Naomba kujua kosa langu Wana jamvi

Naomba kujua kosa langu Wana jamvi

THANK GOD! This is more like you! Kule kwa wapiga manyanga ya mganga kushadadia ubuyu mwanamke mwenzio anaanikwa WAS NOT LIKE YOU KABISAAA. Kuna wenyewe team USHUZI.

Hahahaha!!! Asante sana, kweli ubuyu una wenyewe Leo kulamba tu umenitoa nishai!!,ila mimi toka mwanzo nilimsihi asiseme aachane na hizo habari
 
Kumbe hii mada ishaisha maskini weee jamani hajatokeza leo hata kuchangia.
 
Mmmh! Ni bora tu ungemtaja ili tusikie na kutoka kwake anajiteteaje (if she loves u)!
 
Masai dada upo TGTS ipi nikuunge ukope Gari uepukane na kadhia hizi za Ku boost betri shoga yangu...!!??
 
huyo demu Pasua kichwa cancel usitafute proglam zisizo za msingi ukaanza data
 
Haya si mambo ya chumbani kwani nini mtu analalmika kwa threads nyingi za uongo na kuonekana ni mwema

Pia this is life bhana unajua nime sacrifice nini hadi niyatende hayo ninayo amini ni upendo
Na nimesema hivyo hata wengine wajifunze na wapo waliojifunza hebu kamwambie akusimulie ukweli then uje utueleze

Huwezi kuwa kimya wakati unajua hujatenda lolote na unapewa shutuma,Hebu muite aje nadhani umemjua

Hebu acha ushamba na utoto, that is ur private business.
 
Asilimia kubwa ya wanawake hapa jf wanamtetea huyu mjinga sijajua ni kwa nini, mleta mada kaomba ushauri ili ajue kosa lake liko wapi ili kwa mara ya pili asirundie tena,

ni wachache sana waliomshauri lakn wengine wote mnarukaruka tu, kosa la mtoa mada liko wapi??

Mkuu, huyu mleta uzi tayari amejiharibia hapa jf na kila atakapo gusa azima atatoswa na mdada kwa kuhofia kuanzishiwa uzi.
Minaona amtaje tu kwakua ameshaanza kumwaga ubuyu hahaaa..... Jf bhana....
 
Habari wana jamvi

Naomba ushauri wa kutambua Kosa langu katika hili labda naweza jifunza na kuomba msamaha

Nilipendezewa kiukweli sana na binti mmoja mwana jamvi humu nikaanza kumtokea lakini alinieleza kuwa ana yupo likizo ktk mahusiano ya kimapenzi kwa sasa.

Niliendelea kumshawishi ili aweze kumaliza hiyo likizo na kumuahidi sita mpa majonzi ya kumfanya achukue likizo tena.

Hakukubali direct ila tuliendelea kuchati kwa muda mrefu tu na tulikuwa tukiwasiliana hadi muda wa kulala tunaagana ndo kila mtu ana lala,nilipenda kumuandikia sms nikiishia na neno Mpz lakini alisema mimi sio mpz wako bado.Mimi nilimwambia sawa japo halidhuru chochote basi nitakuwa nikiandika sms siliandiki na badala yake nikifika sehemu ya kuandika nitaja kimoyoni tu halafu naendelea.

Tuliwasiliana kwa muda lakini hakuwa Daresalaam alikuwa ameenda Mkoani bt siku moja alianza kucharuka na kusema mbona siku hizi nimebadilika na simuiti mpz tena hata simu sipigi.

Nilijitetea kuwa nilikupigia mbona Mara moja akasema mwanzo ulikuwa unapiga Mara tatu sasa umepunguza Mimi nikaona isiwe mada nikaomba radhi akakubali tukaendelea na mawasiliano.

Siku moja aliniambia ujue Mimi nina mtoto nikamuuliza baba yake yupo wapi akasema amenitelekeza nikamwambia pole but maisha yanawezekana pia bila huyo baba yake.akasema ni kweli hadi sasa mtoto ana miaka 3 ana mlea mwenyewe nikasema hongera kwa uvumilivu na kuamua.

Tuliendelea na mazungumzo ila siku moja tarehe kama 30/12/2014 tukiwa tunachati ghafla niliona kaniblock watsapp nikamwandikia sms kawaida nikamuuliza kulikoni hakujibu!!nilikuja kumpigia saa tano usiku akawa ana kata na baadae alituma sms na kusema hawezi pokea Simu amelala na mtoto ataamka nikakubali na kesho yake akaendelea kuwa kimya.

Aliniambia ana taraji kurudi tarehe 1/1/2015 kwa kuwa ni mwalimu wa shule moja hivi lakini kwa kuwa hakuwa anawasiliana nami tena niliamua kupotezea tu,Leo majira ya saa nne asb nikaona sms yake on my way!!nikamwambia umeanza safari ya kuja akasema ndio basi nikamwambia karibu sikutaka kukumbusha yale .


Tuliendelea kuwasiliana hadi alipofika nikaenda kumpokea baadae nilimuambia vipi ulisema unakuja na mwanao mbona hujaja nae akasema hana dada wa kazi ameamua kumuacha na mama yake baadae aliniuliza una mtoto nikamwambia ndio akasema hawezi olewa na mwanaume mwenye mtoto nilimuambia kwa nini aksema huwa mna kumbushia nikasema Jf Leo kulikuwa na Uzi wa hii mada na ulikuwa unachangia kuonesha inawezekana Leo vipi akasema hayo ni mamabo ya mtandaoni siwezi kuzungumzia

Tukaendelea na safari nikawa nimepigiwa Simu na dada yangu mmoja nikaongea nae na baadae niliongea na Mama wa mwanangu ambaye alinipigia Simu akaanza kuniuliza mwanao ana itwa nani? Nikamwambia akasema na huyo mama yake nikasema ndio akasema mbona mna active communication nikamwambia ni active communication na sio active mapenzi.

Akaanza kuwa mkali na kusema nimshushe njiani kwani hapendi kudanganywa nikamwambia hapo uongo upo wapi?akasema unawezaje kuwa na mpz na ukaongea na ex Wako nikamwambia inawezekana akasema Mimi nilikudanga sina mtoto nilitaka kukupima!!!!???

Najiuliza

1. lengo la kusema ana mtoto ndo kumpima mwanaume?
2. Mbona aliniomba nimtafutie dada wa kazi kwa ajili ya mwanae au alikuwa ana nipima back
3.Mbona nilipopiga simu usiku alisema amelala na mtoto au ndo alikuwa ana nipima?

Najiuliza maswali mengi zaidi ya hayo ?na baadae aliomba nimushushe njiani ila nilimtoa ubungo hadi Mbagala maji matitu kwa umbali huo na alikuwa naelekea chamazi akadai ana boreka na uongo wangu na pretending na ndo maana hawapendi wanaume akaomba kushuka na ikabidi nimshushe japo nilimwambia Leo Luna panya road umewaona nakuonea huruma just nikufikishe karibu na kwako alikataa na nikabidi nishushe na sijui amefika au LA


Nawasilisha naweza mtaja akiridhia na sheria za Jf kama zina ruhusu kwani nimeumia na kuwaza sana which kind of woman is this

Naomba radhi kwa kuwachosha japo lengo langu muelewe kwa kiasi pa kuanzia kunishauri


Regards,
Superbrand

Ana tatizo la afya ya akili,au ameathirika kisaikologia, msaidie akapewe ushauri nasaha au tiba ya afya ya akili, asipokupa ushirikiano WACHANA NAE kabisa kabla hayajakukuta makubwa zaidi, mtiririko Wa maelezo yako unabainisha uwepo Wa psychological disorder.
 
mkomage na nyie kushadadia visichana mnaacha watu wa maana wameelewa maisha can make life with you unakimbilia visissterduu ukute hata sio mwalimu pole yako 'ubungo - mbagala' si mchezo ujueeee

umeongea ukweli ni tatzo kupenda visichana badala yakupenda mwanamke ambaye anajua maisha yakuishi wawili yako vipi
 
Mpaka muda huu sijamjua ni nani ngoja niangalie madada ambao hawajakoment thread hii najua mmoja wapo atakuwa ni yeye
 
mkuu, huyu mleta uzi tayari amejiharibia hapa jf na kila atakapo gusa azima atatoswa na mdada kwa kuhofia kuanzishiwa uzi.
Minaona amtaje tu kwakua ameshaanza kumwaga ubuyu hahaaa..... Jf bhana....

hata demu wako unayemgonga yupo humu jf usidhanie kuwa tunawashobokea mademu wa humu ambao wezi na waongo sana hawana lolote ndo maana hawajaolewa kwa tamaa mbovu za kupenda kudandia treni kwa mbele
 
msuto unakuja, na keki juu na shampeni na amekodiwa mzee yusufu kabisaaa, uzi utaanzishwa na mtuhumiwa. Haiwezekani mwanamke mwenzetu adhalilishe hivi. Hicho kichambo fungua mwaka. Cc amu

ndo maana nasemaga wanawake wote akili zenu zinafanana sasa unamtetea nini huyo mwenzio wakati mboga kaimwaga mwenyewe
 
Last edited by a moderator:
hata demu wako unayemgonga yupo humu jf usidhanie kuwa tunawashobokea mademu wa humu ambao wezi na waongo sana hawana lolote ndo maana hawajaolewa kwa tamaa mbovu za kupenda kudandia treni kwa mbele

Aiseeee......2015
 
Back
Top Bottom