Nani mkali kati ya Diblo Dibala na Dally Kimoko

Nani mkali kati ya Diblo Dibala na Dally Kimoko

Huna lolote. Nimekuwa mwanamuziki kwa zaidi ya miaka thelathini na tano kwa hiyo ninafahamu ninachoongea. Sisimuliwi na mtu. Huwezi kumfananisha Tosh na wapiga solo mahiri wa Congo, kwa mfano Dally na Diblo, kwa vyovyote vile. Tosh alikuwa anapiga rhythm guitar na sio solo (labda hujui tofauti). Mpiga solo mahiri toka Jamaica enzi hizo alikuwa Junior Marvin, na bado anaendelea kwa sasa. Tosh hamfikii hata chembe mpiga rhythm Lokassa ya Mbongo. Yaani ukijiita ras ndio unaona umekuwa bingwa wa reggae na historia yake? Tosh alikuwa mpiga guitar wa kawaida sana. Heshima kubwa aliyokuwa nayo Tosh ni katika utunzi, uimbaji na uanaharakati, hilo sibishi. Wewe inaonekana ni mtu wa kusimuliwa, ndio maana unakimbilia google kupata historia. Nimeishi enzi za Tosh na Bob sihitaji kusimuliwa.
Mpe huyo. Muongeze , muongeze akija mkoleze. kumbe tupo na babu zetu humu. miaka 30 kwenye game si mchezo
 
Bora ungemlinganisha dalik moko na lukasa ya mbongo ila diblo kwa hawa anasubiri saana

Ni Lokasa ya Mbongo na siyo Lukasa ya Mbongo Mkuu. au Wewe ni Mnyakyusa akina Lukasa hivyo unataka kuhalalisha kiulazima kuwa Lokasa ni wa Kwenu na siyo Mzairwaaaa ( Mkongoman ) ?
 
Mosi,Hakuna wimbo hata m,moja wa Allan Konkou ambao solo ilipigwa na Didlo Dibala...

Pili,Jean Baron alipigiwa nyimbo chache sana na Diblo Dibala na wimbo maarufu wa Pardon kapiga solo Diblo Dibala lakini nyimbo kali zaidi na zilizovuma kama PANTALON MORIBA na KOUDIA NDAMBOU,solo kapiga Dally Kimoko....

Ishu hii iko pia kwa Aurus Mabele na kundi lake la Loketo ambalo Jean Baron alikuwa ni mmoja wa wanamuziki wa kundi hilo akiwemo Awilo Longomba na akina balou Kanta na Lucien Bokilo ambako zipo nyimbo chache ambazo solo alipiga Diblo Dibala lakini nyimbo nyingi alipiga Dally Kimoko na baadaye alikuja mtu mmoja anayeitwa Cayen Madoka ambaye alimpigia pia Mack Makaire ambaye naye aliwahi kuwa mwanamuziki wa Loketo ya Aurus Mabele....

Kwenye Soukous Stars sijui unaizungumzia ipi,lakini ile ya mwaka 1996 ambayo ilikuwa na wanamuziki Ngouma Lokito,Yondo "baby" Sister,Shimita,Balou Kanta,Lucien Bokilo,Saladin Wizoo na Lokasa ya Mbongo,solo ya kwenye nyimbo zote hakupiga huyo Diblo maana walikuwa na mpiga solo hatari anayekwenda kwa jina la Saladin Ferreira "Wizoo" na ukitaka kusikia solo yake sikiliza wimbo unaitwa "Abba Guimo" ambao yeye mwenyewe ni mtunzi au sikiliza wimbo wa Yondo Sister unaitwa Derniere Minute....

Kwa ujumla wa hoja yako na wanamuziki uliowataja siyo kweli solo kapiga Diblo Dibala kwa ujumla wake bali kapiga baadhi tu....

Umetisha mzee. Agiza nakuja kulipa
 
Dally kimoja ni mtaalamu wa kuchenjua gitaa la solo enzi hizo.aleeh!tomboka nakobita te mokolo mosusu ngai te
 
Msaada kwenye tuta:

Kuna wimbo nadhani umeimbwa na Franco, ila nimeusahau jina ni wimbo ambao ndani kuna sauti ya huyo mwimbaji na mwanamke mmoja ambae anaimbiwa arudi nyumbani baada ya kuondoka kwa mmewe.

Kinaimbwa kifaransa kwenye huo wimbo, ila yule mwanamke anaonekana yuko mbali sasa franco anampigia simu inaita ngiriiiiii ngiriii ngiriiii anaongea kifaransa hapo na yule mama anajibu.

Napenda sana huo wimbo Nani mwenye kuujua anisaidie jina la huo wimbo niutafute.
 
Msaada kwenye tuta:

Kuna wimbo nadhani umeimbwa na Franco, ila nimeusahau jina ni wimbo ambao ndani kuna sauti ya huyo mwimbaji na mwanamke mmoja ambae anaimbiwa arudi nyumbani baada ya kuondoka kwa mmewe.

Kinaimbwa kifaransa kwenye huo wimbo, ila yule mwanamke anaonekana yuko mbali sasa franco anampigia simu inaita ngiriiiiii ngiriii ngiriiii anaongea kifaransa hapo na yule mama anajibu.

Napenda sana huo wimbo Nani mwenye kuujua anisaidie jina la huo wimbo niutafute.
Unaitwa mamou umeimbwa kwa kilingala na sio kifaransa
 
Back
Top Bottom