...Lakini hakuwahi kutamka nyo wala nywe, tokea alipoondoka Dodoma, 1995
Kwa mara ya kwanza naenda kwenye rekodi kumtetea Kikwete.
Nilipata bahati ya kukutana na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Jakaya Kikwete, New York, wiki chache kabla CCM haijaenda Dodoma kuchagua tiketi.
Baada ya mkutano wa Mkapa na Watanzania New York kuisha, Muungwana akabaki ukumbini anasogoa sogoa, unajua tena watu wa Chalinze walivyo Watu wa Watu.
Nikamuuliza, Musee, utagombea Urais?
Musee akanijibu, "sijaamua kama nitagombea."
Nikasema yes! Mwanasiasa tunae! (mpaka kampeni zilipoanza siku moja akachemsha, akadhihaki uniform za Polisi, nikamwona huyu nae mchovu.)
Na wote tunajua Musee aliaanza kukaa mkao wa kula Urais toka 1994 alipo gandisha "vijisenti" vya marehemu Mpwani mwenzie, Kighoma Malima.
Kwa jibu hilo la Kikwete, nadhani alikuwa mjanja kuliko Zitto, inapokuja kwenye kujibu maswali ya Kisiasa Siasa.