyo imepoteza mwelekeo kutokana na hayo matatu juu. Nape amejikuta mahali ambapo kila anachokisema kinaonekana kupingana na maboss wake (Msekwa na Mukama). Swala la barua, Msekwa alisema wao hawafanyi kazi kwa kupitia vyombo vya habari (limeisha kimya kimya). Swala la siku 90, Mukama akasema halimo kwenye tamko la NEC. Swala la mafisadi watatu ambao walikuwa wakilengwa na Nape, Mukama alisema CCM haina list ya mafisadi. But Nape alisema anawajua na kwamba wameambiwa wazi na walitajwa majina kwenye vikao, sasa kwanini Msekwa na Mukama wanaingia mitini?

Nape yuko njia panda na si ajabu anajuta kwanini alitamka hayo maneno wakati wa ile mikutano ya mwanzo ya Operation Vua Magamba. Maneno aliyoyatamka amekuta hayatekelezeki au walio na uwezo wa kuyatekeleza, hawataki au wanaogopa. Sasa inabidi aje na vijembe, vioja na lugha za kejeri, typical Mzee Makamba na Tambwe Hizza.
 
Ninachoshangaa huyu kijana si kiongozi wa juu Chamani, ni kiongozi mwandamizi aliye chini Mwenyekiti na Katibu Mkuu. Pia kuna kamati za maadili na washauri wanaoweza kumpa mwongozi kija ajaribu kuwa na lugha za mvuto wa kiuongizi, lakini hizi lugha za vibaka, mmmhhhhhhhhh, kazi ipo
 
Badala ya kuikashifu JF, nape angeweza kutumia forum hii iliyojaa wasomi wa ngazi za juu, wakati na hata wale wenye elimu ya msingi, vijana kwa wazee, wake kwa waume kufafanua sera, malengo,kujibu hoja na pia kuisafisha image ya CCM mbele ya jamii....sasa yeye anafanya kinyume chake kuikashifu JF. Juzi tu walikuja na azimio la wao kuitumia hii forum kama sehemu ya kuendeleza hoja za kukisafisha chama sasa yeye kashindwa kulifanyia kazi hilo au ameamua kufanya kinyume chake..Wake up Nape before its become too late for U!
 
Jamani,

Huyu bwana mdogo naona amekuja na staili inayoweza kumwingiza kwenye kundi moja la wazee wa taarabu tuliowazoea la mzee Yusufu Makamba na Tambwe Hiza.

Katika siku za hivi karibuni nimeona kasi ya Nnape ya kuropoka na kubwabwaja kama kasuku imeongezeka kiasi cha kutilia shaka uwezo wake katika kukiletea mabadiliko chama chake kilichompatia dhamana ya uongozi.

Sasa ameibuka na kauli yake kwamba Dr. Slaa ni fisadi! Yeye anadhani watanzania ni watoto wanaoweza kudanganywa na kauli nyepesi nyepesi hivyo!!!

Sasa nimeanza kuamini maneno ya watu waliobeza slogan ya kujivua gamba kwamba nyoka akijivua gamba anabaki kuwa nyoka. Na ndivyo ilivyo kwa CCM.

Mwanzoni, nilidhani sasa tutaanza kusikia kauli zenye mashiko kutoka kwa huo uongozi mpya wa ccm ulioingia baada ya kile kilichoitwa kujivua gamba. Nilijua nyimbo za taarabu zitakuwa zimeisha.

Kumbe wapi, kilichobadilika ni wanamuziki tu, hivi ni kweli ccm imeishiwa watu wa maana wanaoweza kuongoza chama professionally?
Mkuu African Stars ipo toka enzi hizo za kina Mbinga na Mtido wao ni Twanaga pepeta wameingi na Kutoka kina Banza,Ally choki,Muumin,Khalid Chokolaa,Badi bakule lakini Twanga ipo palepale na mtindo wao ni uleule na Radha yake ni ile ile twanga Pepeta.Vivo hivyo CCM ya Mwalimu , Mwinyi, Mkapa na hatimaye Kikwete itabaki kuwa CCM ile ile yenye maana ileile CHUKUA CHAKO MAPEMA,watabadilika viongozi lakini Sera za chama zipo kwenye maandishi kila ajae lengo ni kuchukua nchi na kutawala si kuwaletea maendeleo chanya.
 
Naomba mwanajamiiforum mmoja adondoe porojo moja tu ya Nape, tuanza kuijadili. Msiseme jumla jumla km hamjaenda shule.

:dance:
 
Wadau katika gazeti la mtanzania Nape Nauye (aka..Tambwe Hizza) amejibu makombora ya chadema na amesema kwamba Chadema wanatapatapa kwa sababu sasa amepatikana mtu makini wa kujibu hoja zao.

Pia amedai kwamba Chadema walizoea kuionea CCM kwa sababu hakukuwa na mtu makini anayejua kujibu hoja.Ameapa ataendelea kuianika Chadema mpaka pale watanzania watakapotambua ni nani fisadi kati ya CCM na Chadema.

Pia amedai kwamba mshahara wa katibu mkuu wa CCM Wilson Mukama hauzidi milioni 3 kwa sababu CCM haina mafisadi kama chadema.Amesema pia kwamba hakuwahi kuomba kujiunga chadema eti kwa sababu yeye si mchaga.

Kuna vyombo vingine vya habari Nape amedai leo atazidi kuilipua na kuimaliza kabisa Chadema.

Kama ni haya aliyoyasema basi ni ya kweli kabisa hayana hata ubishi
 
Nape kama Nape namukubali kuwa ana uwezo ukimlinganisha na vijana wengi waliopo CCM na CDM LAKINI ili kulinda heshima yake ni lazima atoe ufanunuzi kwanini HAPENDI watanzania wenzake hasa Wachagga kama alinukuniliwa vibaya aeleze umma si vizuri kijana ambae ndio kwanza ameanza kuibuka kama mpiganaji kuwa na lebel ya kibaguzi hii simu haikubaliki popote dunian hata makuburu ambao ni waasisi wa ubaguzi siku hizi wameachana na hizi siasa hatarishi
 
Mafilili, mimi naona umeathirika na ugonjwa wa ufisadiliasis ,kwahiyo na kule mwanza,mbeya ,iringa,kigoma ni vitongoji vya kaskazini!.Mmh wewe ni shabiki wakijani tu kumbe,nilifikiri unahoja.Taswira tuliyonayo sisi CDM ndo chama kitakacho mkomboa mtanzania sio hicho chenu cha wanafamilia na walafi.
 
Jamani,

Huyu bwana mdogo naona amekuja na staili inayoweza kumwingiza kwenye kundi moja la wazee wa taarabu tuliowazoea la mzee Yusufu Makamba na Tambwe Hiza.

Katika siku za hivi karibuni nimeona kasi ya Nnape ya kuropoka na kubwabwaja kama kasuku imeongezeka kiasi cha kutilia shaka uwezo wake katika kukiletea mabadiliko chama chake kilichompatia dhamana ya uongozi.

Sasa ameibuka na kauli yake kwamba Dr. Slaa ni fisadi! Yeye anadhani watanzania ni watoto wanaoweza kudanganywa na kauli nyepesi nyepesi hivyo!!!

Sasa nimeanza kuamini maneno ya watu waliobeza slogan ya kujivua gamba kwamba nyoka akijivua gamba anabaki kuwa nyoka. Na ndivyo ilivyo kwa CCM.

Mwanzoni, nilidhani sasa tutaanza kusikia kauli zenye mashiko kutoka kwa huo uongozi mpya wa ccm ulioingia baada ya kile kilichoitwa kujivua gamba. Nilijua nyimbo za taarabu zitakuwa zimeisha.

Kumbe wapi, kilichobadilika ni wanamuziki tu, hivi ni kweli ccm imeishiwa watu wa maana wanaoweza kuongoza chama professionally?

mkuu nini kazi ya katibu uenezezi wa chama chochote cha siasa?
 
kwa sababu CCM haijamkosoa Nape na ni mtu tunaemuamin kwa yote ayasemayo na kujibu hoja zenu,siku zote hoja za hovyo hujibiwa hovyo,hvyo hata Chadema hamna hoja za msing
 
Back
Top Bottom