Superbrand mimi nakuomba sana sana kama dada yako yatosha sasa,unakoelekea siko kabisaaa,umeshalitoa lako la moyoni yatosha sasa usijibu tena,wewe hujamtaja mtu ila watu ndo wanaendelea kupamba.
Jua tu hakuwa wako huyo na shukuru Mungu anakupenda amekuonyesha mapema kabla hujadondoka mzima mzima,sisi wote ni wakosaji hakuna aliyekamilika hata mmoja,hilo ni funzo kwako na kwetu pia huwezi kujicommit asilimia zote kwa mtu unayemfahamu kwenye keyboard,zipo kanuni za upendo na katika huo upendo zipo hatua za kupenda,na katika hilo my kaka ulibugi,so haina haja ya kulalamika sana huwa tunajifunza kupitia makosa.
Narudia tena weka hasira pembeni maisha yaendelee,hii hasira uliyonayo iwe chachu bora ya kuwa makini zaidi ya kumchagua umpendaye,hasira hii take it positively utakuja shangaa how good you are,unavyoendeleza hasira na chuki hapa hautendei haki moyo wako,please achana na hii kitu usijibu tena quotes za watu namna hiyo.