Kusaidia watu wawili watatu huku jukwaani hamkufanyi mtu kua great thinker. Kwangu Mimi great thinker ni mtu ambae jamii inanufaika na mchango wake wa moja kwa moja kijamii, kisiasa, kiuchumi na kimaendeleo kwa ujumla. Tuna matatizo mengi sana kwenye hizo angles nne kwenye nchi yetu. Sasa kama mtu anatoa mawazo humu with hiden identity na huku tuko wachache tu, kuna jamii kubwa nje ya hili jukwaa inasuffer vibaya mno kutokana na changamoto mbali mbali zinazotokana na aina ya siasa tuliyonayo ambayo inaathiri moja kwa moja uchumi na maendeleo yetu kwa ujumla. Kwahiyo mleta mada labda uzi wako uubadilishe uwe "Nani anaweza kutoa ushahidi vile amesaidia jamii inayomzunguka nje ya hili jukwaa kutokana mchango wake wa mawazo humu ndani kuonekana una mashiko sana"? Yani ni sawa tu tumuulize mwanafunzi wa Chuo kua ametumiaje elimu aliyoipata Darasani kutatua changamoto zinazoikabili jamii inayomzunguka kutoka zile A na B+ alizokua anapata kwenye mitihani. Otherwise tuendelee kupiga stori zetu zile zile na kuskilizia michongo na mambo mbalimbali yanayoendelea kwenye nchi yetu