Jinsi pre-form one inavyoharibu kizazi cha leo

Its_grey

New Member
Jul 22, 2021
3
2
Leo ni tarehe 30 Septemba kuna baadhi ya watoto wametimiza wiki mbili kwenye shule zao ambazo walijiunga kwa ajili ya pre form one inawezekana kuna ukakasi kwenye kichwa cha habari lakini endelea nami nikufafanulie ni kwa namna gani pre form zinaharibu kizazi cha leo

1a) Katika kizazi hiki asilimia kubwa hasa shule za private ni boarding oriented ivo kabla ya katazo la mwaka huu yakuwa wanafunzi wanaoruhusiwa kukaa boarding ni kwanzia darasa la tano asilimia kubwa ya wanafunzi wa private walikua ni wanafunzi wa bweni. Turudi kwenye mada husika

Kwa nini preform one zinachangia kwenye ushoga maradhi na umaskini

1b). Neo colonialism(ukoloni mambo sasa) Mzungu akitaka kutimiza azma yake kwa karne hii hakushikii tena bunduku bali anakutengemezea mfumo ambao kwa sisi wa Africa ni ngumu kuugunduaa lakini ni mfumo ambao utaua FIKRA NA TAMADUNI ZETU BILA YA SISI KUFAHAMU AU KUTAMBUA .Nafahamu utajiuliza linahusina vepe na hii mada twende taratibu utaelewa

1c). Mwanzo tuliongelea shule za boarding na private sasa tutaongelea day schools yaani shule za kutwa .leo hii mtoto anaesoma kutwa anaondoka nyumbani kabla ya mzazi hata kwenda kazini wakirud nyumban ni saa kumi na mbili jioni wanakutana na either mzazi aliyechoshwa na kazi au mzazi bado hajarud kutoka kazini lakini pia wao wenyewe wakirud ni homework za kutosha maanake there is no room for (parent -child interaction ) yaani hakuna nafasi ya mzazi kufahamu yanayomsibu au kuendelea katika maisha ya mwanae yes utasema kuna Jumamosi na jumapili asilimia kubwa ya wazazi bado hutumia jumamosi kama siku yao ya kazi na wanabaki na Jumapili ambapo ni maandalizi ya jumatatu (kmmm maanake kuna nafasi finyu sana ya mzazi kuzungumza na mwanae

SASA KWA JINSI GANI PREFORM ONE INACHANGIA KWENYE MAMBO HAPO JUU

2a) Amini kwamba baada ya kumaliza elimu ya msingi meaning la saba huo ndio mda pekee amabao mzazi anapata nafasi ya kumchunguza tabia mwanae aliyekua anatoka asubuhi na kurudi jioni au ambae amekaa bweni kwa miaka yote saba yaani ataweza kufanya behavior Analysis maana ni muda wa zaidi ya miezi mitatu ya kuishi na mtoto kabla ya kwenda kuendelea na elimu ya sekondari (Mwanzo mzazi akirud kutoka kazini ni alikua anamkuta mtoto yupo bize na ma Homework lakini katika kipind hiki mtoto yupo huru ivo mzazi anapata mda wa kumdadisi mtoto wake na hata kupitia wale wanaoshinda nae nyumbani japo binadamu hatuaminiki)

2a) Lakini pia ni katika kipind hiki mzazi anapata wasaa wakuongea na mwanae kuhusu malezi na mambo mbalimbali ya kidunia yapi yakuepuka na yapi yakuyakumbatia Nahisi ni kipind kizur sana kwani mtoto atapewa nasaha kabla ya kwenda sekondari ambapo uko ndipo kuna shule za (JINSIA MOJA) ndo muda muafaka kwa maongezi baina ya mtoto na mzazi ndio kipind cha kukemeeeaa ushoga na kama mzazi umechunguza mtotoo na kumkuta na chembe chembe ya izo tabia basii ndo muda muafaka wa kujaribu kumrudisha kwenye njia Sahihi kabla ya kwenda tena kuchanganyika na vijana wenzake TRUST ME PRE FORM ONE IS THE RIGHT TIME TO ANALYSE BEHAVIORS AND SHAPE A CHILD FROM HIS OR HER PRIMARY SOCIETY

--- UKIANGALIA KWA A BIGGER PICTURE PRE FORM ONE INAMNYIMA MZAZI FURSA HII YA KUKAA NA MTOTO NA KUMREKEBISHA NA KUMPA WASAHA KUHUSU MAISHA HASAHASA IZI TABIA ZA USHOGA ZINAZOENDELEA NA KUKUA KWA KASI LAKINi
PIA MAISHA KWA UJUMLA WAKE

---- KWANINI NIMEINVOLEVE SERIKALI NIAMINI UKISKILIZA VIONGOZI WOTE WANAOKEMEA IZI TABIA (USHOGA NA NYINGINEZO) UTAGUNDUA WANANZA KUWAHASA WAZAZI KUKAA NA FAMIILIA ZAO NA KULEA NA KUWAFUNDISHA JINSI MILA NA TAMADUNI ZETU ZILIVOKINYUME NA HAYA MAMBO YA KILEO HIVO NI SERIKALI ILIPASWA KULIONA HILI MAPEMA ILI KUKEMEA IZI PROGRAMM ZA PRE FORM ONA NA KUTOA DIRISHA KWA MALEZI YA KARIBU KATIKA WAZAZI NA WATOTO WAO IVO NI JUKUMU LAO BASI KAMA HAWALIONI HILI LAZMA TUWAKUMBUSHE KWA KUWALAUMU NA KUTAKA WACHUKUE HATUA


3a) Nimeongelea maradhi kwenye subject nikimaanisha magonjwaa utajiuliza PRE FORM ONE NA MAGONJWA YANAUHUSIANO GANI ??KARIBU NIKUONESHE USICHOKIONA

3b) Sina takwimu za kutosha lakini kwa sasa hakuna magonjwa yanaongoza kwa vifo kama non communicable diseases yaani magonjwa yasiyoambukizwa kama vile PRESSURE KISUKARI MAGONJWA YA MOYO NK)


LEO ASILIMIA KUBWA YA WATOTO WANAOMALIZA DARASA LA SABA HAWAJUI KUANDAA CHAKULA CHAO WENYEWE NIKIMAANISHA*** KUPIKA*** YAANI HAWAJUI KUPIKA maanake miaka kumi+ plus tutakua na kizazi cha free delivery na Junk food mEANING tutakua na idadi kubwa ya watu amabao wanasumbuliwa na pressure na maradhi ya moyo na mengine yatokanayo na poor living life style HASA JUNK FOOD CONSUMERS huwezi kuliona hiliii lakini trust me its COMING chakula unachoandaa na kupika mwenyewe si sawa na unachopikiwa na kuandaliwa na mtu mwengine

LAKINI KAMA KIPINDI ICHI CHA MIEZI MITATU MTOTO ANGEKAA NYUMBANI MAANAKE NDIO MUDA MUAFAKA WA KUJIFUNZA KUJIHUDUMIA NA KUJIPIKIA NA LABDA SIO KWA KIASI KIKUBWA SANA INAWEZA KUSAIDIA ILA KUNA NAMNA TUNGEWEZA KUOKOA KIZAZI KIJACHO NA JUNK FOOD IVO KUPUMGUZA MARADHI YATOKANAYO NA MLO MBAYA (WESTERN COUNTRIES WENGI WA WANANCHI WAO WANASUMBULIWA NA HAYA MARADHI YASIOAMBUKIZWA KUTOKANA NA POOR LIFE STYLE HASA JUNK FOOD CONSUMING WENZETU HAWAFI MAANA WANAMATIBABU BORA ILA CHA MOTO WANAKIONA TRUST ME TUSIPOWALISHA WANETU VILE WE PREPARE OUR FOOD SIJUI LAKINI NAHISI HATUTAKUA TUNAELEKEA PAZURI

INAWEZEKANA IKAONEKANA SIO POINT YA MUHIMU ILA AMINI KWAMBA SMALL LITTLE THINGS MATTER NA HILI PIA TULIANGALIE KWA JICHO LA TOFAUTI


4A) MAYBE KWA KUENDA PRE FORM ONE HAWATAPATA MDA WA KUJICHANGANYA NA MAKUNDI MABAYA MTAANI NI KWELI KABISA NA INAWEZA KUA NA FAIDA SANA LAKINI LEO MZAZI UKIMPA MWANAO KAZI ZA KUJISHUHURISHA NAZO NYUMBANI NAAMINI HATOPATA MDA WA KUZURURA TENA NDO MDA UNAWEZA UKAMPA MWANAO VITAVBU VILE VYA LIFE PRINCIPLE and COACHING AKASOMA KAMA VILE

:::----THINK BIG AND GROW RICH
:::-----POWER OF POSITIVE THINKING
::::-----GIFTED HANDS

NA UKAMJENGA MWANAO KISAIKOLOJIA NA AKAYAAONA MAISHA KATIKA PICHA YA TOFAUTI SANA AKIWA MDOGO

TUNAWEZA KUWATUMIA KINA JOEL NANAUKA wakawa na semina maalumu kwa ajili ya watoto waliomaliza primary ili kuwaimarisha mitazamo yao mbalimbali
NA WAKATI HUO HUO WAKAPUMZIKA UKU WANAJIFUNZA BILA STRESS TENA TUKAWA NA SEMINAR NA PROGRAMM MAALUMU ZA JINSI GANI WANAWEZA KUJIMANAGE KUJIAJIRI HUKO MBELENI BILA KUTEGEMEA SERIKALI AU WALICHOKISOMEA IMAGINE UMETENGENEZA FOUNDATION KIPIND ICHI AMEMALIZA LA SABA MEANING KITASTCK NA ATAKIDIGEST KWA MIAKA YOTE IYO MPAKA AMALIZA SHULE AKITOKA HAPO ANAWEZA AKAANZA KUPAMBANA MWENYEWE MDO MDO BILA YA KUSUBIRIA SANDUKU LA AJIRA

SERIKALI NDIO CHOMBO PEKEE KINAWEZA KIKAZUIA IZI PRE FORM ONE NA KUWAPA ROOM WATOTO KUPUMZIKA NA PIA WAZAZI KUKAA NA WATOTO NA KUWAJENGA KATIKA TAMADUNI NA MAISHA YETU YA KIA AFRICA NA KUWAPA MADINI KUHUSU MAISHA LAKINI KUANDAA PROGRAM ZA KUWAJENGA WATOTO HAWA KIFIKRA NA KIMTAZAMO

TRUST ME PREFORM ONE INAFAIDA LAKIN HASARA NI KUBWA ZAIDI NIIISHIE HAPO KWA LEO
 
Tayari wanafunzi wapo hostel za pre form one wanafundishwa, haijulikani wanafundishwa nini na walimu wao ni kweli wana mafunzo ya ualimu au wameokotezwa mitaani? Watoto wamehitimu juzi tu wamekimbizwa pre form one. Januari wanatakiwa waende form one kama watafaulu mitihani yao ya elimu ya msingi. Mtoto ataenda sekondari kachoka akili haitakuwa na uwezo wa kupokea maarifa mapya. Hivi hizo pre form one zinakaguliwa na wakaguzi wa elimu?
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Tayari wanafunzi wapo hostel za pre form one wanafundishwa, haijulikani wanafundishwa nini na walimu wao ni kweli wana mafunzo ya ualimu au wameokotezwa mitaani? Watoto wamehitimu juzi tu wamekimbizwa pre form one. Januari wanatakiwa waende form one kama watafaulu mitihani yao ya elimu ya msingi. Mtoto ataenda sekondari kachoka akili haitakuwa na uwezo wa kupokea maarifa mapya. Hivi hizo pre form one zinakaguliwa na wakaguzi wa elimu?
Ikifika muda wa wanafunzi kumaliza elimu ya msingi.Mimi huwa naona ndio kipindi cha shule binafsi kuchuma pesa ,za interview na pre form one.
Mimi watoto wangu huwa hawaendi hizo pre form.Ni muda wao wa kula,kupumzika,kucheza na kunisaidia kazi hapa nyumbani.Hata kama nikiwa na dada wakazi nampa mapumziko wao kila anajua ratiba ya kazi zake.
Mpaka january wanaenda shule ya upili.
Yaani mimi ni mtata sana hata wakiwa shule ile habari ya sijui masomo ya ziada kipindi cha likizo,mimi watoto wangu huwa hawaendi shule na huwa nawaambia walimu watoto wanahitaji kupumzika na kunisaidia kazi ndogo ndogo za nyumbani.

Yaani si upendi huu ujinga wa pre form one au tuition kipindi cha likizo.
Kama mtoto hajaelewa masomo kwa miezi 3 au 4 ndio ataelewa huo mwezi mmoja?
Pravite school wakati mwengine zinabuluza sana wazazi na wanafunzi.

Mbona shule za umma hazina huo mjinga wa pre form one au tuition.
 
Government nao wameanza huo mchezo.

Kuna member ametuma barua inayoelekeza watoto kuandikishwa pre form mkoa fulani hapa Tz!!!!!!!
 
Back
Top Bottom