Nani mmiliki wa jengo la TANESCO Ubungo?

Nani mmiliki wa jengo la TANESCO Ubungo?

Inasemekana jengo hilo limeingia kwenye road reserve

Ova
Sasa siwaliambie litoke?, wakati linajongea mpaka likaingia walikua wapi?.
Kulibomoa sio suluhisho wamuulize mlinzi aliyelifungulia get.
 
Hili ni mali ya Tanesco na ndio maana wakali brand na rangi zao.
Tanesco wanalo jengo mjini Samora Avenue na walihamisha makao yao baada ya kujenga hilo jengo.
Haya mengine ni ya mitaani tu.
Kuvunja hili jengo ni hasara kwa serikali tena kubwa. Hili jengo ni limetumia billions kulijenga hivyo mbomoaji hayo yeye hajali bali bomoa bomoa tu.
Kuna njia nyingi za kufanya kupitishia flyover kuli save hilo jengo. Ila Akili ni nywele kila mtu ana zake !
 
Halijulikani mmiliki ndiyo maana linapigwa chini! Labda angetoa siku saba aletewe ripoti ni la nani!
 
Kama kuna mtu Ana taka kiki Kama Dr shika awe star Aende pale tanesco anadai yeye ndiyo mmiliki wa jengo hilo

Ova
 
Wandugu salama,
Kuna ukweli wowote kwenye hili, hapa nilipo kuna malumbano yanaendelea juu ya nani mmiliki wa lile jengo la makao makuu ya TANESCO pale ubungo, pia inasemekana kutokuwa mali ya serikali ndio sababu iliyomfanya Magufuli kutaka kulibomoa ili kumkomoa mmiliki.

Je, wadau kuna ukweli wowote kwenye hili?

hilo swali kawa hulize wakazi wa ubungo mpaka mbezi mwisho,walio kando kando na barabara.
 
Screenshot_20171128-093838.png
 
Duh? Hata kama sio la serikali ndo ubomoe rasilimali ya pesa mingi ivo? Si bora kulitaifisha sasa kama wanataka kukomoana. Kuchukua maamuzi ya "tukose wote" ni utoto!
Sio utoto ni upumbavu
 
Duh, huu ulikua uongo mtupu, kimara, mbezi watu wamebomolewa bila kulipwa fidia
Mtu mwenye tittle deed na building permit, hawezi kuvunjiwa bila fidia!, naasume, wengi wa waliovunjiwa bila fidia ni vendors tuu, ambao waliishi hapo miaka mingi bila hati. bila building permits.
Hata hivyo, niliwahakikishia, wote waliovunjiwa bila fidia, lazima watafidiwa tuu, na nimesisitiza hapa
Kama Hii Ndio Situation ya Bomoa Bomoa ya Ubungo na Kimara Bila Fidia, Then Faraja Pekee ni Kuwa, Watafidiwa Tuu!.
Paskali
 
Kiwanja ni cha Tanesco hivyo Jengo ni la Tanesco ila the developer ni PPF.

Jengo hili lilijengwa kwa mujibu wa sheria ya zamani. Kwa majibu wa Sheria zamani ya mwaka 1936, kweli jengo liko kwenye road reserve. Sheria mpya ya Ardhi 1999, ilifuta sheria ya 1936 na kupunguza road reserve, na ile ya 1936 ikaja kuchomekewa tena mwaka 2007 hivyo sehemu ya jengo hilo kuingizwa kwenye road reserve!.

Sababu ya kuvunjwa kwa jengo hilo ni kitoa fursa kujengwa kwa flyover pale Ubungo na sio kumkomoa yoyote!.

Majengo yote yaliyojengwa kwenye road reserve kabla ya 2007 yanapaswa kufidiwa, hivyo hakuna ukomoaji wowote!.
Update
Kama Hii Ndio Situation ya Bomoa Bomoa ya Ubungo na Kimara Bila Fidia, Then Faraja Pekee ni Kuwa, Watafidiwa Tuu!.

Paskali

Swala Ni hasara ya kulibomoa,
Hekima na busara zinge tumika zaidi, makosa yamshatokea, lingeweza kukwepwa kidogo,
 
Nimesoma comment za watu humu lakini mwisho wa siku kuna ambao walikuwa wanaangalia tu wakati linajengwa achilia mbali watoa vibali vya ujenzi maana ghorofa kama lile lazima lifuate taratibu za ujenzi ikiwa pamoja na vibali tofauti na vijumba vyetu
 
Emmmmhhh tfanye ynayotuhusuuu jamanii mengine tyaache yapiteeeee
 
Back
Top Bottom