Naongea naye nini?

Naongea naye nini?

Kabla hatujawa....mwanzoni wa kuanza kujuana(Ushakumbuka?)

Ndio maana siku ile nilo ku pm, nikakwambia nilikuwa nakuogopa kumbe hauko kihivyo mwaya!!

Nakumbuka tulikuwa tunakwaruzana lakini kukutakana, l will have to go back.
Nashukuru kuwa umenisamehe

Nina maswali nitakuuliza PM, kama hautajali!
 
Nakuelewa FP,
Kukujibu swali lako la kwanza, simu alikuwa nayo kabla ya likizo na ni kwaajili ya mawasiliano nami na ndugu zake wengine.

Angekuwa binti ningekuwa na reservation hasa akifikia hiyo age ya miaka 13 na kuendelea lakini kwa maisha ya sasa huwezi zuia kikubwa mambo ya utandawazi; cha msingi mtoto anatakiwa kujitambua na kufuata values ulizomjengea.

Vijijini watoto wanapata mimba at 15, wanakuwa na simu?

Uncle zake hawako nyumbani muda mwingi, na pia wanakuwa na mambo yao; naweza ongea naye kwa muda mfupi na very general issues, lakini mostly huwa napenda tuongee muda karibia wote ili anipe story za shule na mambo kama hayo (hiyo ndio njia pekee si tu ya kuwa naye karibu lakini pia kujua what he is thinking and doing.

Umesema wewe mwanao yuko day, it is different; nami nisingekuwa na sababu ya kumpa simu kama ningekuwa naye hapa, na ndio maana amesema mwenyewe hana mtu wa kuongea naye for the time being coz rafiki zake wako shule na mimi niko naye hapa nyumbani.

Trust me, l know how to raise my kid in my own way; kilichonitatiza ndicho nilichokileta, na ninashukuru kwa ushauri.
mimi mwanangu hayupo day, na alianza boarding tangu akiwa darasa la 5. anatumia simu yangu kuwasiliana na rafiki zake anapokuwa likizo.
Poa, all the best my dear
 
Nakumbuka tulikuwa tunakwaruzana lakini kukutakana, l will have to go back.
Nashukuru kuwa umenisamehe

Nina maswali nitakuuliza PM, kama hautajali!

Uliza tu usihofu....na usisahau ahadi ulonipa ukirudi kutoka Kigoma
 
duh umechelewa ulipaswa mpeleka mazoezi ya karate age six

The Big boss! hapo umenoa, hatutumii nguvu kumtongoza mvulana hivyo hatazitumia zaidi ya kuzitumia wakati wa kubikiriwa tu.
Suluhusho la kwanza Kaunga ni kumweleza ukweli wa mambo wewe mwenyewe au Mjombake
Au achana na boarding ingawa hata day school (Baden Powel wanafirana kama hawana akili nzuri) nazo mchezo huo upo, lakini unachelewa kuanza au mtoto kuja kukustakia na hivyo kuweza kumsaidia mapema.
​

Ma sister Pole ya dhati kabisa kwa mfadhaiko ulionao juu ya maisha ya baadaye ya mpwa wangu.

Ndimi Bazazi!
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na wewe Kongosho,mimi nakumbuka nikiwa form one likizo ya kwanza nampa mama story namwambia shule yenyewe haina hata fensi ya maana,akaniangalia akanijibu mwanangu fence is yourself ile iliyowekwa si kwa ajili yenu ili msiruke ni kwa ajili ya kuwalinda na wanyama kama mbwa vichaa nk.Nilikua nikikumbuka neno hilo tu la fence is yourself nawashangaa sana wanaoruka kwenda town for shopping.
ndio maana huwa naamini sana maneno ya mzazi au nyumbani kwa ujumla.

Kuna viunzi mtu unaviruka ujanani kwa kukumbuka neno moja tu la mzazi.

Hongera kwa kujitambua.
 
Bazazi, nashukuru ingawa l hate ur language and ur name. Bahati tu hatuchagui ndugu, lkn hiyo typical Nyamwezi language yako, sina jinsi zaidi ya kukusemea kwa Sikonge.
 
Last edited by a moderator:
Kaunga,

Pole na mawazo yaliyo kichwani. Kwa kweli hii hali inatisha sana kwa sasa maana kila ukigeuka ni Ushoga tu. Na wanazidi kuwa na nguvu sana hawa mashoga hasa miji mikubwa. Too sad. Ila ndiyo ukweli wenyewe maana duniani tumezidi sana na matokeo yake ni lazima tupungue. Zamani yalikuwepo magonjwa ya kutisha na vita ila sasa hakuna tena au yamepungua sana. Lazima tupungue, sasa nature ifanyeje? Kasheshe.

Ongea nae na ikiwezekana kama walivyo ongea wengine, tafuta WAJOMBA wamuweke kiti moto. Muonye kupenda vya dezo na hasa UNGA au Bange maana akishapenda sana na siku moja akawa hana pesa ya kulipia, basi hali itakuwa mbaya sana kwake.

Muhakikishie kuwa utakuwa tayari kuendelea kuwa mama yake bila kujali nini kimetokea. Asiwe na wasiwasi kukuambia jambo lolote mara litakapoanza.
Mfanyie na kisherehe umuone kama anachangamkia Wakamwana wako. Ukiona kimya, tafuta mchungaji....

Anyway, kwa sisi Wakristo tunasema "Kama Bwana hatailinda nyumba, wailindao wanasumbuka bure."
Bazazi, nashukuru ingawa l hate ur language and ur name. Bahati tu hatuchagui ndugu, lkn hiyo typical Nyamwezi language yako, sina jinsi zaidi ya kukusemea kwa Sikonge.
 
Last edited by a moderator:
Asante kaka yangu Sikonge kwa maneno ya busara. Umeongezea pale waliponishauri wengine.

Ana crash na mtangazaji mmoja wa Muvie TV ya Zambia, aiitwaye Lulu; so ninamshukuru Mungu kwa dalili hizo. LOL
 
Last edited by a moderator:
Yepi Dark City? Naweza yaona kwa binti au mvulana wa miaka 14 na kuendelea lkn a 10yrs boy kumiliki nokia ya torch ambayo anaitumia weekend akienda home (coz sidhani kama kuna shule inaruhusu simu).

Samahani sana Kaunga,

Nimeshindwa kuja kukujibu mapema.. hata hivyo naamini sijachelewa!

Hawa watoto wanafanya vitu vingi sana kwa kutumia simu kiasi kwamba ni vigumu hata kuelewa au kuamini pale tunapofumaniwa....Sitaki kuongelea mambo mabaya ila kuna wengine wanatumia muda kwenye mwingi kwenye mitandao ya kijamii kama vile fb badala ya kusoma. Pia wengine wanatumia muda wao mwingi kwenye games. Hilo nalo ni hatari kwa sababu wanatumia muda ambao wangekuwa wakijisomea kufanya vitu ambavyo havina tija.

Hivi majuzi, tulikuja kugundua kuwa kajukuu ketu ka 5yrs kanatumia muda mwingi kucheza games kwenye simu. Kakiona simu tu, kanakimbia nayo kwenda mahali pa peke yake na kuanza kucheza...Basi ilitubidi tukae naye na kumweleza kuwa asitumie simu ya mtu bila kuomba na hata ile ya nyumbani. Baada ya hapo alianza kuomba simu na hivi karibuni kamepunguza.

Hayo ni machache ila naamini wengine wanaweza kuwa na mifano ya aina nyingine ambayo inaweza kusabibisha distraction kwa mtoto.

Ila hoja yako kwa FP inaeleweka pia.

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
sijasema kumpa mtoto hela nyingi maana yake hatakuwa mzuri darasani.
na najua wewe si mzazi, believe me, watoto huwa ni waelewa sana, ukimpa good reason kwa nini humpi hela nyingi ya kula biskuti kila anapotaka atakuelewa, na hatajisikia vibaya. unataka kuniambia kila mtoto anayesoma Feza anapewa pocket money nono? unataka kumshindanisha mtoto wa Kaunga na watoto wa waarabu? Kaunga anasema anafanya kazi kwa bidii ili kumwandalia mwanae future nzuri, hao waarabu ndo tunapigiziana nao makelele kuwa wao ndo wameshika uchumi wa nchi yetu, hawa watu tunaweza kuwaweka pamoja?
mimi sifanyi vitu fulani kwa watoto wangu siyo sababu sina hela za kuwafanyia hayo, ila sioni sababu ya kufanya hayo. Itakuwa vizuri sana badala ya kumjazia pocket money ambayo huna uhakika kama ata-save au la, ni bora kumwongezea kiasi anachomwekea kwenye account yake, hizo una uhakika atazikuta baadae na zitakuwa msaada kwao wote wawili.
hapa dada mkubwa kaongea!
 
l hate ur language and ur name. lkn hiyo typical Nyamwezi language yako,

My Dear Kaunga nini tena kunichukia nduguyo bila kosa lolote. Tatizo la lugha linatokana na umasikini, kukulia TMK kwa Kindande ambako unafundishwa kuuita mkono "MKONO" na sio kishikio. Kwenye red umepotea kabisa.

Ndimi Bazazi!
 
Last edited by a moderator:
Great topic, Kaunga.

Here's my two cents based on my own experience:
-Ongelea umuhimu wa elimu. Mkumbushe anachoendea shule. Set high standards (top marks, great reviews from teachers).
- Mshauri achague marafiki vizuri (wasomi, wanamichezo, wenye tabia nzuri). Ajichanganya nao. Never be a loner and stand up for yourself if bullied. Kama ataonewa let him know that it is always OK to report any incident to you directly if his teachers do not take any action, or if any abuse if coming from teachers themselves. Kama mzazi unayo haki kujua kama mwanao anakuwa treated with respect na haonewi!
-Asiendekeze wasichana kwani umri wake bado mdogo. He might already begin feeling attracted to them at this point, which is very natural. Simply remind him that a time will come where he can act on his feelings, but that time is not now.

Kuhusu swala la ushoga, usijali sana. Kuna tofauti kati ya mashoga (homosexuals) na wabakaji/wanaolawiti (sexual abusers/predators). Tatizo ni sexual abusers kwani hawa si lazima wawe mashoga, kwani mashoga huendana na mashoga wenzao. Kama wengine walivyokushauri, mwambie kijana wako asikubali kushikwa nyeti zake na mtu YEYOTE. Ajilinde na asione aibu hata siku moja kuripoti kwa kiranja, matron/patron, mwalimu, na wewe pia.

Ushauri kwa wengine pia, it is never too early to speak to your child about sexual abuse. Never. Speak to your sons and daughters please. Sexual abusers can be anyone, si lazima wawe strangers. Hata ndugu mnaokaa nao manyumbani, be very careful who you let close to your children. You cannot be there to keep them safe 100% of the time, but you can give the the skills to get themselves out of a difficult situation.

My son anaenda kuanza form one, (preform one next month) boarding school he is going to be 12 next year.

As a mother namuambia nini? Nafeel kuna kitu napaswa kumwambia sijui nimwambie nini na jinsi gani.

Sijasoma boarding school O'level so sijui kunakuweje, nasikia ushoga unaanziaga huko. Bullying inanitia wasiwasi ukizingatia umri wake ni relatively Mdogo.

Nisaidieni nini cha kuongea naye.
N.B Namlea mwenyewe as a single mom.
 
Samahani sana Kaunga,

Nimeshindwa kuja kukujibu mapema.. hata hivyo naamini sijachelewa!

Hawa watoto wanafanya vitu vingi sana kwa kutumia simu kiasi kwamba ni vigumu hata kuelewa au kuamini pale tunapofumaniwa....Sitaki kuongelea mambo mabaya ila kuna wengine wanatumia muda kwenye mwingi kwenye mitandao ya kijamii kama vile fb badala ya kusoma. Pia wengine wanatumia muda wao mwingi kwenye games. Hilo nalo ni hatari kwa sababu wanatumia muda ambao wangekuwa wakijisomea kufanya vitu ambavyo havina tija.

Hivi majuzi, tulikuja kugundua kuwa kajukuu ketu ka 5yrs kanatumia muda mwingi kucheza games kwenye simu. Kakiona simu tu, kanakimbia nayo kwenda mahali pa peke yake na kuanza kucheza...Basi ilitubidi tukae naye na kumweleza kuwa asitumie simu ya mtu bila kuomba na hata ile ya nyumbani. Baada ya hapo alianza kuomba simu na hivi karibuni kamepunguza.

Hayo ni machache ila naamini wengine wanaweza kuwa na mifano ya aina nyingine ambayo inaweza kusabibisha distraction kwa mtoto.

Ila hoja yako kwa FP inaeleweka pia.

Babu DC!!
hawa watoto wetu tunawapenda sana, na kweli tunataka wawe na kila kitu ambacho tuna uwezo nacho. siyo mbaya kufanya hivyo, lakini tujiulize tunamsaidia nini mtoto kwa kumfanyia tunayomfanyia?
 
My Dear Kaunga nini tena kunichukia nduguyo bila kosa lolote. Tatizo la lugha linatokana na umasikini, kukulia TMK kwa Kindande ambako unafundishwa kuuita mkono "MKONO" na sio kishikio. Kwenye red umepotea kabisa.

Ndimi Bazazi!

Aisee, kumbe sio mnyamwezi. Nilikuona siku moja unataja mitaa ya Kikungu, Ipole sijui Kanyamsenga nikaconclude utakuwa wa huko.

Au nimekosea wanyamwezi hawana dirty language au?
 
hawa watoto wetu tunawapenda sana, na kweli tunataka wawe na kila kitu ambacho tuna uwezo nacho. siyo mbaya kufanya hivyo, lakini tujiulize tunamsaidia nini mtoto kwa kumfanyia tunayomfanyia?

Hilo ni jambo gumu sana dada yangu @FP,

Kuna wakati unamwona mzazi anavyomfanyia mwanae hata huwezi kumwelewa au kuyaamini macho yako....

Kwa mfano, mzazi kumpa pocket money ya malaki mtoto ambaye anaenda shule ya boarding inayotoa kila kitu (tena kwa viwango vya juu sana na pia inaruhusu mtoto kutembelewa na wazazi kila mwezi) hadi unajiuliza hizo pesa zote za nini....??

Hata hivyo, maelezo katoka kwa Kaunga yanaonesha kuwa situations ambazo ni fair na muhimu kwa mazingira yake.

Kitu cha muhimu ni kwa mzazi kujitahidi kumwelewa vizuri mtoto wake ili kile anachomfanyia kiwe miongoni mwa vitu ambavyo mtoto anavimudu kwa umri na uwezo wake wa kiakili.

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Duh! Thanks Kaunga for this thread, naamini na mimi nitapata kitu hapa japo wa kwangu ni she

My son anaenda kuanza form one, (preform one next month) boarding school he is going to be 12 next year.

As a mother namuambia nini? Nafeel kuna kitu napaswa kumwambia sijui nimwambie nini na jinsi gani.

Sijasoma boarding school O'level so sijui kunakuweje, nasikia ushoga unaanziaga huko. Bullying inanitia wasiwasi ukizingatia umri wake ni relatively Mdogo.

Nisaidieni nini cha kuongea naye.
N.B Namlea mwenyewe as a single mom.
 
Hilo ni jambo gumu sana dada yangu @FP,

Kuna wakati unamwona mzazi anavyomfanyia mwanae hata huwezi kumwelewa au kuyaamini macho yako....

Kwa mfano, mzazi kumpa pocket money ya malaki mtoto ambaye anaenda shule ya boarding inayotoa kila kitu (tena kwa viwango vya juu sana na pia inaruhusu mtoto kutembelewa na wazazi kila mwezi) hadi unajiuliza hizo pesa zote za nini....??

Hata hivyo, maelezo katoka kwa Kaunga yanaonesha kuwa situations ambazo ni fair na muhimu kwa mazingira yake.

Kitu cha muhimu ni kwa mzazi kujitahidi kumwelewa vizuri mtoto wake ili kile anachomfanyia kiwe miongoni mwa vitu ambavyo mtoto anavimudu kwa umri na uwezo wake wa kiakili.

Babu DC!!
Babu, mimi nilisema haya nikakumbushwa tena kwa sauti kubwa kabisa kuwa mtoto anaenda Feza, siyo shule tu ya uchochoroni. kule wanasoma watoto wa mabilionea kwa hiyo na mtoto wa Kaunga naye anatakiwa kwenda kama milionea. Well, tupo tofauti. mimi siwezi kujiita ni wa level ya chini, lakini kila ninapompeleka mwanangu shule (boarding) huwa namwuliza matron minimum amount ya kumwachia mtoto as a pocket money, najua matron angeniambia minimum ni 2M nisingeshindwa kutoa, lakini akiniambia ni elfu 20 huwa naacha elfu 20.
Huyu mtoto yupo shule..... atakula, atalala, ataingia darasani............. akiumwa atatibiwa ikishindikana nitapigiwa simu, kwa nini nimwachie laki? ataifanyia nini? si bora hiyo laki nimwekee kwa account yake ataikuta siku atakapoihitaji?
Pamoja na mzazi kumwelewa mtoto, kitu muhimu pia ni kukaa na mtoto wako na kumwelewesha. kama wazazi hatupaswi kudictate mambo, sawa, lakini tunapaswa kukaa na watoto na kuwaambia hali halisi. na huwa wanaelewa wala hawana shida
 
Last edited by a moderator:
This great my dada, umenena ukweli mtupu, hata mimi sion sababu ya kumwachia mtoto mihela kibao wakati yuko boarding na shule inaprovide kila kitu, kwa mahitaji yake madogomadgo ndo unaweza kuacha pesa kidogo kwa matron

Back
Top Bottom