Nani mwenye jukumu la kulipa hela ya kunyonya maji ya choo endapo kitajaa kati ya mwenye nyumba na mpangaji

fundi bishoo

JF-Expert Member
Jun 26, 2018
12,955
22,654
Kwema wakuu nataka nilianzishe hapa maana mtu unalipa kodi kila baada ya miezi 6 halafu choo kimejaa, mwenye nyumba hakai hapa lakini je ni nani mwenye jukumu la kulipa wakati sio mwenye nyumba ndo anaestahili kulipa hyo pesa kama shilingi 80,000.

Inakuaje wapangaji tupigishwe mchango wa elfu 10 kila chumba wakuu?
 
Mwenye nyumba, maintance zote za nyumba na mazingira yake inabidi ahusike!! Sema ndo hivyo umkute mtasha ila hawa nyumba za kurithi ni wapuuzi sana!! Niliwahi kuishi nyumba moja faza house alikuwa mzungu sana hata kitasa kikipata shida ni gharama zake!!!

Pia alikua anaishi mbali na pale walau kila baada ya miezi kadhaa alikuwa anakuja kutatua changamoto!!
 
kwema wakuu nataka nilianzishe hapa maana mtu unalipa kodi kila baada ya miezi 6 halafu choo kimejaa mwenye nyumba hakai hapa lakini je ni nani mwenye jukumu la kulipa wakati sio mwenye nyumba ndo anaestahili kulipa hyo pesa kama shilingi 80,000 inakuaje wapangaji tupigishwe mchango wa elfu 10 kila chumba wakuu....?
Hama nyumba chap
 
Maeneo ya Sinza wana bill za maji masafi, maji taka na umeme. Kwa msingi huo, Bill ya maji taka ndiyo hiyo ya kuita gari la kunyonya hizo septic tanks.

Lakini sehemu nyingi hazina huo mfumo wa maji taka kwenda baharini. Mashimo ya vyoo au septic tanks na kimazoea bill imekuwa ikibebwa na mwenye nyumba.
 
Back
Top Bottom