Magamba matatu ndani ya CCM

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Messages
12,586
Points
2,000

britanicca

JF-Expert Member
Joined May 20, 2015
12,586 2,000
Kila litamkwapo neno Gamba akilini kwa wengi umfikiria Mtu aliye au anyemiliki kadi ya Kijani kwa Kifupi mwanchama wa CCM aliye na ngazi serikalini,

Ilifika muda kila likitajwa neno Gamba unamuwaza Nape na kukwidana kwake na yale Majina ya Rostamu ,Lowassa na Chenge kwa kifupi AEA

Ikaanza kampeni maalumu ya Kutokomeza Magamba ndani ya chama

Kuna walio weza kutikisika lakini wengine walishindwa kutoka,

CCM ikajinasibu 2015 Kwamba mastermind wa Ugambani Lowassa kutimuliwa kaelekea UKAWA, japo ulikuwa mpango maalumu,

Katika Gazeti la Mzalendo lenye Kichwa

CCM INAWEZA “KUJIVUA GAMBA”?
ASHAKH (KIONGOZI)

20/08/2013
Ikumbukwe miaka miwili nyuma ndani ya chama tawala CCM kuliibuka kundi lenye mzozo na kundi jengine kuputia dhana na kauli mbiu ya “Kujiva Gamba”. Kauli hii ilitokana na lile kundi la viongozi waliojiona kuwa ni wasafi mbele ya kundi la viongozi walioshukiwa kujihusisha na mambo rushwa.
Uhasama ukajengeka miongoni mwao hivyo kutakiwa wale wote wanaojihusha na vitendo vya ufisadi kujchukuliwa hatua ya kuvuliwa nyadhifa za uongozi na kufukuzwa uanachama.
Kama vile unayebeba kilo 100 za usufi, dhana ya kujivua gamba ndani ya CCm haikuweza kutekelezwa. Licha ya kuonekana wepesi wake, ugumu ulikuwa umezidi na kuumiza migogo ya viongozi na wale wote walizaa dhana hii.
Leo hii fununu zimetanda kutaka utekelezaji wa dhana ile, kwa baadhi ya viongozi wa CCM Zanzibar kupendekeza baadhi ya wananchama wao wavuliwe gamba. Tofauti kidogo sababu kuu ya kuvuliwa gamba na pale mwanzo. Mara hii ni kwa wale wanachama waliotumia fursa ya kuwataka Watanzania wote washiriki na watowe maoni yao katika upatikanaji wa katiba mpya ya Tanzania.
Hii ni aibu, kwani kama mwananchi wa Tanzania bila ya kujali itikadi ya chama, kutoa maoni ni haki ya kila mtu kwa mujibu wa sheria. Vipi leo kuwe na fukutu la kufukuzwa uanachama kwasababu tu mawazo yako yako kinyume na mawazo ya wengine.
Hivi kweli CCM inaweza kujivua gamba? Vipi kwa wale wengine waliokuwa na mawazo sawa na wanachama wanaofukuzwa uanachama. Tukichukulia mifano kama vile Jaji Joseph Warioba, Dr Salim Ahmed Salim, Mzee Hassan Nassor Moyo, na wengineo wote hawa ni CCM nao hawakubaliani na Ilani ya CCM kupatikana katiba mya, jee na wao watafukuzwa uanachama?

Yataka ujasiri “Kujivua Gamba

Nikaenda Mbali nikawaza zangu kwamba ni kweli kama ingetumika nguvu sana kuvua watu magamba ingekuwa shida sana?

nimepitia Uzi mmoja hapa uliomshauri nape kuwa CCM kujivua gamba ni kuiua kabisa

Nimeona ni vyema nimpe angalizo K/mwenezi wa chama cha CCM ndugu Nape, Ni ukweli kwamba CCM ilipofikia sasa kujivua Gamba haiwezekani ila ninaloliona mbele ya chama hiki ni kifo cha mende.

Nimesoma Gazeti la mwanahalisi tuhuma nyingi wanazorushiana waheshimiwa mbalimbali wanaowania kiti 2015 kupitia chama hicho ni dalili ya kujiangamiza kabisa. Membe against Lowasa, Uswahiba wa Lowasa , Kinana, Membe, Rostam na Sita uliokuwepo awali umegeuka kuwa wadui miongani mwao.

Mara tunasikia Lowasa amedhamiria 2015, Sumaye asemi lolote lakini bado yumo, Sitta, Membe mwenyewe, Mwandosya japo yuko kimyakimya, Uwezi ukaacha kumzungumzia Kigoda maana alikuwa swahiba mkubwa wa Beni, na pengine bado anauchungu wa kudondoshwa na wengine wengi. Kinachoendelea sasa ni kupigana vijembe ndani ya Chama hicho. Nakumbuka Msekwa alipojaribu kumunyooshea kidole EL kuwa harakati zako za 2015 zitakiharibu chama, yeye alijibu kwani kuna dhambi kufanya hivyo au kuna mtu mumemuandaa ? Msekwa akanyamaza

Hayo machache tu, leo hii Nape unazungumzia kujivua gamba kwa kuondoa mafisadi ndani ya chama chako wakati jambo dogo la kukijenga chama ili kitengamae limekushinda ?

Yapo mengi yanayoonyesha chama hicho kuendelea kuwa Imara ni jambo lisilowezekanika, mtafanyeje ili CCM iaminiwe na watanzania ?
NAONA SASA WOTEEE WAMERUDI ZAO CCM

JE MAGAMBA HAYO NI YALE YALE, AU KUNA MENGINE YAMESHAONGEZEKA HUKO CCM?

waweza kujisomea pia hapa chini
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2018
Messages
4,043
Points
2,000

Kalamu1

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2018
4,043 2,000
nasema wale wakubwa wa jahazi kaka
Ukipata nafasi nzuri, jaribu pia kutuwekea 'spin' kuhusu yaliyowapata waliowezesha magamba 'kuvuliwa kwa mbinde' wakati ule; na sasa baada ya 'magamba' kuvaliwa upya. Ninawafikiria hasa Nape na Mastermind Mkuu Kinana.
Tutafurahi sana kuichangia 'spin' hiyo kuwahusu hao na mkasa wao mzima.
 
Jozi 1

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2015
Messages
6,189
Points
2,000

Jozi 1

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2015
6,189 2,000
Kila litamkwapo neno Gamba akilini kwa wengi umfikiria Mtu aliye au anyemiliki kadi ya Kijani kwa Kifupi mwanchama wa CCM aliye na ngazi serikalini,

Ilifika muda kila likitajwa neno Gamba unamuwaza Nape na kukwidana kwake na yale Majina ya Rostamu ,Lowassa na Chenge kwa kifupi AEA

Ikaanza kampeni maalumu ya Kutokomeza Magamba ndani ya chama

Kuna walio weza kutikisika lakini wengine walishindwa kutoka,

CCM ikajinasibu 2015 Kwamba mastermind wa Ugambani Lowassa kutimuliwa kaelekea UKAWA, japo ulikuwa mpango maalumu,

Katika Gazeti la Mzalendo lenye Kichwa

CCM INAWEZA “KUJIVUA GAMBA”?
ASHAKH (KIONGOZI)

20/08/2013
Ikumbukwe miaka miwili nyuma ndani ya chama tawala CCM kuliibuka kundi lenye mzozo na kundi jengine kuputia dhana na kauli mbiu ya “Kujiva Gamba”. Kauli hii ilitokana na lile kundi la viongozi waliojiona kuwa ni wasafi mbele ya kundi la viongozi walioshukiwa kujihusisha na mambo rushwa.
Uhasama ukajengeka miongoni mwao hivyo kutakiwa wale wote wanaojihusha na vitendo vya ufisadi kujchukuliwa hatua ya kuvuliwa nyadhifa za uongozi na kufukuzwa uanachama.
Kama vile unayebeba kilo 100 za usufi, dhana ya kujivua gamba ndani ya CCm haikuweza kutekelezwa. Licha ya kuonekana wepesi wake, ugumu ulikuwa umezidi na kuumiza migogo ya viongozi na wale wote walizaa dhana hii.
Leo hii fununu zimetanda kutaka utekelezaji wa dhana ile, kwa baadhi ya viongozi wa CCM Zanzibar kupendekeza baadhi ya wananchama wao wavuliwe gamba. Tofauti kidogo sababu kuu ya kuvuliwa gamba na pale mwanzo. Mara hii ni kwa wale wanachama waliotumia fursa ya kuwataka Watanzania wote washiriki na watowe maoni yao katika upatikanaji wa katiba mpya ya Tanzania.
Hii ni aibu, kwani kama mwananchi wa Tanzania bila ya kujali itikadi ya chama, kutoa maoni ni haki ya kila mtu kwa mujibu wa sheria. Vipi leo kuwe na fukutu la kufukuzwa uanachama kwasababu tu mawazo yako yako kinyume na mawazo ya wengine.
Hivi kweli CCM inaweza kujivua gamba? Vipi kwa wale wengine waliokuwa na mawazo sawa na wanachama wanaofukuzwa uanachama. Tukichukulia mifano kama vile Jaji Joseph Warioba, Dr Salim Ahmed Salim, Mzee Hassan Nassor Moyo, na wengineo wote hawa ni CCM nao hawakubaliani na Ilani ya CCM kupatikana katiba mya, jee na wao watafukuzwa uanachama?

Yataka ujasiri “Kujivua Gamba

Nikaenda Mbali nikawaza zangu kwamba ni kweli kama ingetumika nguvu sana kuvua watu magamba ingekuwa shida sana?

nimepitia Uzi mmoja hapa uliomshauri nape kuwa CCM kujivua gamba ni kuiua kabisa

NAONA SASA WOTEEE WAMERUDI ZAO CCM

JE MAGAMBA HAYO NI YALE YALE, AU KUNA MENGINE YAMESHAONGEZEKA HUKO CCM?

waweza kujisomea pia hapa chini
Kwani we hujui kuwa "ccm ni ile ile ooooh....ni ile ilee..."
 
Forum statistics

Threads 1,364,829
Members 521,026
Posts 33,329,801
Top