Nani mmiliki wa jengo la TANESCO Ubungo?

Nani mmiliki wa jengo la TANESCO Ubungo?

Duh? Hata kama sio la serikali ndo ubomoe rasilimali ya pesa mingi ivo? Si bora kulitaifisha sasa kama wanataka kukomoana. Kuchukua maamuzi ya "tukose wote" ni utoto!
Sheria inasema jengo likijengwa road reserved area litaifishwe?
 
Kama Jengo ni mali ya TANESCO basi uamuzi wa kulibomoa uzingatiwe upya kwani kulibomoa ni sawa na kutumbukiza pesa kwenye choo cha shimo. Kwa hili wahusika wapunguze mihemko.
Halafu daraja lipite wapi?
 
So serikali imejipanga kutapanya mabilioni kadhaa kwa mmiliki!!kupanga nikuchagua lakini hakuna muda tukaamua kutafuta namna yakuokoa pesa za walipa kodi kabla ya kufanya maamuzi ya awali na mahitimisho yake??
Hakuna ndio maana linabomolewa.
 
Kwenye ujenzi huu, wengi wanaona jengo tuu la tanesco tuu, halivunjwi lote bali lile la mbele tuu. Lakini ile miundombinu ya DRT, ambayo inavunjwa yote, watu hawaioni na imecost more jengo la Tanesco na hardly ina 5 years!. Kiukweli Watanzania ni watu wa ajabu sana katika mipango miji na upangaji vipaumbele vyetu. Kama plan ya Ubungo interchange imekuwepo more than 10 years kabla ya BRT, kwa nini serikali imespend 20 billions kujenga BRT kisha kuja kubomolewa less than 5 years!.

Paskali
Mbona DRT walisema halivunjwi?
 
Hivi haya maghorofa yanayojengwa kila siku hii Bagamoyo road, kutokea town all the way hadi Sayansi hayako kwenye hifadhi ya barabara kweli au ndiyo tujiandae kwa bomoabomoa na kulipana fidia miaka ijayo?
Hakuna fidia kwenye road reserved na unabomoa kwa gharama zako.
 
Back
Top Bottom