Hizo siasa za zamani za kuogopa kuonesha ambition yako. Urais siyo ufalme ambao mtu anaogopa kusema anautaka. Alichofanya Zitto ni kujisababishia standard ya pekee na kuangaliwa na watu kwa ukaribu zaidi. Amejiweka ili achunguzwe na kupimwa. Haya mambo ya kudanganya ati watu hawautaki Urais lakini zikitolewa fomu wanakuwa wa kwanza kuchukua tena kwa mbwembwe yamepitwa na wakati.
Kama kuna mtu anafikiria kuwa Rais mwakani na ajulikane hivyo. Kinachonishangaza ni kuwa ilipoandikwa taarifa ya gazeti la Raia Mwema wiki chache zilizopita na watu waliojipanga Urais hakuna mtu aliyesema neno. Wao wenyewe hakuna aliyekanusha kuwa si kweli wanautaka Urais. Soma
HAPA
Kama kuonesha nia ya kuutaka Urais ni kosa kubwa na vibaya watu kujua unautaka Urais mbona leo tuna Rais ambaye alijulikana ana utaka? Au kwa vile kasema Zitto kwa vile tunamjua na ni bwana mdogo na kama utani tunamuita "kijana" (kweli ni kijana lakini imetumika with contempt) basi hastahili kusema nia yake?
Urais ni nafasi ya kuwatumikia wananchi wenzako na Taifa lako na hakuna aibu wala kumfanya awe duni ati kwa sababu ametamka kuwa wakati ukifika angependa kufanya hivyo. Tuje na chuki nyingine lakini hizi za kwa vile Zitto kasema lililomoyoni mwake hazina msingi, kwani kuna baadhi ya watu hapa Zitto hawezi kusema lolote zuri, hawezi kufanya lolote jema, na hata kama ana mawazo yoyote basi asiyatoe kwa vile anaweza "kuchemsha" na kuwatibua wataalamu wa JF!
Kwa hili ni ninyi mmechemsha, leteni hoja nyingine, kijana ana haki zote kama Mtanzania yeyote na kama atakuwa na sifa zote za kuwa Rais basi hakuna kitakachomzuia..! and he'll have my full support if he wants to! Na hilo applies to anybody else who would dare to declare his intention na tutaangalia rekodi yake.
Binafsi nampongeza Mhe. Zitto kwa kusema alilonalo, na hivyo kutupa nafasi ya kumuangalia na kumsaidia asianze kufungwa fungwa na mafisadi, na hivyo amejiweka mwenyewe kwenye chekecheo la wakosoaji na tutampima na kumjaribu kama kwa moto na akipita salama itakuwa fahari kumuona akiapishwa kuwa Rais wa Jamhuri yetu! Yes I said it!