Naomba mnielimishe umuhimu wa Imani na Dini

Naomba mnielimishe umuhimu wa Imani na Dini

Ahsante kwa majibu yako. Nimefurahi kwamba sasa umekubali jambo muhimu ulilokuwa umelikataa mwanzo, kwamba intuition au hisia za ndani peke yake hazitoshi kuthibitisha ukweli, bali ni factor mojawapo. Hapo tayari tumekubaliana.

Lakini hapo ndipo Uislamu unaweka msingi tofauti.

Qur'an haimwambii mwanadamu afuate hisia zake tu. Inamwambia atumie akili, ushahidi na wahyi kwa pamoja.

Kwa hiyo Uislamu hausimami juu ya "nilihisi", bali juu ya dalili (burhan), akili ('aql), na wahyi.

Umesema dini nyingi zinaongelea meditation na ufahamu wa ndani. Ni kweli. Lakini hiyo ndiyo hoja yangu.

Kama dini zote zina uzoefu wa kiroho unaofanana, basi uzoefu huo hauwezi kutumika kuthibitisha kwamba dini moja ndiyo sahihi.

Lazima kuwe na kipimo kingine kinachoweza kutenganisha ukweli na makosa.

Umesema pia huwezi kuabudu mti kwa sababu umeumbwa.

Nami nakubaliana kabisa na hilo.

Lakini sasa swali linaendelea:

Kama Muumba ni mmoja, kwa nini tumwamini kupitia mafundisho yaliyobadilika na yenye migongano, badala ya wahyi unaodaiwa kuhifadhiwa?

Qur'an inasema:

Na pia:

Hivyo Uislamu hauombi watu waamini kwa sababu ya ndoto, maono au hisia. Unawataka wachunguze wahyi wenyewe.

Umesema pia watu wamefunuliwa.

Nina swali moja tu:

Tukikubali kwamba kuna watu wa Kikristo, Kiislamu, Kihindu na Kibudha wote wanaodai wamefunuliwa, basi ufunuo wa nani ndiyo wa kweli?

Kama hakuna kipimo cha nje ya uzoefu wao, kila mmoja atasema "nimefunuliwa".

Ndiyo maana katika Uislamu hata mtu akiona malaika au akaota ndoto, ndoto hiyo haifanyi sheria wala haipingani na Qur'an. Wahyi ndiyo unaohukumu uzoefu, si uzoefu unaohukumu wahyi.

Umetaja pia mapepo kutoka kwa jina la Yesu.

Lakini hilo peke yake haliwezi kuthibitisha Ukristo kuwa wa kweli, kwa sababu hata Waislamu wanasoma Qur'an na ruqyah, na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mapepo huondoka pia.

Hivyo tukitumia matukio ya kiroho kama kipimo, kila dini italeta ushuhuda wake.

Mwisho kabisa umesema masuala ya imani hayawezi kuthibitishwa universally.

Hapo ndipo ninatofautiana kidogo.

Si kila kitu kuhusu Mungu kinaweza kuthibitishwa kisayansi, lakini madai ya dini yanaweza kuchunguzwa kwa mantiki na ushahidi.

Swali si "nani amehisi zaidi?" bali ni:

Ni nani analeta wahyi uliohifadhiwa, usio na migongano, unaolingana na tauhidi ya Mitume wote kuanzia Adamu, Nuhu, Ibrahim, Musa na Isa (Yesu), na unaomwelekeza mwanadamu kumuabudu Mungu Mmoja bila mshirika?

Mimi nilipochunguza swali hilo bila kufuata hisia pekee, nikakuta Uislamu ndiyo unaojibu kwa uthabiti zaidi.
Kufunuliwa kwa kiroho hakutegemei dini wala dhehebu.

Watu walofunuliwa ndani yao wanatambua kwamba wakiristo, waislam, wajudah wanamuamini Mungu mmoja. Wale ambao hawaamini katika Mungu huyu wa Abraham/Ibrahim nao waje na facts zao sasa.

Mimi navyojua mtu anafunuliwa akitambua kweli na akaifikia kweli bila kujali kapitia njia gani ilimradi kafika.

Lakini ili ufunuliwe lazima upitie miongozo sahihi, miongoni mwa miongozo ni maandiko ya vitabu mbalimbali vya kiroho.

Kwa maana imeandikwa Hossea 4:6 "Watu wangu wanaagamia kwa kukosa maarifa". Maybe watu wengi hawajui masuala mengi kwa sababu hawana maarifa, na maarifa inabidi wayatafute.

Waefeso 5:8
"Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru"

Huenda wapo bado gizani 😂
 
Tofauti huwa zinaletwa na tamaduni za watu wa maeneo husika tu. Mfano Qur'an iliathiriwa na tamaduni za waharabu, biblia pia imeathiriwa na tamaduni za warumi, wagiriki, na waingereza. Bado pia maandiko haya yana tafsiri za wanadamu. Ndio maana wanasema usome uelewe yale ya msingi, ila ukikalili na kumeza kila kitu kama kilivyo utatoka nje ya misingi.
 
Ahsante kwa maelezo yako. Kuna mambo kadhaa ambayo nakubaliana nayo, lakini bado kuna swali la msingi ambalo hujalijibu.

Umesema:

"Mtu akifunuliwa anaitambua kweli bila kujali kapitia njia gani."

Sawa, lakini swali ni:

Ni nani anayethibitisha kwamba alichokiona ni kweli, na si mawazo yake mwenyewe au udanganyifu wa shetani?

Biblia yenyewe inaonya:

"Mpenzi, msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho kwamba zimetokana na Mungu." (1 Yohana 4:1)

Kama kila anayesema "nimefunuliwa" angekuwa sahihi, basi Yohana asingesema roho zipimwe.

Pia umesema Wakristo, Waislamu na Wayahudi wanamuamini Mungu mmoja. Hilo ni kweli kwa upande wa asili ya ujumbe wa Ibrahim (Abrahamu). Lakini tofauti kubwa si kuhusu kuwepo kwa Mungu mmoja, bali jinsi ya kumwabudu Mungu huyo.

Musa hakufundisha Utatu.

Ibrahim hakufundisha Utatu.

Yesu alisema:

"Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja." (Marko 12:29)

Hivyo swali linabaki:

Kwa nini turejee kwenye mafundisho yaliyokuja baadaye, badala ya kushikamana na tauhidi aliyofundisha Ibrahim, Musa na Yesu?

Qur'an inasema:

"Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lililo sawa baina yetu na nyinyi; kwamba tusimuabudu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote." (Qur'an 3:64)

Hii ndiyo ninayoiona kuwa njia ya kuwaunganisha watu wote waliomfuata Ibrahim.

Umenukuu Hosea 4:6:

"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa."

Nami nakubaliana kabisa. Lakini maarifa hayapatikani kwa hisia pekee; yanapatikana kwa kuchunguza wahyi na ushahidi.

Ndiyo maana Qur'an inasema:

"Leteni ushahidi wenu ikiwa nyinyi ni wakweli." (Qur'an 2:111)

Hata Uislamu hauwaambii watu waamini bila dalili.

Mwisho, ningekuuliza swali moja la kutafakari:

Kama Ibrahim, Musa, Yesu na Muhammad wote walimuita mwanadamu amuabudu Mungu Mmoja bila mshirika, je, si busara zaidi kurudi kwenye ibada hiyo safi ya Mungu Mmoja badala ya kuongeza mafundisho ambayo Mitume wa mwanzo hawakuyafundisha?

Mimi naamini huo ndio ulikuwa ujumbe wa Mitume wote.
 
Tofauti huwa zinaletwa na tamaduni za watu wa maeneo husika tu. Mfano Qur'an iliathiriwa na tamaduni za waharabu, biblia pia imeathiriwa na tamaduni za warumi, wagiriki, na waingereza. Bado pia maandiko haya yana tafsiri za wanadamu. Ndio maana wanasema usome uelewe yale ya msingi, ila ukikalili na kumeza kila kitu kama kilivyo utatoka nje ya misingi.

Hapa naona umeanzisha tatizo jipya ambalo linaathiri hata hoja zako za mwanzo.

Umesema Qur'an imeathiriwa na tamaduni za Waarabu, Biblia imeathiriwa na tamaduni za Warumi, Wagiriki na Waingereza, halafu ukasema tusikariri maandiko bali tuchukue yale ya msingi.

Sasa nina maswali machache:

1. Ni nani anayeamua ni lipi la msingi na lipi ni la kitamaduni?

Wewe? Mimi? Mchungaji? Au kila mtu atajichagulia anachokipenda?

Kama hakuna kipimo, basi dini inakuwa maoni ya kila mtu, si wahyi wa Mungu.

2. Kama maandiko yameathiriwa na wanadamu kiasi kwamba hayawezi kufuatwa kama yalivyo, tuna uhakika gani kwamba mafundisho muhimu hayajabadilishwa pia?

Hapo ndipo Qur'an inatofautiana. Qur'an haisemi ichague sehemu zinazokupendeza na kuacha nyingine. Inasema ni wahyi uliolindwa:

"Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'an, na hakika Sisi ndio tutakaoilinda." (Qur'an 15:9)

3. Umesema kuna tafsiri za wanadamu.

Hilo ni kweli. Lakini tafsiri siyo Qur'an yenyewe. Tafsiri inaweza kutofautiana, lakini matini ya Kiarabu ya Qur'an ni ileile inayosomwa leo duniani kote. Muislamu wa Tanzania, Indonesia, Uturuki au Marekani anasoma Qur'an ileile kwa Kiarabu.

4. Kuhusu tamaduni za Waarabu.

Ni kweli Qur'an iliteremshwa kwa Kiarabu na ndani ya mazingira ya Waarabu, kama vile Injili ilikuja katika mazingira ya Wayahudi. Lakini mazingira si chanzo cha ujumbe.

Qur'an yenyewe inasema:

"Hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mtoaji wa habari njema na mwonyaji." (Qur'an 34:28)

Hivyo ujumbe ni wa ulimwengu wote, ingawa ulianza katika jamii fulani.

Mwisho ningekuuliza swali moja la kutafakari:

Kama unaamini maandiko hayawezi kufuatwa kama yalivyo kwa sababu yamechanganyika na tamaduni na tafsiri za wanadamu, basi unajuaje kwamba mafundisho unayoamini leo ndiyo hasa aliyofundisha Yesu, na si tafsiri ya baadaye ya wanadamu?

Mimi ndiyo maana naona Qur'an inatoa suluhisho. Inamrudisha mwanadamu kwenye Tauhidi ya Ibrahim, Musa, Yesu na Mitume wote: kumuabudu Mwenyezi Mungu Mmoja bila mshirika, na inadai kuwa imehifadhiwa ili isiwe kila kizazi kinachagua "cha msingi" kwa maoni yake.
 
Imani haina tofauti na itikadi. Imani inakupa mwelekeo wa kusimamia masuala yanayohusu utawala usioonekana kwamba ndiyo unaotawala fikra na hisia kuhusu uwepo, uumbaji na yanayodhanika kujiri baada ya nafsi na roho kuachana na mwili. (Hii ni tafsiri yangu)

Dini, ni utaratibu uliobuniwa na unatumika kudhibiti aina ya imani ambayo mtu anapaswa kufuata. Dini inasajiliwa lakini Imani haisajiliki.

Basi nimeona wazimu sana kuwa mwanadamu amelazimisha Imani na Dini vifungamane na kwenda pamoja ilihali kimoja ni bangi kingine ni kitakatifu.

Haya, wanazuoni akina Mzito Kabwela na wengineo, mnaweza kunielimisha beyond hayo madhanifu yangu kwenye Imani na Dini?
Kwenye dini unaamnini kwanza halafu ndiyo una-prove. Kwenye Sayansi, unaprove kwanza halafu ndiyo unaamini.

Kwenye dini, ukiona kuwa kile ulichokiamini hauwezi kuki-prove; ujue umekosea; umepotea. Ni bora ukaachana kabisa na dini. Dini iliyo sahihi ni lazima ifikie mahali i-prove kile unachokiamini na ikishindwa, ujue hiyo siyo dini ya kweli!
 
Kauli yako ina sehemu ya ukweli, lakini imeweka mambo kwa mtazamo unaorahisisha kupita kiasi.

Kwanza, si kweli kwamba sayansi huanza bila imani yoyote. Sayansi huanza na dhana (hypothesis) ambayo bado haijathibitishwa. Baada ya hapo ndipo hufanyika uchunguzi na majaribio. Hivyo, hata sayansi huanza kwa kukubali uwezekano wa jambo fulani kabla ya kulithibitisha.

Pili, si kila ukweli unaweza kuthibitishwa kwa maabara. Kwa mfano, huwezi kuthibitisha kwa maabara kwamba upendo wa mama kwa mtoto wake ni wa kweli, au kwamba haki na maadili ni halisi. Lakini bado tunaamini vitu hivyo kwa ushahidi wa aina nyingine.

Tatu, dini nyingi hazidai kwamba Mungu ni kitu kinachoweza kuwekwa kwenye darubini au maabara. Zinatoa aina tofauti ya ushahidi: historia, ushuhuda wa manabii, maandiko, mantiki ya kifalsafa, na uzoefu wa wanadamu. Unaweza usikubali ushahidi huo, lakini si sahihi kusema si ushahidi kabisa.

Nne, hata sayansi ina mipaka. Sayansi hueleza jinsi (how) mambo yanavyotokea, lakini mara nyingi haiwezi kujibu kwa nini (why) kuna ulimwengu badala ya kutokuwepo kabisa, kwa nini sheria za asili zipo, au kwa nini fahamu na maadili yapo. Haya ni maswali ya kifalsafa na kidini zaidi kuliko ya kisayansi.

Kwa hiyo, hoja sahihi si kusema, "Dini ikishindwa kuthibitishwa kwa mbinu za sayansi basi ni ya uongo." Hoja sahihi ni kuuliza: Je, dini hiyo ina ushahidi wa kutosha unaolingana na madai yako? Hapo ndipo mjadala wa kweli unaanzia.

Ukisema kila jambo lazima lithibitishwe kisayansi ndipo liaminike, basi kwanza uthibitishe kisayansi kauli yenyewe kwamba: "Ni mambo yanayothibitishwa kisayansi pekee ndiyo yanapaswa kuaminiwa." Kauli hiyo yenyewe haiwezi kuthibitishwa kwa majaribio ya kisayansi; ni msimamo wa kifalsafa, si hitimisho la sayansi.
 
SIJASOMA MAELEZO YOTE YA PoST YAKO LAKINI NAOMBA NIKUJULIDJE KUWA PREMISES ULIZOANZA NAZO TAYARI ZINAONYESHA KUWA UNAJI-CONTRADICT. DHANA (HYPOTHESIS) NA IMANI (BELIEF) NI VITU VIWILI TOFAUTI LAKINI WEWE UNASRMA HYPOTHESIS NDIYO BELIEF, KITU AMBACHO SIYO KWELI.

DHANA HUWA INAZALIWA KUTOKA KWRNYE SUSPICION KWAMBA POSSIBLY A INAWEZA IKAWA Z, WAKATI IMANI NI FACTS ZIINAZOJULIKANA TAYARI AMBAZO SIYO LAZIMA ZIWE NA UWEZO WA KUWA PROVED KWA KUTUMIA INSTRUMENTS ZA KISAYANSI, NA XIKO INDEPENDENT OF THE KNOWLEDGE OF THE KNOWER. KWAMBA KWA MFANO, WEWE KUWA NA IMANI KUWA MUNGU YUPO, HAKUMFANYI AKAWA YUPO KAMA HAYUPO, NA VILE VILE WEWE KUWA NA IMANI KUWA MUNGU HAYUPO, HAKUMFANYI AKAWA HAYUPO KAMA YUPO
 
Imani haina tofauti na itikadi. Imani inakupa mwelekeo wa kusimamia masuala yanayohusu utawala usioonekana kwamba ndiyo unaotawala fikra na hisia kuhusu uwepo, uumbaji na yanayodhanika kujiri baada ya nafsi na roho kuachana na mwili. (Hii ni tafsiri yangu)

Dini, ni utaratibu uliobuniwa na unatumika kudhibiti aina ya imani ambayo mtu anapaswa kufuata. Dini inasajiliwa lakini Imani haisajiliki.

Basi nimeona wazimu sana kuwa mwanadamu amelazimisha Imani na Dini vifungamane na kwenda pamoja ilihali kimoja ni bangi kingine ni kitakatifu.

Haya, wanazuoni akina Mzito Kabwela na wengineo, mnaweza kunielimisha beyond hayo madhanifu yangu kwenye Imani na Dini?
Sio kila mwenye imani ana dini na sio kila mwenye dini ana imani
 
Nimegundua huna hoja ya kujibu, ndiyo maana umekimbilia maneno kama "fallacy", "bondage" na "uhuru wa kufikiri" bila hata kuyafafanua.

Unasema dini ni mfumo wa udhibiti. Huo ni msimamo wako, si hoja iliyothibitishwa. Uthibitishe kwa ushahidi, si kwa kauli za jumla.

Unasema kukariri maandiko si ufahamu. Sawa. Lakini wewe unaleta madai bila hata chanzo kimoja cha kuthibitisha unachokisema. Tofauti ni kwamba mimi ninanukuu msingi ninaousimamia, wewe unanukuu maoni yako mwenyewe kana kwamba ndiyo ukweli wa mwisho.

Unadai dini imejengwa juu ya ubaguzi. Basi eleza kwa hoja: je, falsafa, utaifa, ujamaa, ubepari na hata ukafiri havijawahi kujenga ubaguzi au kumwaga damu? Kama jibu ni ndiyo, kwa nini unailaumu dini peke yake? Hiyo ndiyo inaitwa double standard.

Pia unasema nitumie "uhalisia tunaouishi". Ukweli wa kitu haupimwi kwa hali ya jamii bali kwa ushahidi. Zamani watu waliishi wakiamini dunia ni tambarare; uhalisia wao haukuifanya iwe tambarare.

Mwisho, unazungumzia "uhuru wa kufikiri", lakini kila unapokutana na aya au ushahidi kutoka kwenye maandiko unaukataa bila kuujibu. Huo si uhuru wa kufikiri; huo ni uhuru wa kukataa ushahidi usiokubaliana na msimamo wako.

Kwa hiyo acha maneno makubwa yasiyo na maudhui. Kama una hoja, ijibu hoja kwa hoja. Kama huna, usijifiche nyuma ya maneno kama "fallacy", "bondage" na "critical thinking". Maneno hayo hayashindi hoja; ushahidi ndio unaoshinda hoja.
Takataka
 
SIJASOMA MAELEZO YOTE YA PoST YAKO LAKINI NAOMBA NIKUJULIDJE KUWA PREMISES ULIZOANZA NAZO TAYARI ZINAONYESHA KUWA UNAJI-CONTRADICT. DHANA (HYPOTHESIS) NA IMANI (BELIEF) NI VITU VIWILI TOFAUTI LAKINI WEWE UNASRMA HYPOTHESIS NDIYO BELIEF, KITU AMBACHO SIYO KWELI.

DHANA HUWA INAZALIWA KUTOKA KWRNYE SUSPICION KWAMBA POSSIBLY A INAWEZA IKAWA Z, WAKATI IMANI NI FACTS ZIINAZOJULIKANA TAYARI AMBAZO SIYO LAZIMA ZIWE NA UWEZO WA KUWA PROVED KWA KUTUMIA INSTRUMENTS ZA KISAYANSI, NA XIKO INDEPENDENT OF THE KNOWLEDGE OF THE KNOWER. KWAMBA KWA MFANO, WEWE KUWA NA IMANI KUWA MUNGU YUPO, HAKUMFANYI AKAWA YUPO KAMA HAYUPO, NA VILE VILE WEWE KUWA NA IMANI KUWA MUNGU HAYUPO, HAKUMFANYI AKAWA HAYUPO KAMA YUPO
Jaribu kusoma kisha mbeleni wapo waliotoa maelezo ya kina zaidi ya nilichoandika.

Karibu
 
Fikiria hali inayoitwa 'akili'. Tunaposema akili au tunapoongea juu ya neno 'akili' tunarejelea nini, hali gani?

Akili ya binadamu kwa mfano, akili ya wanyama, ya mimea; au akili ya mitambo, ni hali gani? Ni nini? Je! Ni ufahamu? Ni utambuzi? Ni uelewa? Ni kujua?

Imani ni hali ya kiakili inayopita ufahamu na utambuzi wa kawaida wa akili ya binadamu. Kimsingi ni uelewa wa hali ya juu au kina wa mambo na elimu ya vitu, jinsi mambo yalivyo.

Kuhusu dini. Cha kwanza ni uelewa, 'kujua' ukweli kuhusu dini. Halafu hufuata kupenda, 'upendo'. Watu ambao hawana uelewa wa kina wa mambo na elimu ya vitu wanaweza kudanganywa na hivyo kupotoshwa au kupotoka kuhusu ukweli kuhusu dini.
AKILI ni uwezo wa KIUMBE kupokea taarifa,kisha kuichakata na kutoa maamuzi

IMANI ni kuchagua kukubali kwamba kitu fulani kipo bila ya kuwa na UTHIBITISHO wowote

DINI ni IMANI, watu wameamua kuamini kwamba Mungu yupo na ametupa muongozo wa kufuata tunapoishi

NB
Kitu chochote kinacho ambacho KIPO hakiwezi kuwa ni IMANI
IMANI ni kwa vitu ambavyo havipo
 
IMANI ni kuchagua kukubali kwamba kitu fulani kipo bila ya kuwa na UTHIBITISHO wowote

DINI ni IMANI, watu wameamua kuamini kwamba Mungu yupo na ametupa muongozo wa kufuata tunapoishi
Huwezi kutenganisha imani na kujua au na kuelewa.
Mtu ambaye hajui, ambaye haelewi hawezi kusema ana imani na jambo hilo.
 
Huwezi kutenganisha imani na kujua au na kuelewa.
Mtu ambaye hajui, ambaye haelewi hawezi kusema ana imani na jambo hilo.
Kitu kikijulikana kinakua ni FACT………..Fact huwa ni MOJA TU haina LONGOLONGO

Kikombe cha Babu wa Loliondo au maji ya upako ya Mwamposa ni IMANI huwezi ku prove inaponya……. Lakini Dawa mseto ya Malaria ni FACT inatibu Malaria, you can prove it

IMANI sio KUJUA au KUELEWA jambo…….. ni kukubali kuwa jambo lipo bila UTHIBITISHO

Kuna IMANI za MUNGU tofauti tofauti zaidi ya 1000 duniani kote, na kila imani inaamini INAMJUA na KUMUELEWA Mungu wao ndio Mungu wa kweli……,, hii haimaanishi ni KWELI wanamjua na kumuelewa Mungu wao ila wamekubali yupo tu
 
Kujifariji na kujipa matumaini hata kama ni uongo tu
 
Mfano wako wa kikombe cha babu wa Loliondo na maji ya Mwamposa ni ushahidi kuwa watu hao (watanzania wengi) hawana uelewa wa kina wa mambo na elimu ya vitu.

Jambo hilo la kikombe cha babu au maji ya Mwamposa sio mambo ya imani wala hayahusiani na imani kwa sababu hayana sifa hizo.

Imani sio kukubali bila kuwa na uelewa au kujua jambo unalolikubali. Kwa sababu kukubali kitu ambacho hukijui(hujui) ni kukubali kufanya makosa isipokuwa kama jambo hilo ni la kweli.

Kuhusu imani kutoka kwa Mungu (faith). Hii inahusu na inaeleza 'kweli za kiakili'. Jinsi mambo yalivyo.

Kutothibitika kisayansi kwa 'kweli za kiakili' hakuelezwi kuwa jambo hilo halipo. Kunaweza kuwa kwa sababu za maarifa au huruki ambazo zinapita uelewa wetu wa sasa.
 
Imani haina tofauti na itikadi. Imani inakupa mwelekeo wa kusimamia masuala yanayohusu utawala usioonekana kwamba ndiyo unaotawala fikra na hisia kuhusu uwepo, uumbaji na yanayodhanika kujiri baada ya nafsi na roho kuachana na mwili. (Hii ni tafsiri yangu)

Dini, ni utaratibu uliobuniwa na unatumika kudhibiti aina ya imani ambayo mtu anapaswa kufuata. Dini inasajiliwa lakini Imani haisajiliki.

Basi nimeona wazimu sana kuwa mwanadamu amelazimisha Imani na Dini vifungamane na kwenda pamoja ilihali kimoja ni bangi kingine ni kitakatifu.

Haya, wanazuoni akina Mzito Kabwela na wengineo, mnaweza kunielimisha beyond hayo madhanifu yangu kwenye Imani na Dini?
Ukiachana na matangopori tuliyolishwa kuwa ukifanya hivi unakufuru ama ukifanya vile utapata dhambi na kufikiri kwa fikra huru utagundua juu ya dhima halisi ya hizi dini.
1. Dini ni Social institutions ambazo zilibuniwa mahususi ili kumdhibiti binadamu kwa kumlisha itikadi na kumjengea hofu ili aweze kukaa kwa amani na jamii inayomzunguka. Kwa maana hiyo dini inafanya jukumu kama taasisi zingine zilizo kwenye jamii mfano; Mahakama, Shule, vyuo, Magereza na Polisi.

2. Imani ni zao la utamaduni, mafundisho ama experience ya maisha juu ya jambo, mtu, kitu ama tabia. Kwahiyo imani imejengwa katika msingi huo kwa maana imani inatokana na dhana ya kuamini.

3. Kwa muktadha wa sasa Dini inatumika kama chombo cha kubebea imani. Ni kama vile makahama ambayo ni social institution inavyotumika kutafsiri sheria ambayo ni mafundisho jambo sahihi na lisilo sahihi kwa mujibu wa taratibu za jamii husika. Kwahiyo mahakama na sheria ni vitu viwili tofauti ila vinafanya kazi kwa pamoja.

HITIMISHO:
Dini na imani ni vitu viwili tofauti ila vinavyofanya kazi kwa pamoja. Dini ni chombo kinachotumika kubeba imani.
Vyote kwa pamoja vilibuniwa na watu wenye akili nyingi sana kwa lengo la kumdhibiti Binadamu kifikra, kimatendo na kutengeneza ustaarabu kwenye jamii. Hutumia njia njia ya mafundisho, kujenga hofu na uwoga, pamoja na ahadi za adhabu na tuzo kwa wanaotenda kwa mujibu wa mafundisho na wale wanaoenda kinyume. Dhana kama vile dhambi, kukufuru ni nyezo kuu za kudhibiti uwezo wa Binadamu kuwa na hofu ya kuhoji mamlaka zilizoasisi imani hizi na mapungufu ambayo kwasasa yanadhihirika katika imani hizi
 
Mkuu hili andiko lako nimeliongeza kule juu ili waliokaza shingo kwenye kuyachambua haya mambo wakiamini tunakufuru
 
Back
Top Bottom