Naomba mnielimishe umuhimu wa Imani na Dini

Naomba mnielimishe umuhimu wa Imani na Dini

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,461
Reaction score
40,078
Imani haina tofauti na itikadi. Imani inakupa mwelekeo wa kusimamia masuala yanayohusu utawala usioonekana kwamba ndiyo unaotawala fikra na hisia kuhusu uwepo, uumbaji na yanayodhanika kujiri baada ya nafsi na roho kuachana na mwili. (Hii ni tafsiri yangu)

Dini, ni utaratibu uliobuniwa na unatumika kudhibiti aina ya imani ambayo mtu anapaswa kufuata. Dini inasajiliwa lakini Imani haisajiliki.

Basi nimeona wazimu sana kuwa mwanadamu amelazimisha Imani na Dini vifungamane na kwenda pamoja ilihali kimoja ni bangi kingine ni kitakatifu.

Haya, wanazuoni akina Mzito Kabwela na wengineo, mnaweza kunielimisha beyond hayo madhanifu yangu kwenye Imani na Dini?

UPDATE

Ukiachana na matangopori tuliyolishwa kuwa ukifanya hivi unakufuru ama ukifanya vile utapata dhambi na kufikiri kwa fikra huru utagundua juu ya dhima halisi ya hizi dini.
1. Dini ni Social institutions ambazo zilibuniwa mahususi ili kumdhibiti binadamu kwa kumlisha itikadi na kumjengea hofu ili aweze kukaa kwa amani na jamii inayomzunguka. Kwa maana hiyo dini inafanya jukumu kama taasisi zingine zilizo kwenye jamii mfano; Mahakama, Shule, vyuo, Magereza na Polisi.

2. Imani ni zao la utamaduni, mafundisho ama experience ya maisha juu ya jambo, mtu, kitu ama tabia. Kwahiyo imani imejengwa katika msingi huo kwa maana imani inatokana na dhana ya kuamini.

3. Kwa muktadha wa sasa Dini inatumika kama chombo cha kubebea imani. Ni kama vile makahama ambayo ni social institution inavyotumika kutafsiri sheria ambayo ni mafundisho jambo sahihi na lisilo sahihi kwa mujibu wa taratibu za jamii husika. Kwahiyo mahakama na sheria ni vitu viwili tofauti ila vinafanya kazi kwa pamoja.

HITIMISHO:
Dini na imani ni vitu viwili tofauti ila vinavyofanya kazi kwa pamoja. Dini ni chombo kinachotumika kubeba imani.
Vyote kwa pamoja vilibuniwa na watu wenye akili nyingi sana kwa lengo la kumdhibiti Binadamu kifikra, kimatendo na kutengeneza ustaarabu kwenye jamii. Hutumia njia njia ya mafundisho, kujenga hofu na uwoga, pamoja na ahadi za adhabu na tuzo kwa wanaotenda kwa mujibu wa mafundisho na wale wanaoenda kinyume. Dhana kama vile dhambi, kukufuru ni nyezo kuu za kudhibiti uwezo wa Binadamu kuwa na hofu ya kuhoji mamlaka zilizoasisi imani hizi na mapungufu ambayo kwasasa yanadhihirika katika imani hizi
 
Imani ni kukubali au kuamini jambo kuwa la kweli, hata kama ushahidi wake hauonekani moja kwa moja.

Dini ni mfumo uliopangwa wa imani, ibada, maadili, na desturi unaounganisha waumini katika namna fulani ya kumwabudu Mungu au kueleza maswali ya msingi kuhusu maisha. Dini mara nyingi huwa na maandiko, viongozi, na taasisi.

Mtu anaweza:
• Kuwa na imani ya kiroho bila kufuata dini yoyote.
• Kufuata dini lakini imani yake iwe dhaifu au ya mazoea.
• Asiwe na dini wala imani ya nguvu kuhusu mambo ya kiroho.

Watu wengi, imani huwapa maana ya maisha, matumaini, na msingi wa maamuzi ya kimaadili

Dini inaweza kutoa utambulisho wa kijamii, mshikamano, mfumo wa maadili, ibada, na utamaduni wa pamoja. Hata hivyo, inaweza pia kutumiwa vibaya kwa udhibiti wa kisiasa au kijamii, jambo ambalo limeonekana katika vipindi mbalimbali vya historia
 
Imani ya dini ni nzuri kwasababu ukifa utazikwa kwa mapambio au swala na dua.

Swala na dua ni fursa ya mwisho inayo ku backup kusafisha dhambi zako ambazo ulifanya ila kifo kikaingilia kati na kukufanya ukose muda wa kuziungama.
 
Imani haina tofauti na itikadi. Imani inakupa mwelekeo wa kusimamia masuala yanayohusu utawala usioonekana kwamba ndiyo unaotawala fikra na hisia kuhusu uwepo, uumbaji na yanayodhanika kujiri baada ya nafsi na roho kuachana na mwili. (Hii ni tafsiri yangu)

Dini, ni utaratibu uliobuniwa na unatumika kudhibiti aina ya imani ambayo mtu anapaswa kufuata. Dini inasajiliwa lakini Imani haisajiliki.

Basi nimeona wazimu sana kuwa mwanadamu amelazimisha Imani na Dini vifungamane na kwenda pamoja ilihali kimoja ni bangi kingine ni kitakatifu.

Haya, wanazuoni akina Mzito Kabwela na wengineo, mnaweza kunielimisha beyond hayo madhanifu yangu kwenye Imani na Dini?
Dini ni mifumo iliyotengenezwa na watu ila imani ni hisia ya mtu moyoni kuhusu muumba wake.
 
Fikiria hali inayoitwa 'akili'. Tunaposema akili au tunapoongea juu ya neno 'akili' tunarejelea nini, hali gani?

Akili ya binadamu kwa mfano, akili ya wanyama, ya mimea; au akili ya mitambo, ni hali gani? Ni nini? Je! Ni ufahamu? Ni utambuzi? Ni uelewa? Ni kujua?

Imani ni hali ya kiakili inayopita ufahamu na utambuzi wa kawaida wa akili ya binadamu. Kimsingi ni uelewa wa hali ya juu au kina wa mambo na elimu ya vitu, jinsi mambo yalivyo.

Kuhusu dini. Cha kwanza ni uelewa, 'kujua' ukweli kuhusu dini. Halafu hufuata kupenda, 'upendo'. Watu ambao hawana uelewa wa kina wa mambo na elimu ya vitu wanaweza kudanganywa na hivyo kupotoshwa au kupotoka kuhusu ukweli kuhusu dini.
 
nisaidie wew unavyoelewa
Ukisoma post ya kwanza nimefanya ulivyoomba.

Wewe unaelezea void inayoweza kuwa dhahiri na umejielekeza kwenye imani inayoleta miujiza.

Tujadili imani kama msingi unaosimika utambuzi, uwepo na itikadi kwenye fikra na siyo matumaini

Eneo la dini ni mfumo dhibiti na siyo saidizi
 
ni kweli dini inadhibiti je haisaidii kumfanya mtu kuwa na utambuzi na itikadi kwenye fikra zake?

Je kipi kinamfanya mtu kuwa na imani?
 
jamii ndo imetufanya tuwe watumwa wa kukubali iman wanayotupatia ukioji sana wanakuona mkorofi na msumbufu
Nakumbuka nilimuuliza marehemu baba yangu (ambaye baada ya kustaafu alikuwa mchungaji wa kanisa lake) kuhusu uwepo wa majina ya Mungu kwenye makabila yetu. Nikihoji kuhusu Waafrika kuitwa wapagani, makafiri wasio na imani.

Alibaki kushangaa maana majina hata ya watoto kiafrika yanathibitisha uwepo wa Mungu.

Hizi dini ni bangi za watu kuwavuna kiakili wanajamii na kujimilikisha limitation ya kufikiri, kuhoji hata kupokea mawazo mapya
 
upo sahihi dini mtego na inavyoonekana huna dini maana kwenye dini ukihoji sana wanakuita mataifa au kafiri
 
upo sahihi dini mtego na inavyoonekana huna dini maana kwenye dini ukihoji sana wanakuita mataifa au kafiri
Mkuu
Nimezaliwa na kulelewa dini ya Kikristo kama wanavyoita.

Nilikuja kugundua kuwa Yesu alitaka wote wamuaminio wawe Wanafunzi wake. Lakini pale Antiokia enzi za Mitume walianza kujiita Wakristo yaani wafuasi wa Kristo.

Baada ya Wanamatengenezo wa kwanza kuamua kujitenga na dini ya ulimwengu yaani Katoliki, waliitwa Protestants yaani WAASI wa KIDINI/ IMANI. Ambapo ndani yake zipo dini nyingi zinazojiita za Kikristo. Hapo ndipo sasa tunaona Walokole, Waanglikana, Menonite, Wafuasi wa Luther (Waluteri) na kadhalika.

Yesu alifanya huduma yake kila mahala. Aliingia hadi misikitini (Masinagogi) ambapo ushahidi ni yule mgonjwa aliyeshushwa kitanda chake na kamba akiwa sinagogini na akamponya. Leo mwambie mlokole kuwa aende msikitini Ijumaa akavune ngano ya Bwana, atakutoa pepo maana ataona huu ni wazimu.

Dini inabagua
Dini inaweka masharti
Dini inamiliki utashi binafsi
Dini inadogosha Imani halali kwa Muumba
 
Imani haina tofauti na itikadi. Imani inakupa mwelekeo wa kusimamia masuala yanayohusu utawala usioonekana kwamba ndiyo unaotawala fikra na hisia kuhusu uwepo, uumbaji na yanayodhanika kujiri baada ya nafsi na roho kuachana na mwili. (Hii ni tafsiri yangu)

Dini, ni utaratibu uliobuniwa na unatumika kudhibiti aina ya imani ambayo mtu anapaswa kufuata. Dini inasajiliwa lakini Imani haisajiliki.

Basi nimeona wazimu sana kuwa mwanadamu amelazimisha Imani na Dini vifungamane na kwenda pamoja ilihali kimoja ni bangi kingine ni kitakatifu.

Haya, wanazuoni akina Mzito Kabwela na wengineo, mnaweza kunielimisha beyond hayo madhanifu yangu kwenye Imani na Dini?
Imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana!

Cc: Seran, Baba mtakatifu91, Powder
 
Mkuu upo sahihi kabisa tena 100% dini inamwezesha mtu kuishi kwa upendo ambapo ndo golden rule ya kumfikia Mungu. Wanatheolojia wote hutamani waamini watumie akili zao ili kusolve changamoto za kimaisha na kama itashindikana ndo nguvu ya Kimungu ifanye kazi. Cha ajabu waamini wamekuwa waraibu wa dini. Huku mtaani tumezika mtoto wa miaka 7 baada ya kung'atwa na nyoka mama yake ni mlokole alianza kukemea eti toka shetani. Bila kujua snake venom husambaa faster kwenye damu.
 
Back
Top Bottom