Naona kijana anaanza kuchemka sasa!

Basi be informed kuwa Zitto ametamka kuwa 2010 hagombei tena ubunge. Ndio maana nasema sasa hivi tusimshabikie wala kusema kachemka, tungoje kuona strategy aliyonayo.

Good for him, lkn kutokugombea ubunge 2010 hakujeopardize ndoto yake ya kuja kuwa Rais one day, some days!
 
Pole sana Zitto , umesema kweli yako na hata nia na ndoto zako umesakamwa mno .Sijajua hasa kina waumiza watu ukisha tangaza habari kama hii .Jamani Tanzania inabadilika na watu lazima wasema kwa uwazi wanayo yataka .Ugumu ni kwa CCM kudhani wao pekee wanaweza kuitawala Tanzania na si kuiongoza ndiyo ngoma nzito hapa .Njoo utuleze bwana Zitto kama haya ni maneno yako ama magazeti yameamua kukusemea maana nao hawa kawii
 
Kwa hiyo ameanza kampeni siyo? Ajiangalie vizuri,jimbo lake ni miongoni mwa majimbo yatakayogawanywa kama mambo hayatabadilika,lile eneo la wapiga kura wazuri limepewa jimbo jipya Uvinza na kile kipande anachotoka yeye kimepelekwa upande wa mjini zaidi. Kwa hiyo CCm walianza mapema kummaliza na sasa kahitimisha mwenyewe.
 
Sasa kabla ya CCM huko huko CHADEMA kuna loose cannon Chacha Wangwe naye kashasema anataka kuwania urais, na Freeman Mbowe je?

Slaa alitoa a classic response na kwa maoni yangu, at least from CHADEMA, ndiye aliyeonyesha maturity na track record ya kukaribia kufikiriwa kuwa mgombea urais. Actually Slaa amefanya kazi kubwa kuliko hata Mbowe judging from the records available to the public.

Socrates alisema, wanaotaka urais hawauwezi, wanaouweza hawautaki.Tumeshaumwa na nyoka kwa muungwana, we have to be very careful.
 
Hata hivyo naona huu ni mwanzo mzuri kwani angalau tunaweza kujadiliana kama kuwaficha wananchi nia yako ya kuwaongoza ni jambo zuri au baya. NI wazi ukiwa mbinafsi na ambaye unautaka uongozi kwa ajili yako mwenyewe ni vizuri kuficha for you are the center of your own political universe, lakini kama unataka support ya wananchi na wale unaotaka kuwaongoza, kuna vitu havina msingi wa kuvificha.

Putin alisema democracy yao ni ya ki Russia....na sisi tunayo demokrasia ya Tanzania...Zitto amekuwa mkweli hajafuata yanayoandikwa kwenye vitabu ambavyo vijana wetu wasomavyo katika masomo yao ya Political Science...je ni dhambi kuwa mkweli?
 
Kama alivyosema Kitila, si dhambi, lakini si practical.

Huwezi kuwa na a locally bred politics mpaka uwe na a locally bred economy.

Kumuiga Putin ni kuiga tembo kunya, ashakum si matusi utapasuka msamba.
 
Kachemsha kweli.

Kutokukomaa kisiasa, au kuwa katika mfumo ambao haujakomaa kisiasa.

Mbunge huwezi kusema una ndoto za Urais. Tunajua karibu kila kiongozi ana ndoto za Uongozi wa juu zaidi ya alio nao, lakini ukitamka wazi wazi utaambiwa ina maana wewe hu focus kwenye kazi yako ya sasa hivi, ila kila unachofanya ni kupalilia njia ya kwenda Ikulu.

tuache ulimbukeni,kutokusema matakwa yetu ni jambo linalolifanya taifa hili lisisonge mbele. Kwani kuna jambo gani gumu lenye kuhitaji kuwa Rais wa Tanzania ambalo Zitto hana, kama waliopo ni hawa wasioweza hata kufanya maamuzi ya kuwafukuza mawaziri waliowateua wao wenyewe kwa nini zitto asitamani kuwa rais?
 
Sasa kabla ya CCM huko huko CHADEMA kuna loose cannon Chacha Wangwe naye kashasema anataka kuwania urais, na Freeman Mbowe je?

Slaa alitoa a classic response na kwa maoni yangu, at least from CHADEMA, ndiye aliyeonyesha maturity na track record ya kukaribia kufikiriwa kuwa mgombea urais. Actually Slaa amefanya kazi kubwa kuliko hata Mbowe judging from the records available to the public.

Socrates alisema, wanaotaka urais hawauwezi, wanaouweza hawautaki.Tumeshaumwa na nyoka kwa muungwana, we have to be very careful.

Hata mimi nina wazia kugombea Urais maana ni haki yangu kama Mtanzania nakwa mujibu wa Katiba kwa Umri na shule ninayo .je mtanilaani ? Ali Karume katangaza mapema kwa nini alaaniwe na kasema ukweli wake .Mawazo mgando yanawamaliza nyie vijana .
 
Kama alivyosema Kitila, si dhambi, lakini si practical.

Huwezi kuwa na a locally bred politics mpaka uwe na a locally bred economy.

Kumuiga Putin ni kuiga tembo kunya, ashakum si matusi utapasuka msamba
.

swadakta !........
 
Hata mimi nina wazia kugombea Urais maana ni haki yangu kama Mtanzania nakwa mujibu wa Katiba kwa Umri na shule ninayo .je mtanilaani ? Ali Karume katangaza mapema kwa nini alaaniwe na kasema ukweli wake .Mawazo mgando yanawamaliza nyie vijana .

wewe kwa kufuata mkumbo tu, hujambo ! (unauweza sana huo mchezo wa, "me too"!)
 
Kada siku nyingi sijatia timu hapa na wewe ukawapo,ila Zitto namfahamu,mwacheni kijana wa watu..kila mtu ana maono yake

sawa ! Nimekusikia mzee....i wont go against the guy! (tatizo wewe unajificha sana huonekani humu siku hizi, lol)!
 
Pole sana Zitto , umesema kweli yako na hata nia na ndoto zako umesakamwa mno .Sijajua hasa kina waumiza watu ukisha tangaza habari kama hii .Jamani Tanzania inabadilika na watu lazima wasema kwa uwazi wanayo yataka .Ugumu ni kwa CCM kudhani wao pekee wanaweza kuitawala Tanzania na si kuiongoza ndiyo ngoma nzito hapa .Njoo utuleze bwana Zitto kama haya ni maneno yako ama magazeti yameamua kukusemea maana nao hawa kawii

tatizo lako ndio hilo, umekuwa paranoid na ccm kiasi kwamba huwezi kuongea kitu bila kutaja ccm ! hii habari inahusiana zitto kusema alichosema, na wala hakuambiwa aseme na ccm ! wewe unadandia tu! Leo zitto kasema hayo, unasema pengine magazeti yamekosea, eehh angekuwa jamaa mwingine toka ile kambi inayokufanya uwe na paranoia ungesema wanafikiria ulaji tu ehh ?.... mawazo yako ni ya kifisadi, hayo maneno zitto kasema na hakulazimishwa aseme !
 
Kada kweli kwenye hii forum unaweza kusema mimi ni mtu wa mkumbo ? Ama kweli uko kazini wewe .Well turudie mada si dhambi Zitto kuwazia Urais ni haki yake sasa kuweza ama kutokuweza ni jambo jingine .
 
Sasa kabla ya CCM huko huko CHADEMA kuna loose cannon Chacha Wangwe naye kashasema anataka kuwania urais, na Freeman Mbowe je?

Slaa alitoa a classic response na kwa maoni yangu, at least from CHADEMA, ndiye aliyeonyesha maturity na track record ya kukaribia kufikiriwa kuwa mgombea urais. Actually Slaa amefanya kazi kubwa kuliko hata Mbowe judging from the records available to the public.

Socrates alisema, wanaotaka urais hawauwezi, wanaouweza hawautaki.Tumeshaumwa na nyoka kwa muungwana, we have to be very careful
.

kibanda kinawaka ndani kwa ndani, maana NGO yao sasa hivi kila mtu ana eye on the urais.... tutafika kweli ?? slaa akigombea nitamuunga mkono, but not Mbowe not even in a million years to come ! na Mnyika nae anataka ubunge jimbo la ubungo ili apewe uPM na pia anataka kuwa kiongozi wa bunge la vijana taifa ambalo amekuwa akilipigia debe kwa muda wa miaka isiyopungua 8 hadi hivi sasa, tuna viongozi hapa kweli ??!! mpo hapo ??
 
Mimi nafikiri kila mtu ana haki ya kutaka kuwa yeyote katika nchi yetu, ikiwemo urais. Zitto pia ana haki ya kuutaka urais wa nchi yetu au hata Ukatibu Mkuu wa Umoja wa mataifa, mpaka hapo hakuna shida wala mushekeli. Kwamba anaweza au la hilo ni jukumu la wapiga kura kuamua.

Je amefanya a strategic mistake kuweka intentions zake wazi tena mapema namna hii, it is highly debatable.

Mambo mawili muhimu ya kuzingatia kwa mwanasiasa. Kwanza, mwanasiasa hujengwa na kubomolewa kwa maneno yake. Pili, wanasiasa wengi strategic wanazingatia sana kanuni na 3 na 4 za political strategist maarufu duniani anayeitwa Robert Greene. Inasemekana wanasiasa wengi maarufu duniani wanatembea na kitabu chake hiki popote waendapo, kinaitwa "48 laws of power".

Nazinukuu hizi kanuni namba 3 na 4 hapa chini.

Law 3: Conceal your intentions. Keep people off- balance and in the dark by never revealing the purpose behind your actions. If they have no clue what you are up to, they cannot prepare a defence.

Law 4: Always say less than necessary. When you are trying to impress people with words, the more you say, the more common you appear, and the less in control. Even if you are saying something banal, it will seem original if you make it vague, open- ended, and sphinxlike. Powerful people impress and intimidate by saying less. The more you say, the more likely you are to say somthing foolish.

So, kwangu mimi alichosema Zitto sio ujinga lakini pia sio ujanja katika siasa!

(Kisura anasoma between the lines), bwana Zitto eeeh, you have self declared (not in so many words) contender for a President from your very own party. Huyu ni mmoja wao! Anafanya alichokieleza hapo juu.
 
tuache ulimbukeni,kutokusema matakwa yetu ni jambo linalolifanya taifa hili lisisonge mbele...

Kigarama uko sahihi.

Katika jamii changa Kisiasa kama Tanzania tu.

Hii forum inanisaidia sana kuijua zaidi na zaidi jamii ya Watu wa nchi yangu. Ningekuwa sijawahi kuja hapa JF ningeweza kusimama hadharani Bongo nikasema "Zitto kachemsha" halafu mimi ndio nikaonekana limbukeni.

Sasa hivi najua kwamba, aaaanha, kumbe Kibongo Bongo Zitto hajachemsha!

Kitu kimoja lakini. Madaktari wa Saikolojia wanasema kamba, wale wagonjwa wa Mirembe wanaojaribu kupita kwenye milango iliyochorwa ukutani wanatuona sisi tuliowafungia mle ndio tuna matatizo. Na sisi tunawaona wao ndio wana matatizo inabidi tuwafungie mle. Sasa, mimi na wewe si wagonjwa na hatuko Mirembe. Lakini nadharia ya Madaktari wa Mirembe inatusaidia kuelewa kwamba inawezekana mimi na wewe wote tuko sawa.

Kwamba, katika aina ya ulimwengu wa mawazo ninayoishi mimi, Zitto kachemsha. Katika mtazamo wa jamii unayoishi wewe, mimi ni limbukeni. Nakubali 100%
 
Kada kweli kwenye hii forum unaweza kusema mimi ni mtu wa mkumbo ? Ama kweli uko kazini wewe .Well turudie mada si dhambi Zitto kuwazia Urais ni haki yake sasa kuweza ama kutokuweza ni jambo jingine .

Lunyungu wewe ni mtu mmoja niliyekuwa nikiwaamini sana humu kwa info na pia nilikuamini kwa kutegemea mawazo yako mwenyewe bila kupelekeshwa na watu wachache humu..... Kuna watu kazi yao ni "kwenda against na kitu chochote kile kizuri" yaani kwa kifupi hiyo ni destiny yao, na wewe hukuwa mmoja wa hao watu, lakini ghafla bin vuu nikashangaa kwamba na wewe umo ndani ya huo mkumbo, kwa kutetea vitu visivyopaswa kutetewa, lakini hayo ni maoni yako tu so am not sweating ! On the other hand, kuna "damage control" ambayo watu wanafanya na ghafla nimeshangaa wewe umo ndani, kwa kweli hili limenifanya nipoteze imani na wewe....

Anyway kurudi kwenye mada, ni kwamba unadhani zitto kama zitto amefanya jambo zuri ? yaani kutaka kuwa "big potato in this country one day", huyu mtu anatuchezea au ? huko jimbo kwake amewafikiria hiyo miaka ya baadae au ndio kaona vizuri yeye kuwa big potato kuliko hao wananchi waliomchagua, ?

sasa anapanga nini michakato ya kugombea urais au maendeleo jimboni kwake ?? Mie nashindwa kuelewa, plans za urais sio lele mama, it can take a toll on somebody's life hadi kuwa rais ! kwa kifupi, zitto amechemsha, na anachotakiwa kufanya ni kwamba he needs to lay low, watu wasahau then baadae atoke upya, lakini hili suala watu watakuwa nalo tena hadi 2010 ukizingatia jimbo hilo la kigoma kaskazini asipokuwa makini zitto anaweza asipate tena au kama akipata basi chadema in over all wanaweza wasifanye vizuri kitaifa maana wataendeshwa sana huko kigoma kaskazini na watajikuta wanaspend muda wao mwingi huko badala ya kumkampeni mgombea wao wa kila siku anayeshindwa ambae pia atakuwa na wakati mgumu 2010.

Lakini haya yote ni kama zitto atagombea huko kigoma kaskazini, maana kuna info nilipata kwamba wapinzani wengi hao wakubwa 2010 wanaweza kugombea Dar !
 
Hivi mafanikio ya Zitto jimboni kwake ni yapi? mwenye data atuletee kuanzia elimu,afya,miundo mbinu etc,na vipi bungeni ana mafanikio yeyote yale...nakumbuka kuna wakati aliwasha cheche akafungiwa.
 
Back
Top Bottom