Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Wakuu,

Katika harakati za kutafuta nyumba kwa ajili ya shughuli mbalimbali madalali wamekuwa wakitumika kufanikisha jambo hilo. Wenye nyumba hutafuta madalali ili kuweka wepesi katika kupata wateja, na imekuwa rahisi kwa wapangaji kufikia maeneo hayo kirahisi kupitia madalali.

Ambapo, baada ya kufanikisha zoezi la kupata mteja mpangaji anatakiwa kulipa kodi ya mwezi mmoja kwa dalali kama ujira wake, na asipolipa atafanyiwa figisu mpaka ashindwe kupata sehemu hiyo au ataletewa mtu mwingine na yeye kulazimika kuhama

Sasa swali linakuja hapa, nani anatakiwa kulipa ujira wa dalali? Kama dalali amepewa kazi na mwenye nyumba kwanini ujira alipe mpangaji? Kwanini asilipe mwenye nyumba aliyetoa shavu hilo kwa dalali?

Swali la nyongeza, kwanini mpangaji atakiwe kulipa kodi ya mwezi mmoja? Yaani gharama ile ile kwa mwenye mali inatakiwa iende sawa na kwa aliyetoa taarifa juu ya uwepo wake!

Ina maana imekosekana kabisa njia ya kumpa mpangaji unafuu na kumpunguzia, ikiwezekana kumuondolea kabisa mzigo huo? Lukuvi akiwa Waziri wa Ardhi alipiga marufuku madalali kuwadai wapangaji kodi ya mwezi mmoj akiita kitendo hiko kuwa ni ujambazi, akisema mwenye nyumba ndio alipe pesa hiyo.

Katazo hili liliishia wapi? Ilikuwa ni kauli tu ya kisiasa kufurahisha watu huku wakiaacha wananchi waendelee kuumia?

Wakuu mnazungumziaje suala hili.
 
Wewe wakati unataka nyumba ulienda kwa mwenye nyumba akupangishe au ulienda kwa dalali akutafutie nyumba ya kupanga?

Kama ulienda kwa dalali akutafutie nyumba sharti umlipe gharama za kukutaftia nyumba.

Na kama ulitafuta mwenyewe nyumba bila kumshirikisha dalali ukapata, hutalipa hizo gharama, maana dalali hatakuwepo.
 
Wewe wakati unataka nyumba ulienda kwa mwenye nyumba akupangishe au ulienda kwa dalali akutafutie nyumba ya kupanga?

Kama ulienda kwa dalali akutafutie nyumba sharti umlipe gharama za kukutaftia nyumba.

Na kama ulitafuta mwenyewe nyumba bila kumshirikisha dalali ukapata, hutalipa hizo gharama, maana dalali hatakuwepo.
🤔🤔 nani anamuweka dalali? Tuanzie hapo... nyumba nyingine ukienda wenye nyumba anakabidhi kia kitu kwa dalali yaani hataki kudeal na wapangaji, hili unalizungumziaje?
 
Back
Top Bottom