Gosbertgoodluck
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 2,855
- 401
Jamani,
Huyu bwana mdogo naona amekuja na staili inayoweza kumwingiza kwenye kundi moja la wazee wa taarabu tuliowazoea la mzee Yusufu Makamba na Tambwe Hiza.
Katika siku za hivi karibuni nimeona kasi ya Nnape ya kuropoka na kubwabwaja kama kasuku imeongezeka kiasi cha kutilia shaka uwezo wake katika kukiletea mabadiliko chama chake kilichompatia dhamana ya uongozi.
Sasa ameibuka na kauli yake kwamba Dr. Slaa ni fisadi! Yeye anadhani watanzania ni watoto wanaoweza kudanganywa na kauli nyepesi nyepesi hivyo!!!
Sasa nimeanza kuamini maneno ya watu waliobeza slogan ya kujivua gamba kwamba nyoka akijivua gamba anabaki kuwa nyoka. Na ndivyo ilivyo kwa CCM.
Mwanzoni, nilidhani sasa tutaanza kusikia kauli zenye mashiko kutoka kwa huo uongozi mpya wa ccm ulioingia baada ya kile kilichoitwa kujivua gamba. Nilijua nyimbo za taarabu zitakuwa zimeisha.
Kumbe wapi, kilichobadilika ni wanamuziki tu, hivi ni kweli ccm imeishiwa watu wa maana wanaoweza kuongoza chama professionally?