Naomba Msaada: Nyumba yetu inakaribia kuuzwa

Ana miaka 74, mimi ni ke,
Niko kwangu
Tunaye kaka mmoja ambaye kwa sasa maisha yake yameyumba hivyo anamshawishi mama auze nyumba ya familia ampe mtaji, hata hivyo hajawah kukanyaga mahakamani zaidi alitutumia ujumbe kwa simu kuwa nyumba inauzwa.
Yamkini kumbe Mama mdogo mnamsingizia isije kuwa huu mpango wote ni huyo Kaka yenu.
 
Ewaaaahh!! Mwana kwetu.
Hao watoto mama yao kuna kitu kaona, hao trust me akifa huyo mama bila kuuza nyumba watachinjana..!! 😹

Mama aache kula pension aliyochiwa na mumewe awaendekeze mijitu mizima isiyowaza kutafuta jasho lao.
 
Ana miaka 74, mimi ni ke,
Niko kwangu
Tunaye kaka mmoja ambaye kwa sasa maisha yake yameyumba hivyo anamshawishi mama auze nyumba ya familia ampe mtaji, hata hivyo hajawah kukanyaga mahakamani zaidi alitutumia ujumbe kwa simu kuwa nyumba inauzwa.
Sio mamdogo tena? 😹😹
Wewe muongo muongo.
Itoshe kusema mama auze hiyo nyumba ikimpendeza ampe kila mmoja chochote kitu mtauana akifa…!!
 
Kwanza watoto kulea wazazi ni tatizo lakini mzazi kuuza mali zake halafu alelewe na watoto ni tatizo kubwa zaidi.
Huyo mzazi kuna kitu kaona, lakini pia sio mbaya kuuza nyumba yake ikiwa watoto wakubwa wanajitegemea..!!
 
Sisi tumezaliwa wa5 ke4 me1 na

Mama amezeeka anataka kwenda kuwekeza wapi ktk umri huo, kama siyo ushauri mbaya wa mama yenu wadogo.

Nyumba katikati ya mjini ni mali kubwa na nyumba na kiwanja chake ni asset / mtaji endelevu inayoongezeka thamani na kutoa fursa kwa watoto na wajukuu kuingia katika mikataba minono na matajiri au mabenki huku mkiingiza kipato endelevu, makazi ghorofani ya kukodisha, kuishi n.k ikiwa mtaingia mikataba sahihi.

Mama kuuza nyumba mjini kati kisha kwenda kujenga majoring ktk uzee huo ni kosa kubwa dhidi ya legacy ya mtaji aliyowawekea nyie na mama yenu na watoto wenu.

Mstueni mama yenu, endeleeni kumtunza katika umri wake mkubwa hadi mwisho wa maisha yake ili asisikilize maneno ya nduguze ambao ni wazee pia kiumri.

Tutalalamika kuhusu familia za kina Dewji, Gulamali, Mengi n.k zenye utajiri. Utajiri huongezeka pale mali kama hizo zinapotunzwa zirithishwe kwa watoto ili legacy iendelee ya utajiri endelevu.

Kwanini siku zote waswahili haturithishi vizazi, tunadai kila kizazi kianze moja ktk kutafuta utajiri ?
 
Ewaaaahh!! Mwana kwetu.
Hao watoto mama yao kuna kitu kaona, hao trust me akifa huyo mama bila kuuza nyumba watachinjana..!! 😹

Mama aache kula pension aliyochiwa na mumewe awaendekeze mijitu mizima isiyowaza kutafuta jasho lao.
Ni kweli kabisa.
Wao wasimamie tu uuzwaji wa hiyo nyumba ili mama asipigwe, awakatie kidogo na wao. Huyo mwanaume anashindwa kwenda kupambana kwa ajili ya familia yake yeye kazi kumlia timing bi.mkubwa.
 
Mama mdogo sio ndugu yako na endapo kama yeye ndio kizuizi na mshawishi basi chezeni na akiri yake! Mbona Hilo jepesi Sana? Mshawishi ndio mvunjifu wa haki zenu na Mali zitapotea kwakuwa yeye Ana ushawishi hivyo, mama mdogo sio ndugu yenu, narudia tena huyo ni ndugu wa mama yenu ni bora mumtie uchizi kabisaaaa nyambafu huyo.
 
Yani ndugu inaumiza sana aisee, toka baba afariki na mirathi aliyoacha hakuna mtoto yyt ambaye amesema apewe mgao bali tuliona ni vyema kila baba alichoacha mama aendelee kusimamia na kodi ya nyumba zote anakusanya yeye kwa matumizi yake binafs ya chakula mavazi na kila atakacho, yani from no were ameshauriwa eti kwakua umri umeenda sana auze nyumba kiasi cha pesa ajenge nnyumba ndogo chanika na nnyingn afanye biashara. Yani unaona kabisa mwisho wa hili inaumiza mno
 
Sio mamdogo tena? 😹😹
Wewe muongo muongo.
Itoshe kusema mama auze hiyo nyumba ikimpendeza ampe kila mmoja chochote kitu mtauana akifa…!!
Shida ni kuwa umetanguliza kuongea sana kuliko kuelewa nilichoandika. Nidanganye ili i jitahidi kufungua ufahamu utanielewa.
Nimesema kashauriwa na mama mdogo auze nyumba na kaka ameafiki hilo sbb anataja apewe mtaji na dada zake tumepinga.
Umenielewa sasa?
 
Sasa si bora iuzwe sasa kuliko mama yenu akifa, ushafikiria nini kitatokea km huyo kaka yenu mkubwa anataka iuzwe pia?
 
Sasa si bora iuzwe sasa kuliko mama yenu akifa, ushafikiria nini kitatokea km huyo kaka yenu mkubwa anataka iuzwe pia?
Kila kitu ni kwa utaratibu sio kihuni.
Inaweza ikauzwa ama isiuzwe hata mama akiea hayupo
 
FATILIRN ARISE N SHINE
USIKU SAA TATU

WIKI IJAYO NJOON KAWE CHUKUENI MAJI NA MAFUTA YANENEEE MUNGU HAJASHINDWA

UKISIKIA UKOMBOZI WA ARDHI NJOO NA UDONGO WA HAPO KWENU CHUKUA CHANGANYA OMBEA IMILIKIE MALI KUWA YENU N JESUS NAME

UTANIPA MATOKEO
Wwe nae unaleta masihara kwenye vitu vya kisheria, mirathi iko kisheria na si kimaombi ya huko kanisani!!
 
Mkuu asante sana, najaribu kukuinbox bila mafanikio. Naomba ukiona hii reply yangu please naomba uniinbox. 🙏🙏🙏
 
Mwanzo alisema anataka kujenga nyumba nyingine chanika, sasa anasema anataka kuhamia kijijini akafuge kuku ndiyo maelezo aliyotoa mahakamanii hivi majuzi.
mama ako atapgwa tukio na mdogo wake huyo.
Kufuga kuku sio lelemama
 
Pole mkuu kwa changamoto hiyo. Ila kichwa cha mada hakiko sahihi. Nyumba yenu ndiyo INAYOTAKA KUUZWA?
Inawezekana nimekosea kwa kutokuwa mwandishi mzuri, au kwa kupanick, je ningeandikaje?
 
Tujikumbushe mali ni za baba na mama maana wa ndio waliozitafuta na sio za watoto.
Kwenye mali wengi wanafikiri ni za mwanaume tu na je kama hiyo nyumba alinunua mama yenu ndio ikaandikwa jina lake hamuoni mtakuwa mnamdhulumu mama yenu??
Hakununua mama sababu hakuwa na kazi yoyote, baba ndio alikuwa mfanyakazi meneja wa breweries.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…