Falsafa ya kujivua gamba inavyoiokoa CCM

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
Nianze kwa tafakuri Jadidi,je falsafa ya kujivua gamba maana yake ni kujiondoa mwenyewe au kuondolewa? turejee dhana ya CCM kujivua gamba iliyoasisiwa na ndugu Wilson Mukama,dhana hii ilikuwa na maana ya kuangalia mazingira yaliyopo,palipokosewa wapi,tujivue gamba,lakini pia Naibu Katibu Mkuu wa CCM wakati huo,Ndugu John Chiligati,nae alisema wanaotuhumiwa kwa ufisadi ndani ya CCM wajiondoe wenyewe kwenye nafasi zao ndani ya chama la sivyo watafukuzwa,alisema "wale wote wanaotuhumiwa kwenye ufisadi wa Richmond, Kagoda, Epa na Dowans hata kama chama hakina ushahidi wajiuzuru kwa kuwa Jamii imewatuhumu,

Magamba hayo yajipime na wajivue nyadhifa zao,tuliona kigogo mmoja akijiuzuru lakini magamba mengine yalikataa kujiuzuru, jibu tuliliona 2015 wanachama wa CCM waliona aibu kuvaa sare za CCM na kila aliyevaa sare za CCM alizomewa, lawama zikamwangukia mwanzilishi wa dhana ya "vua gamba" Wilson Mukama kwamba ni muoga na ameshindwa kuwawajibisha magamba yaliyong'ang'ania,hata hiyo robo ya gamba ilihoma kung'oka na mmoja aliita waandishi wa habari akang'aka na kudai falsafa ya chama kujivua gamba ni mpango wa siasa uchwara ndani ya chama zenye mlengo wa kuharibiana jina akadai yeye ni mtu mwenye heshima kubwa hivyo kumuita gamba ni kumharibia hadhi ya jina lake katika biashara zake,

Falsafa ya kuvua gamba ilipotambulishwa rasmi ndani ya Chama na kuitishwa kwa utekelezwaji wake,mtuhumiwa mkuu akaibuka yeye hakuleta unafiki mbele ya kikao cha halmashauri kuu ya Chama Taifa akainuka alivua gamba kiujasiri,hakulivua kukubali kushindwa bali yeye aliwaonyesha watanzania kuwa gamba si lake bali mwenye nalo ni kiranja mkuu angalau yeye alifanikiwa kuzima moto wa kuvua sehemu ndogo ya gamba na kuwaonyesha watanzania ukweli kwamba Chama kizima ni gamba lahitaji kuvuliwa kukazania sehemu ndogo ya gamba ni kutaka kulaghai wananchi,baada ya kushindikana dhana ya kuvua gamba 2011,Wananchi wakakosa imani na CCM, hata wale wachache waliokuwa na matumaini na chama hiki walipoteza matumaini kabisa baada ya kubaini kuwa hii ilikuwa kauli mbinu ya kisanii tu hasa kutoka kwa mwenyekiti,hii ni baada ya kuona watuhumiwa wakigoma kujiuzuru.

-Tathmini ya uchaguzi 2010 ilizaa falsafa ya Vua Gamba ndani ya CCM.

Tathmini ya mwenendo wa chama,mapendekezo mbalimbali ambayo yanaweza kukisaidia Chama kuweza kuboreka zaidi kuanzia kwenye muundo hadi utekelezaji wa makukumu ya kiutendaji uwa inapelekea kwenye hoja ya kujivua gamba au "operation vua gamba" Ripoti ya Katibu Mkuu mstaafu,Wilson Mukama iliyokuja na suluhisho la chama kujivua gamba tuliona utekelezwaji wake,April 11 mwaka 2011 ambapo yeye Wilson Mukama aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM kumrithi ndugu Yusuph Makamba ambaye yeye na sekretariati yake waliachia ngazi baada ya mtikisiki wa uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo Dkt Wilbroad Slaa aliitikisa CCM kupitia chama cha Chadema.

Upepo wa Daktari Wilbroad Slaa mwaka 2010 uliondoka na wabunge wengi na madiwani wengi na katika kura za Urais, Daktari Wilbroad Slaa alinawiri akiwa na hoja ya ufisadi uliotamalaki ndani ya CCM na Serikali yake,kazi ya tathmini ya Ndugu Wilson Mukama aliyepita Tanzania nzima kufanya tathmini,ndiyo iliyowashawishi vigogo wa CCM kumpa kazi ya ukatibu mkuu wa CCM ili atekeleze kwa vitendo yale yote yaliyokuwamo kwenye ripoti ya kamati yake.Jambo hili lilijirudia tena mwaka 2016 pale Dkt Bashiru Ally Kakurwa alipoteuliwa na CCM kutekeleza yale yaliyomo kwenye kamati yake baada ya kuzunguka Tanzania nzima kufanya tathmini ya mali za chama cha Mapinduzi,CCM.Ni dhahiri tuliona matokeo ya Ndugu Wilson Mukama na Matokeo ya Dkt Bashiru Ally Kakurwa.

Kwenye dhana ya kujivua gamba,mapendekezo ya Daktari Bashiru Ally Kakurwa yalikuwa ni kurudishwa mali za chama,Dkt Bashiru Ally aliwataka majizi yote yaliyoiba mali za CCM kuzirudisha mara moja,lakini kwa Ndugu Wilson Mukama,yeye alipendekeza kuvunja mikoa ya kichama,kwamba uongozi wa CCM uanzie ngazi ya Taifa uruke hadi kwenye Wilaya,kusiwe na uongozi wa Mkoa,pendekezo hilo lilikataliwa na wanene wa CCM,lakini Ndugu Wilson Mukama akatoa pendekezo namba mbili lenye hoja ya "CCM kujivua gamba" hoja hiyo ilichukuliwa na kuja kutolewa rasmi na Rais Jakaya Kikwete kwenye hotuba aliyoitoa Dodoma February 5 mwaka 2011 katika maadhimishi ya miaka 34 ya Chama Cha Mapinduzi, Mwenyekiti Rais Kikwete alisema chama kina miaka 34 ni lazima kijivue gamba "kuji-rebrand,repositioning na repackaging" hata hivyo ndoto hiyo iliota mbawa na watu waliomba dunia ipasuke pale vigogo walioambiwa wajivue gamba waliposimama na kumtazama Mwenyekiti,mzito mzito akapewa Katibu Mkuu,ndugu Wilson Mukama aweze kutekeleza hoja yake hiyo ya CCM kujivua gamba.

Nimalizie kwa kuipongeza CCM inapoendelea kusimamia na kutekeleza falsafa yake ya kujisafisha kwa kuwatema na kuwatenga makada wake wenye dosari za ufisadi,matumizi mabaya ya madaraka na kashfa mbalimbali,CCM kisimame imara kijisafishe na kisitetereke,kisimamie misingi ya kuundwa kwake na kirudishe maadili na uzalendo wa wanachama wake kwa taifa letu,niwakumbushe kauli ya Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani wakati CCM ikitangaza kujivua gamba,alisema "Sumu ya nyoka CCM imeenea hadi kwenye damu suluhu sio kumvua nyoka huyu CCM gamba suluhu ni kumuua ili tishio la mdudu huyu isiwadhuru Watanzania,Sumu ya nyoka CCM ni ufisadi ni ulio wazi ndani ya Chama ufisadi sio mtu mmoja mmoja ni mfumo mzima nani anaweza kuwa msafi ndani ya mfumo huu?nani atayeweza kumtupia mwenzie jiwe? hakuna aliye msafi ndani ya CCM wa kuweza kumtoa kafara mwenzie na kumuita gamba wote ni wachafu ufisadi unawahusu niseme tena kuanzia juu mpaka chini" hii ilikuwa kauli ya Mwenyekiti wa chama cha upinzani mwaka 2011.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
Back
Top Bottom