Naongea naye nini?

Naongea naye nini?

pia mkumbushe asijikweze na kuwaona 'walioshindwa' ni wazembe. hii ni mtego ambayo watoto ambao ni 'mfano' unawapata mara kwa mara. naambiwaga mno nyumbani na wazazi
yeye sasa anaona wenzie ndo bab kubwa...... wakiwa kwao ni TV nk, hakuna kufua, kupika, kudeki....... yeye anajiona looser, kwa hiyo hawezi kujikweza kwa wenzie
 
Thanks FP kwa michango yako. Nimepata hazina kubwa sana kwa experiences zenu mlizoshare nami.

BADILI TABIA, namtupia neno moja moja nikipata nafasi; cha kwanza nilichojifunza from him kuwa age inayoruhusiwa hapo shuleni kwao kwa form one ni 11 mpaka 13 tu, which is a huge relief to me kwani ni almost umri sawa. Hakutakuwa na a 15yrs boy in a class.

Lkn nilipata chance wakati tunatoka church kusisitiza kuhusu sala na kuchagua marafiki vizuri.
Naenda naye mdogo mdogo. Asante mwaya kwa ushauri.
Kila kitu kitakuwa sawa my dear, wala usihofu. pamoja na kukazana kutafuta hela za kumlipia ada ya kusoma shule nzuri kazana pia na kumwekea kwenye ulinzi wa Mungu
 
Kila kitu kitakuwa sawa my dear, wala usihofu. pamoja na kukazana kutafuta hela za kumlipia ada ya kusoma shule nzuri kazana pia na kumwekea kwenye ulinzi wa Mungu

Ni kweli God is everything na ni source ya all that is good. Kwa muda anajitahidi hata yeye kusali, l pray that he continue puberty isimpeleke kwingine.
 
Lol, kuna mmama mwanae akiwa mdogo sana aliona mbaba katoka toilet kwao na hajafunga zipu ya sarawili. Akakimbia kitchen akamuambia mama siri imefichuka! Mama anauliza nini akamuambia twende ukaone. Yaani till now, tumemuoza huyo kijana lastvyr na still tunamtania. Coz aliweka msamiati, inaitwa siri!
mimi wangu walikuwa wanasema TT,pichu ni teitei!ongezea hiyo BAK
 
Last edited by a moderator:
Kaunga, mbona hujasema aunt zake tukampikia visebeo? Ama watoto wa dot com hawabebi visheti?
 
Last edited by a moderator:
Kaunga, mbona hujasema aunt zake tukampikia visebeo? Ama watoto wa dot com hawabebi visheti?

Ha ha ha
Naambiwa niongeze tu monthly allowance maana wana variety ya cookies na biscuits kwenye canteen ya shule. LOL

Nakumbuka enzi zetu, visheti na vijiandazi vigumu ilikuwa mpango mzima. I miss those days kwa kweli.
 
Last edited by a moderator:
Ha ha ha
Naambiwa niongeze tu monthly allowance maana wana variety ya cookies na biscuits kwenye canteen ya shule. LOL

Nakumbuka enzi zetu, visheti na vijiandazi vigumu ilikuwa mpango mzima. I miss those days kwa kweli.
mimi hapo kwenye RED huwa sipafagilii kabisa. unamfunza mtoto kuwa na matumizi mabaya ya hela. huwa nasisitiza sana wanangu kula vyakula vya shule sababu tunavilipia pia. kuna watoto hawali kabisa vyakula vya shule, anashindia biskuti na soda kwenye duka la shule, matokeo yake anakuwa anashinda na njaa tu maana anatumia akili nyingi kusoma.
Mimi nimesoma boarding ya serikali, enzi zile chakula kilikuwa kibaya sana, lakini tulikula na hatukuumwa.
kuna siku mwanangu alikuwa 5 years, yupo day ila shule kwao tunawalipia chakula. kuna siku akaniambia mwl kasema kila ijumaa wawe wanaenda na hela ya kununua burger, kweli mwanangu anapenda sana burger, lakini nikawaza kwa nini waende na hela na wakati tunalipia chakula? nikamwuliza teacher akaniambia kuna mzazi anasema mwanaye ale burger kila ijumaa kwa hiyo anampa hela, lunch time mtu anatumwa kununua, so darasani kwao watoto wengi wamewaambia wazazi wao nao wanawapa. Nikakaa na mwanangu, nikamwambia sitakupa hela ya burger shule, utakula chakula cha shule ila kila nikipata muda nitakuwa nakupeleka kukununulia burger...... akakubali na hadithi ya burger ikaishia hapo.
 
FP l was not serious, hajasema na yuko tofauti sana na watoto wengi; anaweza kula na kuishi popote. Hiyo ya variety ya biscuit nimekuta kwenye forms za shule. Nilikuwa namtania my wifi.

Mwanangu, nikijisahau huwa hasemi mpaka mwenyewe najishtukia. Jana kanipa voucher ya voda aliyonunuliwa na bibi yake, amesema rafiki zake wengi wako shule na mimi niko naye so haoni mahitaji ya airtime.
 
Last edited by a moderator:
Wow nice thread, mamii@Kaunga plz naomba usiwaambie mods waitoe hii kitu soon nahitaji kuisoma kwa utulivu coz nina young brother he is 12 mwakani anaenda fomu1,nimekuwa nawaza kukaa naye tuzungumze kwani tuko close kweli kuna ishu hawezi kuzungumza na maza wala dingi bt kwangu hafichi kitu.nilikuwa nataka kuzungumza naye kuhusu ishu ya ushoga bt sikujua nianzie wapi japo nishawahi mdadisi nikagundua ana idea kidogo juu ya hii ishu.tatizo ni mwepesi kushawishiwa na wenzie na hilo hunipa hofu kila napomtazama so nilitaka nimpe firm ground.
 
FP l was not serious, hajasema na yuko tofauti sana na watoto wengi; anaweza kula na kuishi popote. Hiyo ya variety ya biscuit nimekuta kwenye forms za shule. Nilikuwa namtania my wifi.

Mwanangu, nikijisahau huwa hasemi mpaka mwenyewe najishtukia. Jana kanipa voucher ya voda aliyonunuliwa na bibi yake, amesema rafiki zake wengi wako shule na mimi niko naye so haoni mahitaji ya airtime.
hiyo safi sana my dear Kaunga. hawa watoto wetu tunatakiwa kuwafunza matumizi ya kila kitu kwa kiasi. kuna siku nililetewa list ndeeefuu ya mahitaji ya shule na binti. nikakaa naye nikamwambia, naomba sana katika hii list vitu ambavyo kwa haki ya Mungu havina umuhimu kwa shule, i.e. ni luxury uvikate; tulibaki na robo ya list, tukaenda shopping na wala hakununa.
 
Last edited by a moderator:
Duh Ciello kumbe wenye wasiwasi tupo wengi. Pitia huu Uzi kwa utulivu, maana hata nami nibahitaji kutulia na kuupitia sana; l was bombarded with lots of michango at per. Yaani problem shared is mostly problem solved. Karibu kuenjoy ushauri ulioenda skuli.
 
Last edited by a moderator:
hiyo safi sana my dear Kaunga. hawa watoto wetu tunatakiwa kuwafunza matumizi ya kila kitu kwa kiasi. kuna siku nililetewa list ndeeefuu ya mahitaji ya shule na binti. nikakaa naye nikamwambia, naomba sana katika hii list vitu ambavyo kwa haki ya Mungu havina umuhimu kwa shule, i.e. ni luxury uvikate; tulibaki na robo ya list, tukaenda shopping na wala hakununa.

Sasa mimi wa kwangu ni tofauti, ananionea huruma na anakuja na incomplete list. So l have to figure out nini kinahitajika, nikishindwa then ile allowance yake namwambia utanunua tulichosahau.

As a boy, anatake a role ya man of the house kiasi kwamba nafeel ananijali mimi kuliko yeye. LOL
 
Last edited by a moderator:
Ila wifi unajua bado natafakari hili toka jana. Ina maana huyu mwenetu anamiliki simu tayari? Why? Manake ba unoko wangu ningemuwekea ttcl kabisa ili nimpigie mwenyewe. Kids dont need simu jamani.
 
Hata mimi la simu nimejifikiria nikasema labda mimi ni wa zamani...

Maana kuna mambo ya kwenda na wakati...wenzake wote wana simu yeye kama hana atajiona mnyonge...

Kwa kweli sijuhi kama shule zote zinaruhusu mtoto kumiliki simu...

na sijuhi umri gani ni proper kwa mtoto kuwa na simu...

Unajua akishakuwa na simu maana yake ana access na internet...hapo ndio balaa linapoanza.


Ila wifi unajua bado natafakari hili toka jana. Ina maana huyu mwenetu anamiliki simu tayari? Why? Manake ba unoko wangu ningemuwekea ttcl kabisa ili nimpigie mwenyewe. Kids dont need simu jamani.
 
Ila wifi unajua bado natafakari hili toka jana. Ina maana huyu mwenetu anamiliki simu tayari? Why? Manake ba unoko wangu ningemuwekea ttcl kabisa ili nimpigie mwenyewe. Kids dont need simu jamani.
Hata mimi sikubaliani na mambo ya simu kwa watoto wadogo. Hata Tv huwa wanaangalia kwa ratiba maalumu. Hivi vitu. ni vizuri ila pia madhara yake ni makubwa!
 
Hata mimi la simu nimejifikiria nikasema labda mimi ni wa zamani...Maana kuna mambo ya kwenda na wakati...wenzake wote wana simu yeye kama hana atajiona mnyonge...Kwa kweli sijuhi kama shule zote zinaruhusu mtoto kumiliki simu...na sijuhi umri gani ni proper kwa mtoto kuwa na simu...Unajua akishakuwa na simu maana yake ana access na internet...hapo ndio balaa linapoanza.
Ni kweli kabisa NK... Access kwenye haya mambo inahitaji kifuatliwa with high level of PG!
 
Ila wifi unajua bado natafakari hili toka jana. Ina maana huyu mwenetu anamiliki simu tayari? Why? Manake ba unoko wangu ningemuwekea ttcl kabisa ili nimpigie mwenyewe. Kids dont need simu jamani.

Sikuona madhara ya simple Simu (nokia ya torch), ambayo akiwa Dar inabaki kwa uncle wakati yeye yuko shule; (hawaruhusiwi shuleni). Weekend inanisaidia kuwa naye karibu atleast kwa mawasiliano. It is hard as a mother kuwa mbali na mtoto, lkn texting, na kuongea husaidia kupunguza umbali.

Apart from Internet access ambayo hawezi ipata kwenye kinokia cha torch, na harmful rays ambazo anakuwa exposed say once per 2weeks madhara ya Simu kwa 10yrs boy ni yepi my wifi?
 
Hata mimi sikubaliani na mambo ya simu kwa watoto wadogo. Hata Tv huwa wanaangalia kwa ratiba maalumu. Hivi vitu. ni vizuri ila pia madhara yake ni makubwa!

Yepi Dark City? Naweza yaona kwa binti au mvulana wa miaka 14 na kuendelea lkn a 10yrs boy kumiliki nokia ya torch ambayo anaitumia weekend akienda home (coz sidhani kama kuna shule inaruhusu simu).
 
Last edited by a moderator:
mimi hapo kwenye RED huwa sipafagilii kabisa. unamfunza mtoto kuwa na matumizi mabaya ya hela. huwa nasisitiza sana wanangu kula vyakula vya shule sababu tunavilipia pia. kuna watoto hawali kabisa vyakula vya shule, anashindia biskuti na soda kwenye duka la shule, matokeo yake anakuwa anashinda na njaa tu maana anatumia akili nyingi kusoma.
Mimi nimesoma boarding ya serikali, enzi zile chakula kilikuwa kibaya sana, lakini tulikula na hatukuumwa.
kuna siku mwanangu alikuwa 5 years, yupo day ila shule kwao tunawalipia chakula. kuna siku akaniambia mwl kasema kila ijumaa wawe wanaenda na hela ya kununua burger, kweli mwanangu anapenda sana burger, lakini nikawaza kwa nini waende na hela na wakati tunalipia chakula? nikamwuliza teacher akaniambia kuna mzazi anasema mwanaye ale burger kila ijumaa kwa hiyo anampa hela, lunch time mtu anatumwa kununua, so darasani kwao watoto wengi wamewaambia wazazi wao nao wanawapa. Nikakaa na mwanangu, nikamwambia sitakupa hela ya burger shule, utakula chakula cha shule ila kila nikipata muda nitakuwa nakupeleka kukununulia burger...... akakubali na hadithi ya burger ikaishia hapo.

Kumbuka this kid goes to Feza, may be you huifaham ipo vipi? Chakula ni kizuri sana but canteen napo kuna various options as most of kids wanakuja na pocket money nzuri.. So atleast mtoto asijisikie vibaya wenzake wakinywa soda etc awe na pocket money nzuri.... I remember those days watoto wa kiarabu wanawekewa mpaka bills na mama zao wachukue wanachotaka anytime at schools na bado hao watoto wanakimbiza darasan na wengi wao wanaongoza family business baada ya varsity.... Kumpa mtoto wa sekondari pocketmoney nzuri sio kumuharib but unaaanza kumfundisha financial management mapema as wengi tulikuwa tunaseve hela tukirudi likizo tununue sneakers etc
 
Back
Top Bottom