Kuwa makini unapotaka kuuza au kununua gari,nilikuwa nauza gari yangu kipindi flani,jamaa akatokea anaitaka hiyo gari,lakini sharti ili anunue ni lazima niipeleke kwenye yard yake ili akaikague,nikamwambia kwanini ni lazima nikuletee, kama unaihitaji njoo uione au tupange mahali pengine zaidi ya pale jamaa akaingia mitini,ila ikawa kila baada ya siku mbili au tatu ananipigia simu kutaka nimpelekee gari nikaachana naye.Mwingine alitaka kuniuzia gari nzuri sana lakini wakati naikagua ile gari nikaona pale kwenye engine namba ndani ya bonnet kile kibao kimen'golewa nilipomuuliza kaniambia njoo kesho,kuanzia kesho yake hakupokea tena simu yangu.Mwingine nilitaka kumuuzia gari akaja kuikagua akaniambia anataka kuiteset nikamuambia twende wote,tukiwa njiani jamaa alikuwa anaongea na watu wengine kwa lugha ambayo nilihisi ni Kikongo,tulipofika mahali ambapo alidai nimsubirie jamaa aliingia mitini na hakupokea simu yangu.Sasa ukiangalia utaona kuna sababau gani usiipokee simu kama gari ulikuwa hutaki kununua au hutaki kuuza? ni lazima tuwe waangalifu sana...